Patrick Mfugale katika umri wa miaka 71 alikuwa anafanya nini ofisi ya umma?

Ili kampani ya meko hiyo, Corona itawamaliza
Katika hali ya kawaida serikali inaweza kumuongezea muda wa utumishi serikalini mtumishi ye yote wakati ikijipanga kuandaa watumishi wengine wanaoweza kuchukua nafasi ya mtumishi anayestaafu. Kitendo cha Mhandisi Mfugale kuongezewa muda wa utumishi wa serikalini kwa muda usiojulikana hadi anafariki dunia ni dharau iliyopindukia kwa watumishi wengine wa TANROADS na kuna kila dalili za ufisadi na wizi wa fedha za umma kupitia TANROADS.

Haingii akilini kuwa hakuna Mtanzania mwingine ye yote ambaye angeshindwa kuchukua nafasi ya Mfugale baada ya kupata mafunzo stahiki! Kuna haja na sababu muhimu kufanyika kwa uchunguzi kwa nini Mfugale akaongezewa muda mrefu kiasi hicho. Aidha kuna haja ya kufanya uchunguzi kwa watumishi wote walioongezewa muda kupindukia uhusiano wao na watawala. Mfano mwingine wa mtumishi aliyeongezewa muda kupindukia ni marehemu Kijazi.

Uchunguzi huu ni muhimu na hasa kipindi hiki ambacho vijana wengi wanakosa ajira na hivyo kuwanyima fursa za kuonyesha vipaji vyao.

Mfugale alizaliwa mwaka 1953 na alipaswa kustaafu mwaka 2013 baada ya kutimiza umri wa miaka 60.
 
Hahahahah
Sikumwelewa Mwendazake kwenye moja ya hotuba zake za mwisho akiwa kwenye uzinduzi wa daraja la Kijazi kama sijakosea, alisema "...namwomba Mungu asimchukue Mhehe huyu kabla hajamaliza kazi za ujenzi zinazoendelea nchini..."
 
Jamaa alikuwa productive kwenye nchi kuliko wapuuzi kibao mnaomponda! Amefanya vitu vya kuonekana kabisa!
Hivi kama yeye asingepewa nafasi enzi za alivyoajiriwa angefanya yote hayo? Lazima sheria ifuatwe na ni muhimu damu mpya ili nayo ipewe nafas ya kufanya kama aliyofanya huyu hayati ndo mana kukawa na kustaafu kwa hiari na lazima
 
Serikal iliwah kupitisha ruhusa kwa kada flan kuendelea kufanya kwa maana ktk serikal baada ya ule umri wa kustaafu kufika ..nafikir pia ilikuwa kwa wanazuoni Dkts,profs ..nafikir na exceptional professionals .....correct me if i am wrong
'Think tanks' lazima watunzwe na kuendelea kutumika kwa maslahi mapana ya jamii/taifa. Ukienda nchi zilizoendelea utashangaa zaidi!
 
Angefanya kazi za consultancy, huku akila pensheni, wanasiasa walimpotosha na kumtumia tu huyu baba, kafia kazini, na kafariki na kashfa, na hatutokumbuka madaraja bali REPORT ya B.o.T ya TANROADS kujilipa mara 2,2.

Pole SANA watani zangu, wanyalukolo wa Ifunda.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Hivi kama yeye asingepewa nafasi enzi za alivyoajiriwa angefanya yote hayo? Lazima sheria ifuatwe na ni muhimu damu mpya ili nayo ipewe nafas ya kufanya kama aliyofanya huyu hayati ndo mana kukawa na kustaafu kwa hiari na lazima
Saw damu mpya itapewa nafasi yeye ameshafariki
 
'Think tanks' lazima watunzwe na kuendelea kutumika kwa maslahi mapana ya jamii/taifa. Ukienda nchi zilizoendelea utashangaa zaidi!
Wenzetu life expectacy yao ni miaka mingi mtu kufika 90 akiwa fit kawaida,sisi huku miaka 50 presha kisukari ,ukimwi,korona vyote vyako muda mwingi unaspend hospitali badala ya ofisini,
 
Umri sahihi wa kustaafu utumushi wa umma ni miaka 55 kwa hiari na miaka 60 kwa lazima, japo kanuni zinaruhusu kuendelea kutumikia umma kwa mkataba wa miaka miwili miwili, Mfugale hajawahi kustaafu na amekuwa akiongezewa mikataba juu kwa juu.

Madhara yake mnabana nafasi za ajira kwa wengine.

RIP Mfugale 1950-2021

Mfugale alizaliwa 1953, siyo 1950
 
fundisho kwa vijana tubobee na kufanya kazi kwa juhudi utazeeka kwa raha. naona nchi za wenzetu wazee wanakufa bado hawahitaji msaada wa kiuchumi kutoka kwa watoto wao.
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom