Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Mkuu kama hutojali naomba unipatie mawasiliano yako nikutafte ,, coz mimi pia nimeanza ufugaji huu wa bata but sijapata details za kutosha kuhusu huu ufugaji, so kam hutjali naomba unisaidie kupata mawasiliano yako kwa ushauri zAidi,, niko Mwanza pia
Nenda kwa PM utapata contact zangu mkuu.
 
Kwa bata huko nimeonja mafanikio, muda si mrefu nitawakaribisha wadau walioko Mwanza tukale bata sehemu nitakayowatangazia.
Mkuu salaaam. Naomba muongozo kuhusu bata. Nimeanza ufugaji lakini vifaranga wanakufa sana ( nimepoteza karibia hamsini sasa). Nimepeleka kwa wataalam wakafanyiwa postmortem nikaambiwa ni pneumonia nikawagonga antibiotics za kutosha lakini wapi wanaendelea kufa kila wakianguliwa. Wanajinyonga nyonga shingo wanakufa shingo zimekakamaaa. Nawafuga kisafi nawawekea hadi majiko ya mkaa usiku kuwapa joto. Pia kwa kuanzia naanza nao na chakula cha kuku wa kisasa grower.. Wenye uzoefu msaada nafugia mlandizi Dar es salaama
 
Facilitator kama ni huyu maji hamna shida, ni rahisi sana kuwafuga kwasababu hawahitaji utaalamu wowoteni zaidi ya kuwafungia kwenye uzio na kuwawekea madimbwi ya kuogelea na vyakula vyenye mchanganyiko wa maji kama uji, wanakula kila aina ya chakula kama kiti na huwa hawaumwi hata siku moja ila sema vifaranga wake siku za mwanzo huwa wabovu sana na rahisi sana kufa.. Uzuri mwingine huwa wanatotoa kwa njia za asili na wanatoa watoto kama 8+.
soko lake linasumbua

Mheshimiwa ili kudhibiti vifo vya vifaranga vya bata unaviweka kwenye ndoo. ndani ya ndoo weka tambara au kanga ya zamani ili kufyonza unyevu watakapokuwa wamelala humo kisha juu yake funikiza na kitu kinachopitisha hewa kama waya au crate ya soda tupu. watakua bila wasiwasi. maana ndani ya ndoo watapata joto. tatizo bata mzazi huwa haatamii vifaranga vyake. kisha siku za mwanzo vipe DCP kwenye maji kwa muda wa siku tano hivi na chakula chao wape ile starter ya vifaranga vya kuku kama wiki mbili baada ya hapo. watakuwa wamefikia hatua ya kuhimili mikiki ya maisha.
 
Pia siku za mwanzo usiruhusu waogelee kwenye maji. wape maji au weka maji kwenye kibwawa ulichowaandalia wakifikisha wiki sita. maji ya kunywa unaweza weka kwenye drinker au chombo ambacho hayatakuwa mengi ya kuwafanya wakaogelea
 
Ni mapishi tu!
Hata nyama unazofikiri ni tamu, zisipopikwa/andaliwa vizuri zinakuwa sio tamu.
Wabongo wengi hawana ubunifu katika mapishi, na wanaanda bata kama wanavyoaandaa kuku, ndio maana anakuwa si mtamu.
Bata ni mtamu balaa,shida ya wabongo mbwembwe nyingi!ila ukipata mpikaji mzuri hutaweza kujua ni kuku au ni bata...tofauti ni mapaja tuu ndo yatakushtua ukubwa wake otherwise bata ni mtamu sana especially bata jike.
Na uchinjaji wake ni kama kuku tuu wala mtu asikutisheee mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi ona chipsi bata, wala kwenye sherehe watu wanakula wali au pilau bata, wala sijawahi ona chips mayai ya bata.

Kwa mtazamo wangu hii inaashiria soko la bata ni finyu. Labda kama unafuga kwa chakula nyumbani na familia yako
Bei yake ni ghali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuga bata wa kienyeji, wanasumbuliwa na ugonjwa wa upofu (macho kutoona) na ugonjwa huo huwapata bata kuanzia wiki 3 hivi hadi miezi 3 na wakipata wanakufa.
Niliongea na mtaalamu wa mifugo akanieleza ni ndui, hivyo nikawapatia wote chanjo ya ndui. Tatizo ni kwamba ni kama wiki sasa wameanza tena kuumwa ugonjwa huo wa upofu na kufa.
Naomba msaada wana jamvi ili mnifahamishe dawa ya kutumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefyga kwa mda gan sasa? Kabla ya kupofuka huwa macho yanaonyesha dalili gani?
Bata anayetaga mpka kutotoa na dume lake ndo hao hao toka uanze kufuga?

Nimefuga kwa mwaka mmoja na nusu sasa. Dume la kwanza niliazima, ila kwa sasa nina madume mawili ambayo ni uzao wa kwanza.
Pia Bata jike ambaye ni chimbuko la Bata wote nilionao bado yupo.
Kabla ya kupofuka wanadhoofu, macho yanaweka utandu mweupe pembeni na kisha yanafumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu viwili ninavyojua ni kuwa ndegewakiwa na matatizo ya macho ni vitu viwili.
1. Vitamin inayopatikana kwenye majani.
2. Ugonjwa wa mfumo wa hewa
Nimefuga kwa mwaka mmoja na nusu sasa. Dume la kwanza niliazima, ila kwa sasa nina madume mawili ambayo ni uzao wa kwanza.
Pia Bata jike ambaye ni chimbuko la Bata wote nilionao bado yupo.
Kabla ya kupofuka wanadhoofu, macho yanaweka utandu mweupe pembeni na kisha yanafumba.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuga kwa mwaka mmoja na nusu sasa. Dume la kwanza niliazima, ila kwa sasa nina madume mawili ambayo ni uzao wa kwanza.
Pia Bata jike ambaye ni chimbuko la Bata wote nilionao bado yupo.
Kabla ya kupofuka wanadhoofu, macho yanaweka utandu mweupe pembeni na kisha yanafumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
walishe majani ya vitunguu umemaliza huo mchezo.
 
Bata ni mtamu balaa,shida ya wabongo mbwembwe nyingi!ila ukipata mpikaji mzuri hutaweza kujua ni kuku au ni bata...tofauti ni mapaja tuu ndo yatakushtua ukubwa wake otherwise bata ni mtamu sana especially bata jike.
Na uchinjaji wake ni kama kuku tuu wala mtu asikutisheee mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
ntaleta mrejesho
 
Nimefuga bata wa kienyeji, wanasumbuliwa na ugonjwa wa upofu (macho kutoona) na ugonjwa huo huwapata bata kuanzia wiki 3 hivi hadi miezi 3 na wakipata wanakufa.
Niliongea na mtaalamu wa mifugo akanieleza ni ndui, hivyo nikawapatia wote chanjo ya ndui. Tatizo ni kwamba ni kama wiki sasa wameanza tena kuumwa ugonjwa huo wa upofu na kufa.
Naomba msaada wana jamvi ili mnifahamishe dawa ya kutumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni dalili gani nyingne unaziona mkuu? Lbda kwenye pua zao wanatoa nn? wamevimba macho ?wanavipere usoni?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom