Paul Chizi wa ATCL asimamishwa kazi

naona kila waziri ameanza kwa mbwembwe za kusimamisha watu.. Hii kweli itasaidia kusimama kwa hili shirika?

si wanaogopa kuwajibishwa, kumbuka kuna vikao kibao vya bunge kabla ya 2015
 
Naona kuna haja ya kuachana na watu wanaokaimu!
Chizi alikuja juu na ile ndege ya kukodi leo chali vibaya ivyo jamani!
 
Aende na TAZARA na TRL pamoja na bandari kwani kote kumeoza huko!

TAZARA alikuwepo huko akakuta wasafiri wametelekezwa usiku wa manane, eti treni hazina mafuta...ngoja tusubiri nako itakuwaje maana ni taasisi ya serikali mbili.
 
naona kila waziri ameanza kwa mbwembwe za kusimamisha watu.. Hii kweli itasaidia kusimama kwa hili shirika?


Ditto, wanachofanya mawaziri ni sawa kabisa. Hawa wakurugenzi wa mashirika wameota mapembe, wanajiona kama hawagusiki pengine kwa sababu wanateuliwa na rais. Mawaziri wamekuwa kama 'messangers' mbele ya hawa wakurugenzi! Ni ukiniambia ni kwa nini mashirika kama BRELA, TBS, TRL na mengine yanazorota ni kwa sababu wakurugenzi wamebakiwa kuwa miungu watu. Hakuna wa kuwasukuma. Sasa wakae wakijua 'messangers' wana mamlaka.
 
naona kila waziri ameanza kwa mbwembwe za kusimamisha watu.. Hii kweli itasaidia kusimama kwa hili shirika?

Siku katibu Mkuu Bwana Omari Chambo atakaposimamishwa kazi hii wizara itatulia! Mwakyembe awe makini sana na huyu mtu coz ndiye mpika majungu namba moja na aliyeididimiza ATCL! Kumbukumbu zangu zinaonesha wakati wizara hii inatenganishwa na ile ya ujenzi alimkimbia Magufuli coz alijua asingefurukuta kwake! Mwakyembe asipoangalia atalizwa kama Nundu alivyofanyiwa na huyu ktb mkuu kwa kula njama na yule mfutakamba! We haya! tuone!!!!
 
Nilitarajia haya TAZARA NA TRL hope soon utayabomoa tupe raha Mwakyembe!
 
maana shirika limekuwa lina matatizo sana,ni bora timu hiyo ikae pembeni maana hawachelewi kuiangusha ndege kwa kukosa mafuta
 
Mchadema nini tena mmeanza kuchanganyikiwa na utendaji wa serikali sikivu ya CCM.

Achana na mambo ya uchamachama fikiria taifa lako kwanza.Wakipokea rushwa husemi wakisimamisha watu serikali sikivu.

Binafsi nampongeza kiongozi yoyote anayefanya kazi kwa maslahi ya taifa letu bila kujali chama,dini,kabila,rangi na eneo atokako.
 
ah hao wengine wanasimamishwa ila mawaziri waweke watu wao...huwezi kula mahali ambako hamna vijana wako mnaojuana
 
Too bad for them. Lakini kama kuwamwaga kutalinusuru shirika hili, ni sawa.
Swali la uzushi: Mwakyembe kamtoa Chizi kamweka Lusajo, je ni ukabila unafanya kazi?
Lusajo M Lazaro! M=Mwakyembe or any other Mwa....! Itakuwa huyu ndie kampiga jungu CHIZI
 
Tema cheche kaka ili uwadhihirishie watanzania kuwa wewe ni mtendaji na si nguvu ya soda nakuamini kaka na nategemea mengi mazuri kutoka kwako
 
tuone utendaji mpya
wasiishie hapa wafufue shirika liwe endelevu
na pia watuwekee reli kati kati ya miji mikubwa
kama kamweka mtu wa kabila lake sioni shida kama ana viwango vinavotakiwa kiutendaji
 
watu8 woga wangu ni kwamba, tatizo sio kufukuza hawa miungu watu kwenye haya mashirika.. inabidi kwenda mbali zaidi na kuangalia system yote kama inafanya kazi.. Kuwafukuza na kuleta wengine bila kubadilisha system ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
 
Last edited by a moderator:
FJM Nakubaliana na wewe.. Nafikiri tatizo lipo katika utaratibu wa kuwapata hawa viongozi.. Labda turudi nyuma na kujiangalia.. Je hawa watu tunaotaka waendeshe mashirika yetu tunataka wawe wateule wa mtu au wapitie taratibu stahiki za usaili ili tupate watu sahihi watakaoweza kutukwamua?

Haya ni mambo ambayo sasa inabidi tuyapiganie na kuyaingiza katika katiba mpya. Hatutaki wanasiasa wawe na nguvu ya kututeulia watu katika nafasi muhimu kwenye mashirika yanayoshikilia njia zetu kuu za uchumi. wanasiasa waachwe wapige siasa na proffesionals washindanishwe waweze kuendesha haya mashirika yetu.

Tutaamini vipi kwamba Mh. Mwakyembe hatatumia nguvu na uwezo wake kumuweka swahiba wake kwenye hiyo nafasi?
 
Mizizi ya matatizo haitatatuliwa kwa kutaka misifa. Chizi anatoka kwenye aviation industry toka enzi za KIMAFA na Nundu. Kinachofanyika kwa wenye fani yetu, tunaona kama ni kuweka mkokoteni mbele ya punda. Anzia Ikulu hadi hapo wizara ya uchukuzi maamuzi yakitaalamu yanafanyika kisanii. Mbona Katibu Mkuu na kushindwa kwake kuiongoza secta ya uchukuzi haguswi? Jiulizeni ana taaluma gani na katokea wapi? Dokezo tu katokea Madini wakati JK ni waziri wa madini mengine jazia.

Hitimisho ni R.I.P ATCL kwa hasira za JK na mshika wake Mataka
 
Was it necessary taarifa hii kutolewa kwa vyombo vya habari?
Actually hata mimi nimejiuliza swali hili; wasingeweza kusimamishwa bila kuatngazwa? au kuna kanuni inayoelekeza kutangaza kwa vyombo vya habari? Nampenda mwana siasa anayefanya kazi yake kwa umakini mkubwa bila kuhitaji kazi yake ionekane, kwa maana kama kuna tuhuma, sheria itachukua mkondo wake; ukweli utajulikana, na hatimaye, ama watuhumiwa watakuwa declared guilty na kuswekwa lupango au watakuwa "not guilty" na kuachwa huru na kulipwa fidia zao. Binafsi sioni ulazima wa kutoa taarifa kwa umma kwa tuhuma peke yake. sisi wananchi tunataka wezi wakamatwe washughulikiwe na kisha wawekwe ndani, basi!
 
Mbwa yupi mkali,Anaekukimbiza huku anabweka au anaekukimbiza kimyakimya?Hapa watu wanatengeneza mazingira 2015!We dili nadhalimu wataifa hili kimyakimya wao wakisha ng'atwa wataropoka mtaani!Mwakyembe bado watanzania wanaimani nawe walau kwa 50% ingawa ulivyotoka kwenye matibabu ulitaka kuchafua hali yahewa!
 
naona kila waziri ameanza kwa mbwembwe za kusimamisha watu.. Hii kweli itasaidia kusimama kwa hili shirika?
Kwa muundo wa ATCL kama Shirika la Serikali sioni kama litasimama wima.Vunja shirika uza mali zake achana nalo.ATCimekuwa njia ya kuvuja mali za umma.Ni aibu kuitwa shirika la Ndege la Taifa.Shirika uongozwa na Menegimenti ikiwajibika kwa bodi ya wakurugenzi.Kilicho machoni mwetu ni Crises Committee ya Wizara.
 
Back
Top Bottom