Patrick Mfugale katika umri wa miaka 71 alikuwa anafanya nini ofisi ya umma?

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
8,435
2,000
Umri sahihi wa kustaafu utumushi wa umma ni miaka 55 kwa hiari na miaka 60 kwa lazima, japo kanuni zinaruhusu kuendelea kutumikia umma kwa mkataba wa miaka miwili miwili, Mfugale hajawahi kustaafu na amekuwa akiongezewa mikataba juu kwa juu.

Madhara yake mnabana nafasi za ajira kwa wengine.

RIP Mfugale 1950-2021
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,866
2,000
Nimeona msalaba unasema amezaliwa 1953, wewe unasema 1950, tukuamini wewe tuamini ndugu walioandika msalaba?

Anyway, umri sio shida sana kama mtu bado ana nguvu na anajiweza.

Dr. Fauci wa Marekani ana miaka 81 na bado anapiga kazi kama kawaida. Alipewa ukurugenzi miaka 36 iliyopita na hajawahi kustaafu.
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,784
2,000
Kuna wakati nilipomuona akiwa kazini anakagua mabarabara nilimuonea huruma kwa hali yake ya kiafya, nilijiuliza kwanini hapumzishwi au kwanini yeye haombi kupumzika? Maskini! hadi amefia kazini.

Hili ni fundisho pia kwa watumishi wengine wenye umri mkubwa au wana matatizo ya kiafya ni vyema wakaomba kustaafu kwa hiyari ili wapate muda wa kupumzisha miili yao kuliko kuifia kazini.

Kumbukeni kazi na afya, Afya yako/uhai wako ni muhimu sana kuliko kazi, ukifa leo kesho tunateua mwengine anashika nafasi yako.
wazee mnaotaka kuifia kazini pumzikeni, pisheni vijana nao wapige kazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom