Paul Makonda aagiza kusitishwa utolewaji zabuni kwa kampuni 4 za ujenzi

Habari wanaJF,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mshimiwa Paul Makonda leo amechukua hatua ya kuzisimamisha na kusitisha Kampuni ya Inshinomya Co. LTD na kuyasimamisha Makampuni mengine ya kujenga barabara ya Germinex construction LTD, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction katika Mkoa wa Dar es salaam

Hii ni kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni haya kutopewa tenda yeyote kwenye Mkoa wa Dar es salaam mpaka Mkuu wa Mkoa atakapojirizisha na utendaji wa kazi kwa Makampuni hayo.
Habari wanaJF,
"Mpaka atakaporidhishwa na utendaji wa kazi" Sasa atarishwaje wakati kawazuia kupata tender? Hapo ni kwamba wamefutwa kufanya kazi dar 4ever!
 
Hao skol kuna barabara wametengeneza st marrys Tbt lami iligeuka tope baada ya miezi mitatu.
 
katika kazi ambayo ni ya kitaalamu lakini rahisi kuikosoa ni kazi ya ujenzi, daktari anaweza kuua lakini ikawa vigumu kuthibitisha lakini kama mtu amejenga barabara baada ya muda mfupi ina mashimo au inavimba ni rahisi kutoa kasoro.
Ni kweli kuna barabara nyingi Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla zinajengwa chini ya kiwango lakini bodi ya uhandisi inakaa kimya mpaka wasio wahandisi wanakuja kutoa kasoro hivyo hatua ya makonda waichukulie kama changamoto
 
Mwenye mamlaka ya ku black list wazabuni nadhani ni PPRA na si RC. Hivyo makonda ilitakiwa awaandikie hao PPRA wazifute hizo kampuni kuomba kazi serikalini. PPRA wasingebisha ukizingatia kajamaa kana sifa kwa Pombe.
 
Inawezekana kirahisi hivyo? As a government ni muhimu kuwa makini, kwani madai dhidi yake yanaweza yakawa ghali sana! Inakuwaje, kwa nini isiwe aliyetoa zabuni kutangaza mgogoro, na mamlaka kama PPRA ndio wazuiwe wasifikiriwe kwa zabuni zingine. Utawala wa kisheria unatukimbia haraka mno!!!
Acha hoja zako za kifisadi,mbona husemi kitu kwa zile keki walizotengeneza na atalipa
 
Inawezekana kirahisi hivyo? As a government ni muhimu kuwa makini, kwani madai dhidi yake yanaweza yakawa ghali sana! Inakuwaje, kwa nini isiwe aliyetoa zabuni kutangaza mgogoro, na mamlaka kama PPRA ndio wazuiwe wasifikiriwe kwa zabuni zingine. Utawala wa kisheria unatukimbia haraka mno!!!
Utaratibu huu unaumiza ila unamanufaa kwa umma kwani hawakurupuki tu hao viongozi wamefanya tafakuri ya kutosha. Utawala wa sheria kwa Africa unawanufaisha wachache
 
Rekodi ya Makonda hadi sasa:
1. Wamiliki silaha wote wakazihakiki - sijui zoezi limepotelea wapi.
2. Ombaomba wote waondolewe mitaani na warejee makwao - wanadunda mitaani bila ajizi.
3. Waliojenga majengo marefu bila kuyajengea maegesho aidha wajenge maegesho au wayabomoe kabisa hayo majengo - kimya mpaka sasa.
4. Alikamata sukari iliyofichwa kwenye ghala la Mohammed Enterprises - hakuna aliyefikishwa mahakamani hadi leo.
5. Mpango mahususi wa walimu kupanda daladala bure - umeyeyuka ghafla.
6. Wakazi wa jiji la Dar es Salaam kufanya usafi wa mazingira na maeneo wanayoishi kwa utaratibu endelevu - mpango umetowekea hewani huu.

Mengine siyakumbuki, hivyo msihofu hizo kampuni zitaendelea kufanya kazi kama zinamsukuma mlevi.
 
Dah, kwani mkandarasi ndo anayejenga vibaya? kwa mradi wa design and build unaweza kumlalamikia mkandarasi, lakini kwa miradi ya build pekee mkandarasi anakua hana kosa ukizingatia ayefanya design na ku approval materials ni consultant. Hofu yangu kama amechukua maamuzi kisiasa ataisababishia jiji hasara kubwa kutokana na claims.
Kuna claim gani hapa? Unachokiongea hukijui! Tulia
 
Kabla ya kujadili chochote, kumbukeni Makonda ni " Client"

Kwenye kazi za "selective" ni rahisi kuwalima hao wakandarasi na ndio ilikuwa njia pekee ya wao kupata kazi!
 
Naona mkuu anawaelewa zaidi Estim construction. But akumbuke kuwa makosa ni ya designer aliyetoa spec za kuweka leya moja ya lami badala ya angalau leya mbili.
Lakini pia mkuu wa mkoa ana mantiki maana Skol wamejenga barabara ya Segerea na haina hata miaka mitatu bara bara yote now ina viraka.
Hongera Makonda kwa kuliona hili.

barabara pia hua zinakua designed kukidhi muda flani alafu baada ya hapo inafanyiwa maintanance. kwa nchi kama tanzania nyingi wanazi design za miaka 10, mi 5 au pungufu ili kutumia pesa kdg kwenye ujenzi wake.. "ufinyu wa budget".. ss usishangae kuharibika ndani ya miaka mi 3. apo hatujaongelea misuse "tonne za magari".. nk nk..
 
Back
Top Bottom