Patrick Oita Nyapara: Askari Polisi aliyemtandika mpenzi wake Risasi 47

Angeanza kumkandamiza risasi mama mtu, kisha akakandamiza risasi dada mtu halafu akamalizia na huyu kufurugobe...

Ni kosa kubwa kwetu binaadamu kuamin mtu 100% watu wote wanaochukua maamuzi mabov ni wale wote wenye kuamini matokeo ya upande mmoja, fikiria jitu limefelu mtihani linachukua maamuzi magumu, means alikuwa anategemea matokeo ya aina moja yale mengine hayakuwa na nafsi..

Unapokuwa na mwenza usimuamin 100 kwa 100, chukulia na binadamu muda wowote anaweza kupiga tikitaka, so unapofnya lako ama kumsaid unajua hilo hata akibuduka samasoti tayar unakuwa katika hali ya utayari kuliko kujitoa 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu humtaki vyake unakula vya nini? Marehemu aliyataka mwenyewe sio kwa dharau waliyomfanyia jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Na jamaa alikuwa very mvumilivu… amemwambia binti lakini wapi, akaenda kwa mama wa binti, balaa, akaenda kwa dada yake... YALE YALE..... wakati huo huo mama alishakula hela za jamaa mara kadhaa… na binti kasomeshwa ...!!!!! kuna wakati shetani tunamlaumu bure tu..
 
Patrick Oita Nyapara, ambaye ni police nchini Kenya alimuua mpenzi wake kwa kumtandika Risasi 47 baada ya binti huyo kumkataa, pindi alipomaliza masomo Chuo Kikuu.
Kwa maelezo ya Patrick ni kwamba alimchukua mdada huyo aliyejulikana kwa jina la Christine Maonga kutoka katika familia duni kijijini na kumpeleka mjini Nairobi kama mke wake ambapo aliamua kumsomesha mpaka chuo kikuu.

Alikuwa akimlipia karo na mahitaji mengine pamoja na kutuma pesa kwa mama mzazi wa binti huyo kama msaada kutokana na familia hiyo kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha.

Baada ya kuhitimu masomo yake, Christine alimwambia Patrick kuwa amechoka kuwa naye kwani ni mtu asiyekuwa na hadhi yoyote na hafai kuwa mpenzi wake hivyo ni vyema kila mtu afanye mambo yake.

"Nimepata mpenzi mwingine ambaye ananifaa sana pia ni Mkurugenzi wa Kampuni moja kubwa sana jijini Nairobi hivyo siwezi kuwa na wewe Patrick mtu usiyekuwa na future na ni daraja D ambalo ni dhaifu kwangu", alisema Christine.

Patrick hakuielewa kauli ya mpenzi wake, akaamua kwenda kijijini kwa mama yake na Christine kuomba msaada wa suluhu ili aweze kumuoa binti yao kwani alikuwa ametumia gharama kubwa mno kumsomesha.

Mama yake binti alijibu kuwa hawezi kumpangia mtoto wake mume wa kumuoa hivyo anapaswa aachwe ajiamulie yeye mwenyewe. Patrick hakukubali, akamtafuta dada yake Christine na kumwelezea hali halisi lakini alijibiwa kuwa hana hadhi ya kumiliki mwanamke aliyehitimu Chuo Kikuu hivyo atafute mwanamke wa level ya mgambo kama yeye.

Aliondoka na kurudi nyumbani na kuchukua uamuzi mgumu wa kumuita Christine nyumbani kwa lengo la kuongea na kumaliza tofauti zao ili waachane kabisa, binti alienda nyumbani kwa Patrick mapema zaidi. Alifika na kumkuta Patrick amejihami kwa silaha, hawakuzungumza chochote zaidi ya kumkandamiza risasi 47 na zote zikapita mwilini mwa Christine hali iliyopelekea kifo chake papo hapo.

Nini maoni yako kwa Patrick Oita? Na Je ungekuwa wewe ungefanyaje?

View attachment 1072075

Cc Zero IQ

Binti alikuwa anahitwa na mauti.
Wakati anasomeshwa aliona hizo pesa zina hadhi naye, lakini baada ya mafanikio, anamwona yule aliyemfanikisha hana hadhi.
Hili ni fundisho toshakwa pande zote mbili, anayehudumia na anayehudumiwa.
 
Patrick Oita Nyapara, ambaye ni police nchini Kenya alimuua mpenzi wake kwa kumtandika Risasi 7 baada ya binti huyo kumkataa, pindi alipomaliza masomo Chuo Kikuu.
Kwa maelezo ya Patrick ni kwamba alimchukua mdada huyo aliyejulikana kwa jina la Christine Maonga kutoka katika familia duni kijijini na kumpeleka mjini Nairobi kama mke wake ambapo aliamua kumsomesha mpaka chuo kikuu.

Alikuwa akimlipia karo na mahitaji mengine pamoja na kutuma pesa kwa mama mzazi wa binti huyo kama msaada kutokana na familia hiyo kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha.

Baada ya kuhitimu masomo yake, Christine alimwambia Patrick kuwa amechoka kuwa naye kwani ni mtu asiyekuwa na hadhi yoyote na hafai kuwa mpenzi wake hivyo ni vyema kila mtu afanye mambo yake.

"Nimepata mpenzi mwingine ambaye ananifaa sana pia ni Mkurugenzi wa Kampuni moja kubwa sana jijini Nairobi hivyo siwezi kuwa na wewe Patrick mtu usiyekuwa na future na ni daraja D ambalo ni dhaifu kwangu", alisema Christine.

Patrick hakuielewa kauli ya mpenzi wake, akaamua kwenda kijijini kwa mama yake na Christine kuomba msaada wa suluhu ili aweze kumuoa binti yao kwani alikuwa ametumia gharama kubwa mno kumsomesha.

Mama yake binti alijibu kuwa hawezi kumpangia mtoto wake mume wa kumuoa hivyo anapaswa aachwe ajiamulie yeye mwenyewe. Patrick hakukubali, akamtafuta dada yake Christine na kumwelezea hali halisi lakini alijibiwa kuwa hana hadhi ya kumiliki mwanamke aliyehitimu Chuo Kikuu hivyo atafute mwanamke wa level ya mgambo kama yeye.

Aliondoka na kurudi nyumbani na kuchukua uamuzi mgumu wa kumuita Christine nyumbani kwa lengo la kuongea na kumaliza tofauti zao ili waachane kabisa, binti alienda nyumbani kwa Patrick mapema zaidi. Alifika na kumkuta Patrick amejihami kwa silaha, hawakuzungumza chochote zaidi ya kumkandamiza risasi 47 na zote zikapita mwilini mwa Christine hali iliyopelekea kifo chake papo hapo.
Nini maoni yako?
 
Back
Top Bottom