Pato la mtanzania mmoja mmoja la ongezeka baada ya miaka 50 ya uhuru

Mgongo wa paka

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
485
34
Kwa mujibu wa waziri lukuvi alipoongea ktk moja ya sherehe zina zokaribisha sherehe kuu ya kutimiza miaka 50 ya uhuru. Anasema wakati tukipata uhuru mtanzania alipata shilingi 770 kwa mwaka huyo mtanzania wa chini. Leo mtanzania anapata anapata shilingi laki saba na sabini elfu. Kwa kujiamini na akionekana akifurahia kuwa pato la mtanzania limeongezeka. Sasa shilingi 770 wakati huo ilikuwa sawa na dola 770. Kwa mahesabu ya haraka mtanzania alipata shilingi milioni moja na lakimbili na hamsini elfu. Kabla ya uhuru na wakati wa uhuru. Lakini leo mtanzania anapata shilingi laki saba na sabini elfu halafu lukuvi anafurahi patao la mtanzania kushuka jamani nivema tuwe wakweli ili tutatue hili tatizo la kushuka kipato cha mtanzania tujiulize wapi tumejikwaa ili tuongeze hilo pato la mtanzani tuwe wazalendo.
 
HAKI bin AMANI

Senior Member
Sep 5, 2011
156
34
Mbona wanaposema pato limeongezeka hawatafsiri pato katika maisha halisi ya Mtanzania? Wala hawafanyi ulinganifu wa thamani ya fedha ya wakati huo na wakati huu.

Miaka 80 Marehemu Sokoine akiwa Waziri Mkuu aliruhusu magari binafsi yasaidie UDA huduma ya usafiri, nauli ilikuwa Shilingi 5/= sawa na 1 USD na ndiyo asili ya neno daladala mpaka leo.

Kwa kuwa hawasomi alama za nyakati ndiyo maana wanachukua siasa za wakati wa ujima wanazileta wakati wa sayansi na teknolojia.
 
Mrdash1

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,378
331
Miaka 50 wameweza kuongeza pato la mtanzania mmoja mmoja, tupo watanzania millioni 40, kwa hesabu hizo itawachukua ccm miaka 80,000 (elfu 80) kuleta maendeleo ya watanzania wote kama idadi ya watu itabakia millioni 50 kwa miaka yote hiyo. ccm oyeee!!
 
majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
430
179
mnamsikiliza huyo kilaza anayetegemea ujinga wa wahehe(watanzania) kuwadanganya kwamba eti pato la mtanzania limekuwa, haelewi kuwa sh5 ya wakati huo wa wazalendo wa kweli ilinunua kilo ya nyama leo hii kilo elfu6? Huu uongozi wa kupeana kutokana na uhandsome au utaalamu wa kucheza ngoma kama lukuvi unatabu sana.
 
Mtoto Wa Mbale

JF-Expert Member
May 15, 2011
457
300
Wakati wa uhuru wa Tanganyika 1Tsh ilikuwa sawa USD ($) ngapi? Sote tunajua leo 1$ = 1805Tsh. Tutafsiri hali hiyo na kuwaeleza watanzania.
 
mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,271
391
Kwa mujibu wa waziri lukuvi alipoongea ktk moja ya sherehe zina zokaribisha sherehe kuu ya kutimiza miaka 50 ya uhuru. Anasema wakati tukipata uhuru mtanzania alipata shilingi 770 kwa mwaka huyo mtanzania wa chini. Leo mtanzania anapata anapata shilingi laki saba na sabini elfu. Kwa kujiamini na akionekana akifurahia kuwa pato la mtanzania limeongezeka. Sasa shilingi 770 wakati huo ilikuwa sawa na dola 770. Kwa mahesabu ya haraka mtanzania alipata shilingi milioni moja na lakimbili na hamsini elfu. Kabla ya uhuru na wakati wa uhuru. Lakini leo mtanzania anapata shilingi laki saba na sabini elfu halafu lukuvi anafurahi patao la mtanzania kushuka jamani nivema tuwe wakweli ili tutatue hili tatizo la kushuka kipato cha mtanzania tujiulize wapi tumejikwaa ili tuongeze hilo pato la mtanzani tuwe wazalendo.

Lukuvi shule hakuna, tumuonee huruma amalizie kipindi chake kwani harudi tena kwenye serikali ya CCM ijayo
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,443
what a joke

vipi amecheki bei ya vitu na kufunga hesabu za buk-kiping tulizofundishwa??

ingawa tunajua hajasoma?
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,219
91,806
Haaahaaa!what a good joke on a special saturday evening! Ngoja nikatafute bia baridi

umesahau wakati wa kampeni.Makamba alisema Kikwete 'emetimiza ahadi zote'????

kwangu ile ilikuwa the joke of the millenium.....lol
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom