Paul Makonda alitakiwa akabidhi Ofisi leo, zoezi limeahirishwa hadi Jumatatu. Je, Makonda atakanusha kugombea Kigamboni kupitia ACT-Wazalendo?

Zoezi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kukabidhi ofisi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa huo wa sasa Aboubakar Kunenge limesogezwa mbele, hadi siku ya Jumatatu baada ya ratiba hiyo kuingiliana na ratiba zingine.


Taarifa ya kuahirishwa kwa zoezi hilo, imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, ambapo hii leo Agosti Mosi, Makonda alitarajiwa kukabidhi ofisi hiyo iliyopo maeneo ya Ilala, majira ya saa 7:00 mchana.

Makonda aliondolewa kwenye nafasi hiyo siku ya Julai 15, 2020, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, na nafasi hiyo ilichukuliwa na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo.

Machi 13, 2016, Rais Magufuli alimteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo awali kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na hivyo amehudumu kwenye nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa zaidi ya miaka mitatu.
 
Nakumbuka ya Laulent Masha Jimbo la nyamagana wakati ana mkabidhi Wenje ofisi .
 
  • Thanks
Reactions: amu
Haaa haaa baba kegan ataki kutoa ufunguo, ndio maana juzi alipost thinking kumbe anafirikilia atoe funguoa asitoe kazi kweli kweli
 
New Big fish in town Tutaelewana tu

Makondakta huu mwaka hatokuja kuusahau
 
Hapana, kwa sababu kama hilo lingekuwa issue asingeenda kuomba kura kwa Wajumbe kigamboni, makonda ni optimistic which is good character ya leadership tatizo linalomgharimu ni ulimbukeni, dharau na kujisahau
Anajisahau mno hajui kama kuna kesho, hivi yule wa Iringa sijui vp yupo kweli?
 
Inawezekana Makonda, alijua siku zake za kuwa RC zinahesabika.
Ndio maana akaamua kukimbilia kwenye Ubunge.?
 
Huyo hana jeuri ya kuhama chama, hapo alipo ndio kichaka alimojificha kuepuka kukamatwa kutokana na maovu mengi aliyotenda.

Nje ya hapo atakuwa kama nyoka aliyeingia mjini.
 
Salaam Mkuu,

Sasa Wiki mbili zimeisha baada ya aliyekuwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar kutenguliwa Cheo chake hicho baada ya yeye kuamua kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni ambapo kura zake hazikutosha.

Lakini tangu kipindi hicho hajakabidhi Funguo za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Mteule mpya.

Kabla ya Jumatatu anatakiwa awe amekabidhi ofisi kwa Mhe. Aboubakar Kunenge Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar.

Kesho hakuna kazi. Je, leo atakabidhi Ofisi?

Kuna tetesi zinadai anataka ajiunge ACT Wazalendo ili akagombee Kigamboni kama CCM hawatampitisha. Kuna Nzi amesema atamuuliza swali hilo siku ya kukabidhi Ofisi. Yajayo yanafurahisha.

Thread

=====

UPDATES; 1324HRS

Zoezi la kukabidhi Ofisi leo limeahirishwa kutokana na sababu zilizo njena uwezo wa Mkuu wa Mkoa Kunenge. Ratiba imebana sana hivyo itapangwa siku nyingine ikiwezezekana Jumatatu.
Kunenge alikuwa eneo la Karume toka asubuhi.
Huyo Bashite ndiye kazingua, sijui itakuwa alikula nini jana tumbo limemshika mpaka muda huu,.
ama la basi kuna vizizi kasahau kuvitoa, kapihga chenga then kesho anakwenda vitoa ili akabidhi jumatatu.
 
Mwambieni Bashite aachie Ofisi haraka, watu tunashida na mkuu wa mkoa saizi..l
 
Back
Top Bottom