Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

mkuu kwa hawa bata wa kienyeji huwa hawana shida wao wanazaliana sana cha muhimu matunzo tu tafuta dume zuri na tetea hapo hakikisha unanunua mbegu kutoka sehemu tofauti ili usifuge wa ukoo mmoja,andaa sehemu nzuri ya kuwaweka na chakula tafuta pumba ya mahindi unawawekea kwenye chombo na pembeni unawawekea maji mengi ya kunywa wao ni maji tu halafu ili wapate vitamini kila siku iwe unawatupia mboga za majani na mabaki ya vyakula mbona utafurahi sana kuhusu dawa mimi huwa siwapi dawa yoyote wao hawana shida
Asante sana mkuu kwa maelezo mazuri,, vip kuhusu aina ya mbegu kama alivyochangia mheshimiwa mmoja hapo juu kwamba , rangi nyeupe ni nzuri kulingana na soko, kwa upande wako unasemeaj kuhusu hilo,

Pia katika ufugaji huu ninaoenda kuuanza , unaweza kukadiria idadi ya chini ya kuanza nayo isipungue kiasi gani ili lengo la kufuga kibiashara liweze kutimia

Nashukuru sana kwa ushauri…!!
 
Asante sana mkuu kwa maelezo mazuri,, vip kuhusu aina ya mbegu kama alivyochangia mheshimiwa mmoja hapo juu kwamba , rangi nyeupe ni nzuri kulingana na soko, kwa upande wako unasemeaj kuhusu hilo,

Pia katika ufugaji huu ninaoenda kuuanza , unaweza kukadiria idadi ya chini ya kuanza nayo isipungue kiasi gani ili lengo la kufuga kibiashara liweze kutimia

Nashukuru sana kwa ushauri…!!
mkuu kama ni hao bukini hebu pitia hapa ujisomee jinsi ya kuwafugaKILIMO BORA: UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI
 
Hapana mkuu,, mimi nahitaji hawa wa kienyeji
ok kama ni hawa wa kawaida huwa awana shida ni wewe tu utaangalia unakiasi gani na utaangalia uanze na wangapi maana uwiano wao dume moja linapanda majike manne hadi sita cha kwanza inatakiwa uwandae mazingira ya watakapo ishi huwa inapendeza kama utawatengenezea fensi kwenye sehemu yao ya kupumzika jioni ndio wanaingia bandani,jiandae pia kuwalisha vizuri na maji wapate ya kutosha
ANGALIZO:hao bata ukiwatunza kiusafi wanakuwa wasafi kweli mfano huu
8ab477eafbaf982d23549daa8967bb4a.jpg

ukiwatunza kiuchafu wanakuwa wachafu kweli hadi wanakuwa hawapendezi mfano huu
ad76b4ec6d28d2624486b4bf762f63f0.jpg
 
Sijajua kipi kimekufanya uache kuku navyoona Bata ni wazuri hawana nagonjwa mengi na gharama kubwa ni pumba na maji tu Lkn sijaona Soko kama la kuku, unaweza kimbilia Bata na ukawapata Lkn Fanya utafiti kabla kwa wanaofuga ili ujue soko lilivyo binafsi Naona kuku wowote wale wana soko kubwa na la hakika
 
Ahsante kwa maneno mazuri ila inakuwa vyema kutiana moyo, sio kutishiana.
Siyo kama anatisha, anasema uhalisia, ni vizuri kuambiwa ukweli ukajua hali halisi na namna ya kupambana kuliko kutiwa moyo kufanya jambo usilolijua ugumu wake. Bora kujua ukweli kuliko kudanganywa ukafanya, ukija kushindwa utakata tamaa kabisa!
 
Kwa bata huko nimeonja mafanikio, muda si mrefu nitawakaribisha wadau walioko Mwanza tukale bata sehemu nitakayowatangazia.
Mkuu kama hutojali naomba unipatie mawasiliano yako nikutafte ,, coz mimi pia nimeanza ufugaji huu wa bata but sijapata details za kutosha kuhusu huu ufugaji, so kam hutjali naomba unisaidie kupata mawasiliano yako kwa ushauri zAidi,, niko Mwanza pia
 
MORIA... upo wapi .... I have the same idea ya kufuga in large scale kwa matunzo ya kisasa zaidi .... nimejaribu kuwatunza watoto 11 wa bata walioanguliwa mwezi wa 7 kwa kuwapa broiler starter in first three weeks na baade kuwapa growers mash ikichanganywa na portion ya pumba za mahindi na matokeo ni mazuri sana ... watoto hawa sasa ni wakubwa sana with a high yield in growth

ninachotaka kufanya sasa hivi ni kununua mayai ya bata kwa wafugaji mbalimbali na kuyapeleka kuanguliwa kwa incubator machine .... naanza na mayai 50 ... then from there I can propel the project well

kumbuka bata wanakuwa vizuri kwa malisho ya majani (grazing) na maji kwa ajili ya spreening
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom