Patrick Oita Nyapara: Askari Polisi aliyemtandika mpenzi wake Risasi 47

Patrick Oita Nyapara, ambaye ni police nchini Kenya alimuua mpenzi wake kwa kumtandika Risasi 47 baada ya binti huyo kumkataa, pindi alipomaliza masomo Chuo Kikuu.

Kwa maelezo ya Patrick ni kwamba alimchukua mdada huyo aliyejulikana kwa jina la Christine Maonga kutoka katika familia duni kijijini na kumpeleka mjini Nairobi kama mke wake ambapo aliamua kumsomesha mpaka chuo kikuu.

Alikuwa akimlipia karo na mahitaji mengine pamoja na kutuma pesa kwa mama mzazi wa binti huyo kama msaada kutokana na familia hiyo kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha.

Baada ya kuhitimu masomo yake, Christine alimwambia Patrick kuwa amechoka kuwa naye kwani ni mtu asiyekuwa na hadhi yoyote na hafai kuwa mpenzi wake hivyo ni vyema kila mtu afanye mambo yake.

View attachment 1072147

"Nimepata mpenzi mwingine ambaye ananifaa sana pia ni Mkurugenzi wa Kampuni moja kubwa sana jijini Nairobi hivyo siwezi kuwa na wewe Patrick mtu usiyekuwa na future na ni daraja D ambalo ni dhaifu kwangu", alisema Christine.

Patrick hakuielewa kauli ya mpenzi wake, akaamua kwenda kijijini kwa mama yake na Christine kuomba msaada wa suluhu ili aweze kumuoa binti yao kwani alikuwa ametumia gharama kubwa mno kumsomesha.

Mama yake binti alijibu kuwa hawezi kumpangia mtoto wake mume wa kumuoa hivyo anapaswa aachwe ajiamulie yeye mwenyewe. Patrick hakukubali, akamtafuta dada yake Christine na kumwelezea hali halisi lakini alijibiwa kuwa hana hadhi ya kumiliki mwanamke aliyehitimu Chuo Kikuu hivyo atafute mwanamke wa level ya mgambo kama yeye.

View attachment 1072149
View attachment 1072150

Aliondoka na kurudi nyumbani na kuchukua uamuzi mgumu wa kumuita Christine nyumbani kwa lengo la kuongea na kumaliza tofauti zao ili waachane kabisa, binti alienda nyumbani kwa Patrick mapema zaidi. Alifika na kumkuta Patrick amejihami kwa silaha, hawakuzungumza chochote zaidi ya kumkandamiza risasi 47 na zote zikapita mwilini mwa Christine hali iliyopelekea kifo chake papo hapo.


Nini maoni yako kwa Patrick Oita? Na Je ungekuwa wewe ungefanyaje?

View attachment 1072075

Cc Zero IQ
The same happened to my father!!.... 12 years ago...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makubaliano yanaweza kubadilika wakati wowote.
Kama makubaliano yana weza badilika muda wowote basi na wewe uwe na uwezo wa kunirudishia gharama zangu ili Kila mtu ale 50 zake la sivyo naku wahisha kuzimu fasta ..alafu ukifika huko bado una kesi ya kujibu kwa nini ulinisaliti ..hahahh moto utakuhusu na huko
 
Mimi nilikoma , kuna demu alipt 4 ya 26. Akawa kakata tamaa, nikampa ushauri we, mpk akaelewa, bdae nkamfnyia mpngo wa chuo, akachaguliwa diploma in community development. Hela nkamsaidia pia ili akamilishe registration after one week akanmbia kila mmj abaki na njia zake. Tangu siku hyo nikaapa mwanamke wa kuheshimu na kujali ni Mama yng tu.Mungu si Athuman kamesoma kamefka mwk wa pili wazazi wameshindwa ada, kameamua kuwa kakibarua kwenye reli za waturuki mpk ada ije itimie

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora ulijiwahi mapema.... Mambo ya kujutia baadae unaweza kuua mtu....
 
Kama makubaliano yana weza badilika muda wowote basi na wewe uwe na uwezo wa kunirudishia gharama zangu ili Kila mtu ale 50 zake la sivyo naku wahisha kuzimu fasta ..alafu ukifika huko bado una kesi ya kujibu kwa nini ulinisaliti ..hahahh moto utakuhusu na huko
Ukiomba kurudishiwa gharama zako unarudishiwa tu. Moto hata wewe unakuhusu. Mie unaniua story inaisha unabaki na mateso na majuto yasoisha.
 
ALIMPIGA RISASI 47

Na Juma Sylvestre Max...

Patrick Oita Nyapara police jamii nchini Kenya alimuua mpenzi wake kwa kumtandika Risasi 47 baada ya binti huyo kujifanya mjanja.
Kwa maelezo ya Patrick ni kwamba alimchukua mdada Christine Maonga kutoka ktk familia duni iliyokuwa ikiishi kijijini na kumpeleka mjini Nairobi kama mke wake ambapo aliamua kumsomesha mpaka chuo kikuu.

Wakati akimlipia karo na mahitaji mengine Patrick alikuwa akituma pesa pia kwa mama mzazi wa binti huyo kama msaada kutokana na familia hiyo kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha.

Baada ya kuhitimu masomo yake Christine alimwambia mpenzi wake kuwa amechoka kuwa naye kwani ni MTU asiyekuwa na hadhi yoyote na hafai kuwa mpenzi wake hivyo ni vyema kila MTU afanye mambo yake.

"Nimepata mpenzi mwingine ambaye ananifaa sana pia ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa sana jijini Nairobi hivyo siwezi kuwa na wewe Patrick MTU usiyekuwa na future na ni daraja D ambalo ni dhaifu kwangu" aliongeza Christine.

Patrick alichanganyikiwa sana akaamua kwenda kijijini kwa mama yake na Christine kuomba msaada wa suluhu ili aweze kumuoa binti yao kwani alikuwa ametumia gharama kubwa mno kumsomesha.

Mama yake binti alijibu kuwa hawezi kumpangia Mme wa kumuoa binti yake hivyo anapaswa aachwe ajiamlie yeye mwenyewe.
Patrick hakukubali akamtafuta Dada yake Christine na kumwelezea hali halisi lakini alijibiwa kuwa hana hadhi ya kumiliki mwanamke aliyehitimu chuo kikuu hivyo atafute wa level ya mgambo kama yeye.

Aliondoka na kurudi nyumbani kufanya uamzi mgumu wa kumuita Christine sehemu ya hotel au nyumbani, walikubaliana kukutana wayamalize na waachane kabisa na binti alienda nyumbani kwa Patrick mapema zaidi.
Alifika na kumkuta Patrick amejihami kama boko haram, hawakuzungumza chochote zaidi ya kumkandamiza risasi 47 na zote zikapita mwilini mwa Christine hali iliyopelekea kifo chake papo hapo.
Mimi nisomeshe kisha niambiwe sina kigezo. 47 chache sana yule ilikuwa inahitajika RPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom