Patience Dabany: Mtalaka wa Rais aliyeuteka ulimwengu wa burudani kwa muziki mzuri

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,794
Dabany.jpg

Patience Dabany akiwa stejini
Tofauti na ma-First Lady wengine wanaostaafu na kuweka miguu juu na kuishi maisha kama ya ikulu nje ya ikulu, Patience yeye anaishi ndoto zake kama mwanamuziki.

Patience Marie Josephine Kama Dabany alizaliwa 22 Januari 1944. Dabany aliwahi kuwa First Lady wa Gabon kutoka 1967 hadi 1987. Kwa karibu miaka 30 alikuwa ameolewa na Omar Bongo Ondimba (aliyekuwa Rais wa Gabon tangu 1967 hadi 2009). Baada ya talaka yake, alihamia katika kazi ya muziki. Yeye ndiye mama wa Rais wa sasa wa Gabon, Ali Bongo Ondimba.

Dabany alikulia katika familia ya muziki na alianza kuimba akiwa mdogo na baba yake, wakati kaka yake alipiga gita. Alijifunza mziki zaidi katika kwaya za kanisani. Mama yake pia alikuwa mwimbaji wa kitamaduni

Kazi ya muziki
Baada ya Joséphine na Bongo kutengana mnamo 1987, Marie alianza kazi ya sanaa chini ya jina lake jipya, Patience Dabany. Albamu yake ya kwanza ilikuwa Levekisha. Albamu zingine zilifuatiwa kama Cheri Sound Disque Est Rayé, nk. Mnamo 1997, alitoa albamu ya Nouvelle Attitude. Mwaka huo huo Dabany alirudi kwao na kujipanga tena Libreville. Mnamo 2001 aliachia Article 106.

Patience Dabany alishirikiana na wasanii wengi kama El DeBarge, Taboo Ley Rochereau, na Tshala Muana. Yeye pia ni rais wa chama cha wafanyabiashara wa Gabon na anafanya kazi za kusaidia jamii.

Baada ya kutumbuiza katika Olimpiki ya Paris mnamo 2001, Patience Dabany ni mmoja wa mabalozi wa muziki wa Gabon anayetamba sana ulimwenguni kote.

Licha ya kuwahi kuwa Mke wa Rais kwa miongo kadhaa huku mwanaye wa kumzaa akiwa ni Rais, mama huyu bado anakonga nyoyo za wapenda muziki kote duniani.

Si watu wengi wangefanya hivyo endapo wangejikuta kwenye nafasi ya mama huyu shupavu wa Kiafrika.



Ali Bongo.jpg

Ali Bongo, Rais wa Gabon ambaye ni mtoto wa Patience Dabany

Omar bongo and Ali Bongo.jpg

Aliyekuwa Rais wa Gabon Omar Bongo (kushoto) na mwanaye Ali Bongo ambaye ni Rais wa sasa wa Gabon
 
Back
Top Bottom