Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Mkuu mi sio muuza mbegu ndg ila kwa hiyo estimation ipo mule mule. Ninayo mipapai hapa kwangu kama mashina 10 hivi yanazaa hakuna mfano ndo maana nikatoa tathmini hiyo kulingana na lumbesa ya matunda inayosheheni kwenye kila shina.
Sorry if i offended you.
.....aah, matunda 250?
Si kweli......mpapai unaozaa sana ni califonia na huzaa 120 !
 
Kwa mwaka average ni 80 kwa mti mmoja hyo ya 250 za kwake huko za kutangazia biashara yake na mpapai unazaa after 9months
 
....Tanzania mashamba yamejaa teeeelee,kwanini usilime wewe unauza mbegu tu
Teh teh teh..... Hili ni jibu Murua sana. Jamaa anaongea theory bila kuweka maelezo ya soko na risk nyingie zinazo tokea ikiwemo 25% ya miche/mbegu zinaweza kutoa mapapai dume. Au labda Mbegu zina faida kuliko matunda!?
 
Mkuu mi sio muuza mbegu ndg ila kwa hiyo estimation ipo mule mule. Ninayo mipapai hapa kwangu kama mashina 10 hivi yanazaa hakuna mfano ndo maana nikatoa tathmini hiyo kulingana na lumbesa ya matunda inayosheheni kwenye kila shina.
Sorry if i offended you.
Mapapai kua mengi nakubali, lakini je yanafikia au kuzidi 250???
 
Kilimoni kizuri sana hasa unapokuatana na hesabu za mchanganuo kama hivi tatizo kinwa ni Soko la bidhaa hizi. HAKIKA UTACHANGANYIKIWA SIKU UKIVUNA UPELEKE MZIGO SOKONI.HUTAMINI
1. hupangi bei wewe
2. Fuso kama mia of the same product zimepaki na hazijauza
3.Michezo michafu ya madalari

4 Risk of perishable products

Fanya utafiti sana sana sana kabla hujaamza kulima zao lolote otherwise utachanganyikiwa
 
.....aah, matunda 250?
Si kweli......mpapai unaozaa sana ni califonia na huzaa 120 !
Nahisi hamjamuelewa amesema hivi ekari moja inapandwa miche 250 yaani jumla ya miche sio mche mmoja unazaa matunda 250 na akasema hivi ukiuza papai moja kwa 500 piga mahesabu kwa kila mche una Papai kwa hyo bei utakua na shilling ngap,?sio mche mmoja uzae matunda 250,hyo ni jumla ya miche shambani,nazani mmeelewa ambao bado hakuna namna labda kurudi shule tu
 
ww ndo hujamuelewa kasema jumla ya miche kwa hekari moja ni 1200 na kila mche mmoja huzaa mapapai 250 kwa mwaka
 
hivi kwa nini tunatoa majibu rahisi tena ya kushindwa na kuwakatisha wengine tamaa? yaani majibu yote yaishie kwenye soko kweli? hakuna sababu nyingine? au hakuna kweli mafanikio katika kilimo hicho?

aliye leta mada kasema kwa mwaka tunaweza kupata kwa mti mmoja zaidi ya papai 250 ambazo sawa na papai 300,000 ambazo zinaweza kuleta pato la shillingi 150,000,000/- kwa mwaka. hivi kweli na hili ni la serikali? hata iweje gharama za uendeshaji hazizidi 50,000,000/- hilo pato bado?

tabu iko wapi kuajiri watu ukagawana nao hiyo mia iliyobaki?

nauhakika nyumba kwa nyumba ukiuza kwa mia tano wateja utapata. huku niliko wakati mwingine papai linauzwa mpaka shillingi 3000.
ijulikane kuwa tunapozungumzia soko tunazungumza zaidi katika vitu vikuu viwili uhitaji wa soko na pia wauzaji au wasambazaji wengine na hapa ndipo tunaweza kuweka bei ambayo itaweza kulipa.
mimi nauhakika soko lipo na la kutosha tabu bado hatujajibidisha katika kulifanikisha mfano jiji la dar peke yake lina watu 6,000,000 ambao hawawezi kushindwa kula mapapai 300,000. ambalo pato tunaliona pale juu.
tujenge ushawishi kwa mfano kwa mwenye matatizo ya kupata choo au anasikia maumivu wakati wa aja kubwa akila papai kila siku hiyo hali inaweza kuondoka.
kiukweli bado hatujafanya matangazo ya kutosha mfano hakuna hata tangazo moja la tv linalotangaza zao kama hilo hebu fikiri unaweza pata milioni 150 unashindwaje kufikiria kugharamia matangazo kwa milion 15?
yapo mengi ya kuelezana lakini kwa leo ni hayo
 
Umeongea kisahihi ila kinadharia zaidi Chiwa. Hii maada inahamasisha watu walime papai, wengi wamesoma hapa, lakini wachache wataenda hatua zaidi kwa kuingia kwenye kilimo hiki. Fikiri watu ishirini tu kila mmoja eka 1 ni eka ishirini hizo, waoteshe papai na yavunwe kama ilivyotegemewa. Unazungumzia papai milioni 6 hivi. Wangapi wataumwa na tumbo watafute papai kama ulivyosema?
Wananchi hawana tabia ya kula matunda kila wakati kama sehemu ya lishe yao, mengi huenda viwandani, mahotelini, mahospitalini na sehemu zinazotoa kipaumbele kwa mlo kamili. Viwanda vya matunda hakuna, mahoteli yanafungwa biashara mbovu, mahospitali yamesitisha huduma za kutoa vyakula kwa wagonjwa... Soko ni kitu cha msingi sana hasa kwa matunda. Tunaona mananasi, maembe, matikiti na machungwa yakioza kila msimu kwa wingi uliokosa soko. Uongezaji wa thamani wa matunda, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa viwanda vya usindikaji vingesaidia.
Kuna haja ya maandalizi makubwa ya miundombinu na masoko kabla ya uwekezaji mkubwa wa kilimo cha matunda na mbogamboga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom