Paul Kagame mkimbizi aliyepitia mengi hatimae kuwa rais wa Rwanda

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
1127712

1127716


1127717


SIMULIZI YA RAIS PAUL KAGAME: MKIMBIZI ALIYEONJA JOTO YA JIWE NA KUWA RAIS WA RWANDA ( SEHEMU YA 1)
Na,
BRIGHT KAROLI.

Ijapokuwa ni mmoja kati ya mwanajumuiya ya Watusi, ameonekana kuunganisha Utusi wake. Huyu ndiye mhusika mkuu wa kuondosha Uhutu na Utusi na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo (Mauaji ya kimbari ya Rwanda).
Hata hivyo, mara nyingi anatazamwa kama dikteta kwa kuwa na rekodi mbaya ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Naam...! Huyu si mwingine bali, namzungumzia PAUL KAGAME.
Kagame ameweka kipaumbele katika maendeleo ya taifa, akilenga kufanya Rwanda isiwe tena kati ya nchi maskini kufikia mwaka 2020. Kweli nchi imepiga hatua kubwa katika masuala mengi, kama vile afya, teknolojia na elimu. Kati ya miaka 2004 na 2010 pato liliongezeka 8% kwa mwaka.
Uhusiano na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo si mzuri, hata baada ya vita kusimamishwa rasmi mwaka 2003; asasi za kutetea haki za binadamu zinadai Rwanda inaendelea kutegemeza makundi ya waasi ili kufaidika na maliasili ya nchi hiyo jirani, ingawa Kagame anakanusha.

JE, PAUL KAGAME NI NANI HASA?
Paul Kagame alizaliwa tarehe 23 October 1957, akiwa mtoto wa mwisho ( Kitindamimba) kwenye familia ya watoto sita huko Tambwe, ambayo kwa sasa inajulikana kama Gitarama., sehemu mmojawapo ya Jimbo la kusini mwa nchi ya Rwanda. Baba yake, Deogratias ambaye kwa asili anatoka katika kabila la Watutsi, alikuwa anatoka katika familia mmojawapo ya watawala ( royal family) wa kabila hilo waliotawala kuanzia karne ya kumi na nane. Kwa maana hiyo, Deogratias alikuwa na ukoo na Mfalme Mutara III, lakini aliamua kujihusisha na biashara na hivyo kuachana na masuala ya Uongozi wa kabila lake kama ilivyokuwa kwa familia nyingi za kifalme barani Afrika.] Pia mama yake, Asteria Rutagambwa, naye alitoka katika familia ya malkia wa zamani wa Rwanda, Rosalie Gicanda. Wakati Kagame anazaliwa, nchi ya Rwanda ilikuwa chini ya Uangalizi wa Umoja wa mataifa (Trust Territory) ikiwa imekabidhiwa mikononi mwa Wabeligiji. Kipindi hicho Rwanda ilikuwa na makabila matatu ambayo yalikuwa ni Watutsi ( wachache lakini waliopewa nafasi ya kushika nafasi za uongozi katika serikali ya Wabeligiji,na hivyo kuonekana kabila bora lenye ushawishi katika nyanja muhimu), Wahutu, ( hawa walikuwa wengi lakini wakulima ambao hawakupendelewa na Wabelgiji kama Watutsi), wa mwisho ni Watwa (hawa walikuwa kabila la mbirikimo ambao makazi yao ilikuwa msituni, ambao idadi yao siyo wengi; ni chini ya asimilia moja ya raia wote wa Rwanda).
Mgogoro wa kivita kati ya makabila mawili ya Wahutu na Watutsi ulianza miaka ya 1950 na hatimaye na kuanza kupamba moto mnamo mwaka 1959( Rwandan Revolution; ambapo vikundi vya wahutu wenye chuki dhidi ya Watutsi vilianza kuwaua Watutsi na hivyo kuwalazimisha Watutsi zaidi ya 100,000 kuyakimbia makazi yao huku wakikimbilia nchi za jirani kama Uganda.Paul Kagame akiwa na umri wa miaka miwili, familia yake ilikuwa mojawapo ya maelfu ya familia zilizoyakimbia makazi yake nchini Rwanda.
Kipindi hicho kulikuwepo na bibi mjane, aliyeaminika kuwa na nguvu za kichawi. Bibi huyo alikuwa anaitwa Zura Karuhimbi. Zura Karuhimbi alikuwa anaishi kwenye nyumba ya jadi yenye vyumba viwili tu. Lakini nyumba hiyo iliokoa maisha ya wakimbizi 100 waliokuwa hatarini kuuawa kipindi chote cha vita ya Rwanda, hususani watoto wadogo kwani walifichwa kwenye hiyo nyumba. Karuhimbi alikuwa anaogopwa sana kwa kuwa nyumba yake aliipaka dawa za kienyeji, hivyo hakuna mpiganaji wa Kihutu aliyethubutu kuingia ili kusaka wakimbizi wa Kitusi, vinginevyo wangekuwa wanajitafutia matatizo. Zura Karuhimbi alisikika akisema kwamba, siku moja mwaka 1959 alichomoa shanga za mkufu wake shingoni akazifunga kwenye nywele za mtoto wa kiume wa miaka miwili ili kuwakwepa wapiganaji wa Kihutu na endapo wangemwona wajue ni msichana kwani watoto wa kiume waliuawa sana. Huyo mtoto baadaye alikuja kugundulika baadaye kwamba alikuwa ni Paul Kagame.
Hivyo, familia ya akina Kagame ilikimbia toka kusini na kwenda kaskazini mwa Rwanda ambako waliishi kwa miaka miwili na baada ya hapo mwaka 1962, walivuka mpaka na kuingia nchini Uganda, kwenye kambi ya wakimbizi Nshungerezi, iliyopo Toro . Ndio hapa Paul Kagame alikutana na baadhi ya marafiki zake ambao baadaye alikuja kushirikiana nao katika vita ya kuikomboa Uganda chini ya NRA na ile ya kuikomboa Rwanda RPF. Mmojawapo wa marafiki zake wakubwa waliokutana hapa ni Fred Rwigyema. Paul akaanza shule karibu na kambi ya wakimbizi iliyokuwa umbali wa kilometa 16 kutoka kambini. Shule hiyo ya msingi inajulikana kama Rwengoro Primary school alikojifunza lugha ya Kiingereza na tamaduni za Kiganda. Alihitimu masomo yake na kufaulu vizuri, akiwa ameshika nafasi za juu kiwilaya. Mwaka 1972 familia ilihamia eneo linaitwa Gahunge. Paul aliendelea na masomo kwenye shule ya Ntare school. Hapa ndipo Kagame alikutana na Yoweri Kaguta Museveni kwa mara ya kwanza naye akiwa mwanafunzi wa Ntare.
ITAENDELEA.........!
 
NAPATA KICHEFUCHEFU KILA NAPO SIKIA LIKITAJWA JINA LA HUYO GOLILA kagame MUUAJI ,SIJUI KWANINI MNA KALETA JF
MWANDISHI UNACHEKESHA ETI KAONDOA UKABILA WAKATI AMEWAGEUZA WAHUTU KAMA WATUMWA NDANI YA NCHI YAO FANYA UCHUNGUZI KWANZA WA SIFA UNAZO KAPA UKUMBUKE KUTAJA NA KINA HABYARIMANA NA KINA MTIKILA KALIO WANYWA DAMU
 
Maneno kama haya yaliwahi kutamkwa na mmoja wa wabunge wakati wa bunge la katiba (alijikita zaidi upande mmoja wa Muungano) ila alikwishatangulia mbele ya haki (RIP).
Lakini maneno yake yataendelea kuakisi ukweli daima.
 
Back
Top Bottom