Paul Chagonja: Ni kawaida kwa timu ilioshindwa...

MAMBO 20 NILIYOJIFUNZA
KWENYE MKUTANO WA CCM
JANGWANI.
1. Yamoto Band wameshangiliUwa
zaidi kuliko Magufuli,
2. Wakati Mbowe amewakutanisha
Lowasa na Sumaye. Leo Jakaya
amewakutanisha Diamond na Ali
Kiba Jangwani,
3. CCM wanajua kuwa mikutano ya
UKAWA inapata mafuriko, kwa hiyo
nao walijitahidi wapate "mafuriko"
4. Watu wengi wameenda
kuwashangaa wasanii, sio
kumsikiliza Magufuli. Kumuona
Diamond bei ghali, leo
wamemuona Live bila kiingilio
wataacha kwenda?
5. Magufuli anajua lugha nyingi za
makabila kuliko anavyojua
matatizo ya wananchi,
6. Mkapa anahitaji maombi ya
kufunga maana anazeeka vibaya.
Amemuita Mpumbavu, Waziri
Mkuu aliyemteua mwenyewe na
kufanya nae kazi miaka 10,
7. Mwisho wa mikutano ya siasa ni
saa 12 kamili lakini CCM
wamezidisha dakika hadi 12:40.
Ikiwa wameshindwa kutekeleza
Sheria waliyoiweka mwenyewe,
watawezaje kutekeleza ahadi zao?
CCM hawapaswi kuaminiwa,
8. Kitendo cha Magufuli kukiri
serikali inanyanyasa Machinga na
mama Ntilie ni kukiri kuwa serikali
yake imechoka na inahitaji
kubadilishwa,
9. Magufuli amemvua nguo
Kikwete hadharani. Kusema
anashangaa meno ya tembo
yamefikaje uarabuni ni kusema
kuwa JK anashiriki biashara hiyo.
Ikiwa Magufuli amesema atazuia
biashara hiyo haramu, nini
kimemshinda JK kuzuia kwa sasa?
10. Magufuli anajua kuwa CCM
inakaribia kufa. Wakati akimalizia
hotuba yake ametoa mfano
ambao haukueleweka vizuri, lakini
fundisho lake ni kuwa
WATANZANIA MSIIUE CCM. Kumbe
anajua kuwa CCM itakufa,
11. Ccm wamewadharau sn
watanzania kwa kuwapandisha
malori ya kubebea vitunguu,
nyanya na viazi. Mtanzania
aliyepandishwa lori leo akiipigia
kura CCM atadhihirisha kuwa yeye
ni kiazi,
12. Mzee Warioba ameshindwa
kabisa kumnadi Magufuli kwa hoja.
Kwa namna alivyojieleza anaweza
kuzidiwa na kijana aliyemaliza
form four akapata division zero,
13. Mzee Mkapa ana matusi
"makali" kuliko wafanyakazi wa
bar,
14. Bila msaada wa malori na
kujazia bodaboda mafuta, uwanja
wa Jangwani leo ungekua mtupu,
15. Warioba anaipenda CCM zaidi
ya anavyoipenda Tanzania,
16. Rais Kikwete amekiri kuwa
Magufuli alikua chaguo lake, it
means hakuwa chaguo la
wanaCCM. Kwa lugha rahisi
Kikwete amedhihirisha kuwa
alienda Dodoma akiwa na majina
yake mfukoni kama ilivyodaiwa,
17. Kwa kuwa Polepole alikiri
Warioba ni "Role Model" wake, leo
tumemjua anayemtuma Polepole
kutukana UKAWA,
18. Jeshi la Polisi linatumika
kisiasa. Wameshindwa kuzuia
maandamano "haramu" ya CCM
na kuzuia mkutano ilipofika saa 12
kamili km sheria inavyotaka,
19. Miongoni mwa watu
wanaopaswa kuchunguzwa UKAWA
ikishika dola ni pamoja na Jaji
Joseph Warioba na Mzee Mkapa,
20. CCM haifai kuendelea kuwa
madarakani baada ya October 25
 
Kauli kama ile ilipaswa itolewe na Nape sio Chagonja amedhihirisha upumbavu wake.

Siku ile ya fiesta ya makabwela pale jangwani Magufuli mwenyewe kama nilimsika akisema polisi huwa wananyang'anywa silaha na raia sasa majibu kama hayo lazima huyapate kwa mzee Chagonja poleni wana ukawa ila kuongopewa na ccm nimechoka jamani!!25th
 
Back
Top Bottom