Pato la taifa la tanzania lakua kwa 7.1% | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pato la taifa la tanzania lakua kwa 7.1%

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Gumzo, Aug 4, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa taarifa ya hali ya uchumi nchini na kufafanua kuwa pato la taifa la Tanzania limekua kwa asilimia 7.1 katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ikilinganishwa na asilimia 6.1 za mwaka jana.

  Ukuaji huo wa asilimia 7.1 unatokana na ongezeko la uzalishaji katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo za kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi na zile za utoaji wa huduma mbalimbali za jamii.

  Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa lengo la utoaji wa taarifa hizo kwa vipindi vifupi vya vya robo mwaka unalenga kuwapatia wadau wa Takwimu za Pato la Taifa uwezo wa kutathmini mabadiliko ya ukuaji wa uchumi nchini.

  Amesema kuwa jumla ya thamani ya pato la Taifa katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ni shilingi 4,220,535 milioni ikilinganishwa na kiasi cha shilingi milioni 3,940,261 za mwaka 2011.

  Amefafanua kuwa ukuaji wa shughuli uzalishaji katika shughuli za kilimo nchini ulifikia asilimia 1.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2012 zikilinganishwa na asilimia 1.2 katika kipindi hicho kwa mwaka 2011 kutokana na upatikanaji wa mvua za kutosha nchini katika mikoa inayozalisha mazao kwa wingi.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Unamaanisha nini pato la taifa wakati serikali imeshindwa kulipa baadhi ya watu mishahara?
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Uchumi unaokuwa kitakwimu bila kukuza pato la kaya ni uchumi hatari kwa dola yoyote yenye maono!

  Kwanza naweza kupingana na takwimu hizo za wanauchumi wa Tanzania kwa sababu mbili:

  1. Mpaka sasa tz hatuna idadi kamili ya watu tangu sensa ya mwaka 2000 ambapo naamini takwimu ile ukitumia leo utakuwa unajiibia wewe mwenye kutoka mfuko wa kulia kupeleka mfuko wa kusho,

  2. Kippimo kinachtumia kujua pato la taifa kimekuwa kikipingwa na mataifa mengi yanayoendelea, na wanapendekeza badala ya utaratibu wa asili wa kujumlisha pato la taifa na kuligawa kwa idadi ya watu na kuonekana kila mtu amezalisha katika uchumi huo, sasa iwe ni kwa kupima pato la kaya!

  Hii itasaidia kutambua wakaazi wa Tanzania kama bado wanaishi chini ya mstari wa umasikini duniani wa shilingi 260 au wapo kwenye shilingi 1000 kama tunavyo laghaiwa na mkoloni mweusi wa ndani mumiani!
   
 4. zungupori

  zungupori Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  alafu hizo takwimu zinazjngatia hela zilizofichwa huko uswisi, us, uk et al? Cha muhimu zaidi mfumuko wa bei umekaa vp na ukiambatanisha unapata picha gani? Hizi data ni kama zile toka china ZIMEPIKWA lakini ni hadithi nzuri ambayo wanataka udadisi eti there's light at the end of tunnel, in fact zitasaidia sana campaign kupiga wawekezaji longolongo
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Halafu hivi hizi takwimu zina credibility gani?

  Katika nchi zenye utawala bora, idara nyeti kama polisi, mahakama, jeshi la ulinzi, na takwimu huwa hazifanyi kazi kumfurahisha kiongozi bali ziafanya kilicho kweli kwa nchi. Kutokana na ukweli kuwa hapa kwetu mahakama zimekuwa zinatumika kuzuia migomo ya wafanyakazi, polisi wamekuwa wanatumiwa kwa mambo ya kisisa, na jeshi la ulinzi (General Shimbo) nalo limekuwa vinatoa matakamo kwa ajili ya kumfurahisha mkuu, je hii idara ya takwimu yenyewe ina tofauti gani na hizo nyingine.

  Nina wasiwasi kuwa sasa hivi wako katika harakati za kujenga vigezo vya kutumika kwenye uchaguzi wa 2015.
   
 6. S

  Sir M.D.Andrew JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukuaji uchumi wa tz ni wa kwenye makaratasi,hauoneshi hali halisi,au unakua kuelekea wapi?
   
 7. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ni hbr njema kwa watz,ila ongezeko uhalisia wake kwa watz halionekani kabisa,vipato bado ni chini sana,mfumuko wa bei!
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  hongera kikwete kwa kukuza uchumi wa kwenye makaratasi,microsoft word na pdf,safi sana! Tunaona huku hali halisi!
   
 9. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ni ukweli au sanaa zilizopikwa kama siyo vihiyo wanaoitwa au kujiita wasomi wanao ima jipendekeza kwa Kikwete au kutumiwa naye? Uchumi hauwezi kukua sambamba na ufisadi na ukosefu wa huduma za jamii na za uhakika.

  Uchumi hauwezi kukua sambamba na ukosefu wa sera.
  Uchumi hauwezi kukukua sambamba na uombaomba na kutegemea misaada toka nje.
  Uchumi hauwezi kukuka chini ya utawala wa kishikaji, kifisadi na kibabaishaji kama huu tulio nao kwa sasa.
  Uchumi hauwezi kukuzwa na takwimu bali reality on the ground.
  Uchumi hauwezi kukuzwa na ongezeko na deni la taifa ukiachia mbali la vitendo vya rushwa vya mawaziri wabunge na watawala kwa ujumla.

  Huu ni uongo wa mchana utahadharini wanangu.
   
 10. s

  sanjo JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Takwimu hizi zina maana gani ukilianganisha na halisi ilivyo ambapo walimu wanagoma? Makontakta hawajaripwa na serikali? Ikike mahali watu waelezwe dosari ya takwimu kama hizi juu ya maisha yao•
   
 11. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hakuna utafiti wowote hapo wala kukua kwapato.labda unieleze kuna tanzania nyingine tofauti na hii ya huku kwangu ninakokaa kijiji cha kasungamile,watu hoiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 12. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Tupeni source zenu basi zinazoaminika kama hamzitaki hizi.
   
 13. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  MJIMPYA acha ujinga nawe, uchumi wa nchi gani ukue kwa 7.1%?
  1.wakati umeme ni wa shida
  2.miradi ya maendeleo imepata 30% ya bajeti mwaka 2011/12
  3.Unemployment imeongezeka hadi kufikia 58%
  4.misaada na mikopo kutoka nje imeshuka
  5.Inflation rate imekuwa double digit for a while now.
  ni taarifa za wachumia matumbo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ndege inapaa hiyo ninyi endeleeni kutokwa mapovu. Badala msaidie kujenga nchi yenu mmekazana kuirudisha nyuma kisa tu siasa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45

  Sasa mimi na wewe nani mjinga?
  Una hasira tu mdogo wangu lakini ukweli ndo huo. Kama uelewi maana ya kukua kwa uchumi na hayo mapungufu unayoyasema ni bora ukaomba msaada uelewe kuliko kutukana mtu usiyemjua.
  Unaongea tu mambo ya kijiweni lakini facts ni kitu kingine.

  If you dont trust the growth rate of about 7.1% why do you trust the inflation, unemployment rate and other figures issued by the same institution? Je nani mjinga hapo?

  Nakuheshimu siwezi kutukana ni bora nawe ukaheshimu wengine maana hunijui sikujui.
  Am sure you like to be respected, reciprocate!
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Mjimpya mbona unatisha watu hapa JF,hatujaja hapa kujua huyu ni nani au huyu ni nani hata ukiwa bwana utouh au hata werema haisaidia kitu,sio kila mtu achukue + chochote unacholeta hapa,whether uwe mfumuko wa bei au kukua kwa uchumi sisi huku mtaani ndio tunaona! Mfumuko wa bei unaonekana dhairi ni 20% tena ni zidi ya hyo fig lkn huo ukuwaji wa uchumi wa 7.1% ni changa la macho hatukubaliani na wewe hata kama wewe ni rais umetumia fake ID.....Huo ukuaji wa uchumi ni wa kwenye mafaili ya makabatini tu!
   
Loading...