Paul Makonda aagiza kusitishwa utolewaji zabuni kwa kampuni 4 za ujenzi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Habari wanaJF,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mshimiwa Paul Makonda leo amechukua hatua ya kuzisimamisha na kusitisha Kampuni ya Inshinomya Co. LTD na kuyasimamisha Makampuni mengine ya kujenga barabara ya Germinex construction LTD, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction katika Mkoa wa Dar es salaam

Hii ni kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni haya kutopewa tenda yeyote kwenye Mkoa wa Dar es salaam mpaka Mkuu wa Mkoa atakapojirizisha na utendaji wa kazi kwa Makampuni hayo.
 
Habari wanaJF,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam meshimiwa Poul Makonda leo amechukua hatua ya kuzisimamisha na kusitisha Kampuni ya Inshinomya Co. LTD na kuyasimamisha Makampuni mengine ya kujenga barabara ya Germinex construction LTD, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction katika Mkoa wa Dar es salaam

Hii ni kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni haya kutopewa tenda yeyote kwenye Mkoa wa Dar es salaam mpaka Mkuu wa Mkoa atakapojirizisha na utendaji wa kazi kwa Makampuni hayo.
Inawezekana kirahisi hivyo? As a government ni muhimu kuwa makini, kwani madai dhidi yake yanaweza yakawa ghali sana! Inakuwaje, kwa nini isiwe aliyetoa zabuni kutangaza mgogoro, na mamlaka kama PPRA ndio wazuiwe wasifikiriwe kwa zabuni zingine. Utawala wa kisheria unatukimbia haraka mno!!!
 
Dah, kwani mkandarasi ndo anayejenga vibaya? kwa mradi wa design and build unaweza kumlalamikia mkandarasi, lakini kwa miradi ya build pekee mkandarasi anakua hana kosa ukizingatia ayefanya design na ku approval materials ni consultant. Hofu yangu kama amechukua maamuzi kisiasa ataisababishia jiji hasara kubwa kutokana na claims.
 
Katika makampuni ya kizalendo skol ni miongoni mwa makampuni yenye mitambo mingi sana. Kuifungia ni kukurupuka, njia nyingine ingetumika kutatua tatizo litokanalo na ubora hafifu kwa baadhi ya kazi.

Vifungu vya mikataba viwe vinasomwa vyote maana vipo vinavyoeleza ikiwa kutatokea mapungufu toka upande wowote wa wadau wa mkataba husika.

Nchi tunaiharibu.
 
Kuna kampuni moja inaitwa Tanzania Building Works kama sijakosea,iliwahi kulalamikiwa sana bungeni kwamba ilikuwa inapewa zabuni inachukua pesa lakini haimalizi kazi na baadaye inakwenda kushtaki.Ilifanya hivyo kwa jiji la Mbeya na Mwanza,sijui ilifikia wapi
 
Mikataba inasemaje. Nazan kwenye mikataba ya ujenzi kuna kipengele cha deffects liability period.
Vipi kuhusu consultant na wao kawafungia.. Mana contractor halipwi bila kazi yake kukaguliwa na consultant na project manager ambaye anamuwakilisha client. Vipi na hao amewatimua. Ngoja tuone hyo series mpya..
 
Inawezekana kirahisi hivyo? As a government ni muhimu kuwa makini, kwani madai dhidi yake yanaweza yakawa ghali sana! Inakuwaje, kwa nini isiwe aliyetoa zabuni kutangaza mgogoro, na mamlaka kama PPRA ndio wazuiwe wasifikiriwe kwa zabuni zingine. Utawala wa kisheria unatukimbia haraka mno!!!
yeye ni mtaalamu wa ujenzi wa barabara? wamepewa nafasi ya kujitetea. Mtalipa fidia mpaka mtafilisika. wafyrahishe wanaowahusudu!
 
Kuna bodi ya Usajili ya Wakandarasi(Contractors Registration Board , kuna PPRA kuna Tanzania Building Agency, hizi ndizo taasisi za kusemea hili.

1. Kuna faida gani za kuinyima kampuni zabuni Dar es salaam kama bado inaweza pata zabuni Morogoro na mikoa mingine?!

2. Kuna faida gani ya kuinyima kampuni zabuni huku bado ikiwa na usajili usio na mashaka kisheria?

3. Inawezekana ni kweli wameharibu lakini ilipaswa hatua zipitie kwenye taasisi/bodi ambazo kampuni hizi zinawajibika kwazo.

Kesho Makonda asipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kampuni hizi zitaendelea na kazi za mkoa wa Dar es Salaam.

Ifike wakati tufanye mambo kwa manufaa, hizo kampuni zitanyimwa tenda za mkoa wa Dar es Salaam ila bado zinaruhusa kufanya kazi ndani ya Dar es salaam kwa kazi ambazo sio za serikali ya mkoa wa Dar es salaam.

Kilichopaswa kufanywa ni kujiridhisha kuwa kampuni hizi hazikidhi viwango vya kufanya kazi hivyo aidha zisimamishwe au kufutiwa usajili na taasisi ilizozisajili na sio matamko ya aina hii.

CRB, PPRA na TBA mpo?!
 
hapa sasa naona watu wa JF mnaanza kupotoka, yaani huyu kanona madudu mengi sana , hawa hawafai kabisa, barabara miezi minne tu imebomoka
 
Habari wanaJF,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mshimiwa Paul Makonda leo amechukua hatua ya kuzisimamisha na kusitisha Kampuni ya Inshinomya Co. LTD na kuyasimamisha Makampuni mengine ya kujenga barabara ya Germinex construction LTD, Del Monte (T) Ltd na Skol Building Contraction katika Mkoa wa Dar es salaam

Hii ni kutokana na kujenga barabara chini ya kiwango na kuagiza makampuni haya kutopewa tenda yeyote kwenye Mkoa wa Dar es salaam mpaka Mkuu wa Mkoa atakapojirizisha na utendaji wa kazi kwa Makampuni hayo.
Habari wanaJF,
Hivi wakuu wa mikoa nao ni waheshimiwa? Nijuavyo mimi mheshimiwa ni yule anayechaguliwa na wananchi na siyo anayeteuliwa.
 
Ngoja nipambane nimalize digrii yangu ya sheria kabla mihemko haijaisha,naona pesa zinanipita bure.....hapa kuna mawakili watalamba pesa mingi kwa kufungua kesi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom