Patrobas Katambi, Naomba uondoe nia yako ya kugombea ubunge Shinyanga Mjini

Kazi za Mbunge sio kuongoza Matambiko, hivyo hatutegemei kabila kuwa ni kigezo kimojawapo cha kumpata Mbunge. Mawazo ya aina hii ndiyo Mwl J. K. Nyerera aliyaita " tumawazo twa kipumbavu". Na upumbavu ni sifa kama urefu au ufupi. Rais J.K Kikwete ni Mkwere ila mbona anakuongoza? Kwanini hukumzuia ili uchague rais Msukuma?

Ubarikiwe sana mkubwa
 
Itakuwa ule msiba wa shangazi yake mtoa nia mwingine,msiba ulikuwa kolandoto sio oldshy,Pass kazaliwa kijiji cha kolandoto wilaya ya shymjini,wapingane kwa hoja na siyo kwa uzawa

Wapingane kwa hoja zenye mashiko na siyo huu upuuzi wa ukabira
 
Wewe PERFECT kajipangeni upya,kwa taarifa yenu Pasi alizaliwa kolandoto hospital,kasoma kolandoto shule ya msingi,baadae baba yake akahamishiwa mkula Hospital Magu,baadae wakarudi tena Shinyanga,Pas ni mzaliwa wa wilaya ya shinyanga mjini upo hapo?issue ya uzawa mmefeli mpaka hapo,Kwanza unamtetea Rachel Mashishanga mtu mwenyewe ana power bank anaishi kwa kupunguza charge za power bank tu,afterall Rachel hafai kuwa mbunge maana hana mipango endelevu ya kuifanya shy town iwe juuu

Duu ni habari ya kufurahisha kwa makamanda kumtafuta kamanda anaye faa kuiongoza cdm
 
Last edited by a moderator:
Duuh siasa hizi ni balaa tunaongelea ukabila Karne ya21 hakika mtoa mada umenisikitisha,halafu mbona muongozo wa jinsi ya kumpata mbunge umeshatolewa atakuwa sio wa kuteuliwa bali ni wakuchaguliwa atakaepata kura nyingi ndio atakaepitishwa iwe umezaliwa kirando au dar suala ni jinsi gani unakubalika kwa wanachama wenzio na wananchi haya masuala ya uzawa,dini,Kabila,urefu au ufupi wake kwa sasa hauna nafasi fursa imetolewa yoyote mwenye uwezo wa kugombea na agombe ondoa fikra za kibaguzi mkuu
 
Nachukia sana ubaguzi wa aina yeyote

Sijui siasa za shy ila kumpiga vita mtu kwa kutumia dhana ya ubaguzi sio sahihi hata kidogo,mleta mada acha watu wachuane kwa hoja hiyo ndio demokrasia ndugu

Siasa za ubaguzi wa kikabira ni noma sana mkuu
 
Nanuku Maneno ya Kamanda Lema... Ukiona Mtanzania wa Leo tunagawanywa kwa kabila au dini tumefika pabaya Asanteni Mwisho
 
Hoja ya uzawa sawa na ukabil, udini, usomi ni hoja za waliofilisika kimawazo...

Lakini tuongee ukweli huyo M/Kiti wa BAVICHA sijui Petrobus naona kama haitendei haki nafasi yake...Hivi alikosekana mwingine wa kuchukua nafasi ya Kamanda John Heche ndo akalazimishiwa huyu ...
Alafu na yeye eti anataka Ubunge....dah wananchi majimboni wanayo kazi mwaka huu..
 
Wasalam Jamvini,

Kamanda Patrobas Katambi, nakuomba uondoe nia yako ya kugombea ubunge Shinyanga Mjini mara moja.

Kamanda, unafahamu kuwa wewe si mzawa wa hapa Shinyanga Mjini. Na kwamba turufu hii tuliitumia kama CHADEMA dhidi ya Masele na kusababisha ushindi kwetu.

Kamanda, unafahamu huna ndugu wala jamii yako hapa mjini unag'ag'ania. Kamanda Masele /Nkurunziza.

Kamanda, unafahamu jimbo la Kahama walikukatalia live, ambako kuna ndugu zako, umefika wilayani hapa na mbunga wamekukubalia kutia nia.

Kamanda, unafahamu ulivyoanzisha mtandao wa kimakundi CHADEMA wilayani hadi kata.

Kamanda, unafahamu wanashinyanga walivyo na misimamo. Juu ya uzawa wameonewa kwa miaka zaidi ya 10.

Kamanda, unafahamu kwana watia nia zaidi ya 10 wenye sifa ila umekomalia kisa ni kiongozi wa kitaifa utapata tu.

Kamanda, unajua ulikataliwa na walimu siku ya seminar yao. Ukimwakilisha Rechal Mashishanga ulizomewa kwa maneno yako kwao. (Ulimi hauna mfupa)

Kamanda unafahamu. Uongozi makao makuu unakubeba, hata mkutano wa hadhara juzi juzi NKMZ Salum Mwalimu alikubeba na kuwaacha watia nia wengine.

Kamanda ni hivi, kujenga CHADEMA si lazma uwe ni Mbunge, mbona una Cheo kizuri kukitumikia chama, BAVICHA TAIFA.

Jipime! usikibomoe chama kwa tamaa zako Kamanda.

Ukweli MCHUNGU wewe si MZAWA wa hapa.

Am always PERFECT.

...............
P.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom