Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Nimesoma maelezo yako nlichokiona ni hivi .Usafi wa mabanda unaweza kua sababu ya kupata maambukizi ya vijidudu mbali mbali kwenda kwenye macho .

Kadhalika upungufu wa hewa safi kwenye banda yan mkusanyiko wa kinyesi kwenye mabanda na uchafu mwingine kinyesi cha ndege kama bata kinazalisha hewa ya ammonia ambayo ikizidi kwenye banda kutokana na labda kutokuwepo kwa madarisha au nyavu ya kuingiza hewa safi ya kutosha mwisho wa siku inaingia macho na kuaribu cornea za jicho na mwisho linapofuka (wengi ni umri mdgo kwakua maumbile yao ya macho yanakua ayajakomaa)
La kuongeza ni kua hewa ya ammonia inaingia kwenye mfumo wa hewa pia na kuaribu mapafu taratibu mwisho wa siku wanakufa (ndo maana madaktr kwenye postmortem wamekwmbia ni pneumonia maanake walikuta mapafu yameadhirika na bila shaka sababu ni hewa chafu yanayovuta)
Nimefuga bata wa kienyeji, wanasumbuliwa na ugonjwa wa upofu (macho kutoona) na ugonjwa huo huwapata bata kuanzia wiki 3 hivi hadi miezi 3 na wakipata wanakufa.
Niliongea na mtaalamu wa mifugo akanieleza ni ndui, hivyo nikawapatia wote chanjo ya ndui. Tatizo ni kwamba ni kama wiki sasa wameanza tena kuumwa ugonjwa huo wa upofu na kufa.
Naomba msaada wana jamvi ili mnifahamishe dawa ya kutumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom