Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Thanks...naweza kupata contacts za hao eden fish farm or hao polo polo fish farm
+255 755 200 335
POLOPOLO Farm Investiment LTD,
BOX 28121
KISARAWE, COST REGION
TANZANIA
Eden fish farm
255 767 979 484
Mkuu uwe unajaribu kutumia search engine kutafuta mawasiliano ya kampuni unazohitaji.
 
Ndugu Nina lengo la kuingia kwenye ufugaji wa samaki mi naomba kwa wajuzi wanipe ushaur mahitaji haswa issue ya mtaji.
 
Kuna aina 3 za ufugaji ambazo ni intensive semi intensive na extensive,.

Ya kwanza ni ufugaji wa kibiashara nikimaanisha samaki wengi, chakula kingi, dawa na uangalizi wa karibu lakini katka eneo dogo.

Yapili ni ufugaji unaofanywa na watu wengi, samaki wachache eneo kubwa, na ya mwisho samaki wanawekwa kwenye eneo kubwa sana na hawategemei ulishaji
 
Ufugaji Wa Samaki Ni Tasnia Pana Kidogo Lakini Ni Rahisi Kuitekeleza Kuliko Ufugaji Wa Wanyama Wengine, Sehemu Nzuri Ya Kuanzia Mtu Kama Wewe Ni Kuonana Na Mtaalamu Akupe ABC Zake Na Ikiwezekana Upate Bussiness Plan Ambayo Itakuwa Na Mchanganuo Wa Kila Kitu.
Mimi Ni Mtaalamu Wa Tasnia Hiyo Kwa Zaidi Ya Miaka 14, Njoo INBOX Tutete Kidogo

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
 
Ungefafanua unahitaji ufugajk upi, na samaki wa aina gani ingekua vizuri zaidi
Kwa maeneo haya nataka nifuge Sato Na kambale.vifaranga wanapatkana kiurahisi kidog.nia yangu ni ya kibiashara zaid .maana naona eneo nililopo samaki hawapatikani sana ..
 
Ufugaji Wa Samaki Ni Tasnia Pana Kidogo Lakini Ni Rahisi Kuitekeleza Kuliko Ufugaji Wa Wanyama Wengine, Sehemu Nzuri Ya Kuanzia Mtu Kama Wewe Ni Kuonana Na Mtaalamu Akupe ABC Zake Na Ikiwezekana Upate Bussiness Plan Ambayo Itakuwa Na Mchanganuo Wa Kila Kitu.
Mimi Ni Mtaalamu Wa Tasnia Hiyo Kwa Zaidi Ya Miaka 14, Njoo INBOX Tutete Kidogo

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
Za mchana boss naweza nani pata mchanganuo..nataka fuga sato au Kambale nna tank Lita 200 yale

Sent from my TECNO DP7CPRO using JamiiForums mobile app
 
Ninaweza Kupatia Mkuu, Ila Kwenye Tenki Kama Hilo Hutapata Mafanikio Zaidi Labda Uliboreshe Kwa Kuweka Mifumo Itakayosaidia Kusafisha Maji Na Kuongeza Oxygen, Hebu Nicheki Kwa Namba Hii 0659841995

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
 
Mi sihitaji kutumia tank nataka nitengeneze ka bwawa kwa ajir hiyo hiv haiwezekani kweli?
 
kwa anaefahamu soko la hawa samaki wa kufuga tafadhali....kama kuna madalali naomba namba zao pia. napatikana Dar es salaam.
 
Nitafte kwa 0759741303 nikupe ABC za ufugaji wa samaki. Mimi ni mfugaji na mzalishaji wa vifaranga vya samaki.

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nahitaji kufuga samaki maeneo ya moshi ,je vifaranga napataje kwa ukaribu ukiacha wanaopatikana mwanza na dar?
 
Unaweza nisaidia contacts zao mkuu?? nasikia huwa wanatabia ukitaka monosex wanakuchanganyia hii changamoto unaweza epuka nayo vipi ndugu?? Na kwenye chakula hivyo vyakula vyote huwa vipo in form of pallets maana niliwahi sikia Hills wao ndio chakula chao huwa in form of pallets hiyo imekaeje ndugu??
Hiyo inatokana na maandaliz hafifu ya kuzalisha hao samaki.+255758991232 piga hiyo ruvu fish farm. Vyakula wote ni pellets. Best quality kwa mtitiriko wa ubora ni Ruvu, Hills na Farmers Centres
 
Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).



Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

N:B
Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.
Je, Inawezekana kuchanganya kambare na sato ndani ya bwawa moja?
 
Kwema humu, Naombeni msaada katika hili wadau je nipo sahihi au??

Katika mita 30 kwa 20 ni sawa na mita za mraba 600
Hivyo basi kwa eneo kama hilo linaweza hifadhi samaki hadi 12,000 kwa kutumia ufugaji wa semi intensive (yani samaki 20 kwa kila mita ya mraba)

Na samaki hula jumla gram ngapi mpaka kufikia uzito wa soko?

Wakuu nipo sahii katika hili kama sipo sawa naombeni mniweke sawa.

Ha Muji
 
Kwema humu, Naombeni msaada katika hili wadau je nipo sahihi au??

Katika mita 30 kwa 20 ni sawa na mita za mraba 600
Hivyo basi kwa eneo kama hilo linaweza hifadhi samaki hadi 12,000 kwa kutumia ufugaji wa semi intensive (yani samaki 20 kwa kila mita ya mraba)

Na samaki hula jumla gram ngapi mpaka kufikia uzito wa soko?

Wakuu nipo sahii katika hili kama sipo sawa naombeni mniweke sawa.
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom