Patrobas Katambi, Naomba uondoe nia yako ya kugombea ubunge Shinyanga Mjini

PERFECT

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
361
131
Wasalam Jamvini,

Kamanda Patrobas Katambi, nakuomba uondoe nia yako ya kugombea ubunge Shinyanga Mjini mara moja.

Kamanda, unafahamu kuwa wewe si mzawa wa hapa Shinyanga Mjini. Na kwamba turufu hii tuliitumia kama CHADEMA dhidi ya Masele na kusababisha ushindi kwetu.

Kamanda, unafahamu huna ndugu wala jamii yako hapa mjini unag'ag'ania. Kamanda Masele /Nkurunziza.

Kamanda, unafahamu jimbo la Kahama walikukatalia live, ambako kuna ndugu zako, umefika wilayani hapa na mbunga wamekukubalia kutia nia.

Kamanda, unafahamu ulivyoanzisha mtandao wa kimakundi CHADEMA wilayani hadi kata.

Kamanda, unafahamu wanashinyanga walivyo na misimamo. Juu ya uzawa wameonewa kwa miaka zaidi ya 10.

Kamanda, unafahamu kwana watia nia zaidi ya 10 wenye sifa ila umekomalia kisa ni kiongozi wa kitaifa utapata tu.

Kamanda, unajua ulikataliwa na walimu siku ya seminar yao. Ukimwakilisha Rechal Mashishanga ulizomewa kwa maneno yako kwao. (Ulimi hauna mfupa)

Kamanda unafahamu. Uongozi makao makuu unakubeba, hata mkutano wa hadhara juzi juzi NKMZ Salum Mwalimu alikubeba na kuwaacha watia nia wengine.

Kamanda ni hivi, kujenga CHADEMA si lazma uwe ni Mbunge, mbona una Cheo kizuri kukitumikia chama, BAVICHA TAIFA.

Jipime! usikibomoe chama kwa tamaa zako Kamanda.

Ukweli MCHUNGU wewe si MZAWA wa hapa.

Am always PERFECT.
 
Wewe lazima n mtia nia mmojawapo unayemwogopa Katambi, umeshindwa kumwabia haya maneno yako hadi huyalete humu?
Mie ni kamanda mpambanaji wala sina haja ya kutia nia.

Nilijipima nikapwaya, mshauri mwezio tusije poteza jimbo kizembe
 
Patrobass katambi ndiye Mbunge mtarajiwa wa Shinyanga...kama mnamwogopa baada ya kutangaza nia...shauri yenu...katambi kwao ni shinyanga na baba yake ni Dr. hapa na wamejenga nyumba hapa na ni msukuma....halafu..kumbuka mijini hakuna cha mzawa..sijui wewe ni wa wapi? acha ujinga wako mkuu wa kutuingiza huko..
 
kama ni kweli mimi mwenyewe sikubaliani nae kabisa ifike wakati mtu kama yeye atulie ajenge chama bado kijana sana yasije kutokea ya heche na waitara tarime ...shinyanga ni jimbo ambalo wazawa wametumika sana kujenga chama sasa asitokee mtu mwingine kisa ana cheo akomalie kugombea....kuna makada wa chadema wanakubalika sana hapo shinyanga ....katambi anatakiwa atulie ajenge chama bado kijana sana ....tulilikosa jimbo la tarime kwa matatizo hayo hayo
 
Unajua kuwa Patrobass alianzia elimu yake Hapo shinyanga? Tunazo taarifa kuwa Kuna mtia nia mwenzake ameogopa baada ya kusikia kuwa Patrobass nae ametia tia, kwa hiyo mengi yatasemwa sana lakini patrobass ni mzoefu wa siasa za hapa Tanzania kwa hiyo hana wasiwasi na maneno yenu hayo....

Kuthibisha kuwa kijana hana tatizo...amewahi kuhudhuria msiba wa ndugu yake hyo mtia nia mwenzake hapo Old shinyanga.
 
Hii habari ya kuanza kuzuia watu kwa kigezo cha uzawa mnaitoa wapi? Tabia hizi ni za kiccm pure, Katambi kama kajipima na kuona anatosha kugombea huko Shinyanga, wewe unapakachuka hapa unadhani waweza kumkwamisha? Nenda kapeleke hoja zako hizi kwenye Kamati tendaji za jimbo/ Wilaya ili angalau uonekane unahoja yenye mantiki. Jukwaa hili si jukwaa.la Cdm hofu zako peleka Lumumba

Watakao mkataa Katambi ni wajumbe rasmi wa Kamati tendaji wanaoingia kwenye mkutano wa kuchagua Mgombea Ubunge kupitia Cdm, kama wewe ni mjumbe nenda huko kapeleke hoja zako kama zinamantiki zitapita na Patrobas atapigwa chini, Vinginevyo Ziba Pakacha lako hapa Wacha wenye nia ya kuwakwamua wananchi wafanye hivyo alaah,!!!!

BACK TANGANYIKA
 
Unajua kuwa Patrobass alianzia elimu yake Hapo shinyanga? Tunazo taarifa kuwa Kuna mtia nia mwenzake ameogopa baada ya kusikia kuwa Patrobass nae ametia tia, kwa hiyo mengi yatasemwa sana lakini patrobass ni mzoefu wa siasa za hapa Tanzania kwa hiyo hana wasiwasi na maneno yenu hayo....

Kuthibisha kuwa kijana hana tatizo...amewahi kuhudhuria msiba wa ndugu yake hyo mtia nia mwenzake hapo Old shinyanga.
Kusoma shinyanga ndio mzaliwa wa hapa?

Wazazi wake wapo wapi?
 
Hii habari ya kuanza kuzuia watu kwa kigezo cha uzawa mnaitoa wapi? Tabia hizi ni za kiccm pure, Katambi kama kajipima na kuona anatosha kugombea huko Shinyanga, wewe unapakachuka hapa unadhani waweza kumkwamisha? Nenda kapeleke hoja zako hizi kwenye Kamati tendaji za jimbo/ Wilaya ili angalau uonekane unahoja yenye mantiki. Jukwaa hili si jukwaa.la Cdm hofu zako peleka Lumumba

Watakao mkataa Katambi ni wajumbe rasmi wa Kamati tendaji wanaoingia kwenye mkutano wa kuchagua Mgombea Ubunge kupitia Cdm, kama wewe n9i mjumbe nenda huko kapeleke hoja zako kama zinamantiki zitapita na Patrobas atapigwa chini, Vinginevyo Ziba Pakacha lako hapa Wacha wenye nia ya kuwakwamua wananchi wafanye hivyo alaah,!!!!

BACK TANGANYIKA

Mkuu,

Kati ya watu wachache makamanda huwa nakuheshimu sana.

Soma vizuri uelewe hoja.

Mwaka 2010, kamanda Marehemu Shilembi na sie wana Chadema, tulikuwa tunajinadi kuwa Masele si mzawa wa hata kaja kuufanya ubunge ni kama take away.

Leo tutasemaje kwa Katambi?

Hebu tuache mzaha kwenye mambo serious.

Abaki kuwa ni mwenyekiti BaVicha
 
Back
Top Bottom