Wernery G Kapinga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 372
- 119
OK yanapatikana wapi hayo...!
Mkuu kwa hapa nchini sina uhakika sana kama kuna kiwanda kinatengeneza hizi tanki, ila kama una uhitaji wa haraka ni bora uagize nje hasa china kuna viwanda vingi wanatengenezaOK yanapatikana wapi hayo...!
Inawezekana pia, au waweza chimba kibwawa chako ukubwa unaotaka, badala ya kusakafia unatumia zile plastic liner ili kutoruhusu maji kunyonywa na udongo.Ok basi naweza kufanya mautundu Kutengeneza la simtank.. Nitakata hata mara bili.....!
Nimesikia ufugaji wa Samaki kwa kutumia bwawa dogo la plastiki nyumbani ni mkombozi tosha wa Maisha. Nahitaji msaada wenu wadau. Je bwawa hilo la plastic liwe na vipimo gani? Hayo maplastic yanauzwa bei gani?
Ati sehemu kama Mbeya Kwenye Baridi baridi waeza funga samaki aina ya Sato.!?Wana JF
Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.
Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.
Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.
Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.
Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.
Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.
Nawasilisha kwa michango yenu.
Nteko Vano Maputo
Penye nia pana njia
--------------------------
-----------------------------
*Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments
NDIO UNAFUGA VIZURI TU, NIMEONA KWA MACHO YANGU KAMBALE PALE TUKUYU MWAKA JANA, WAKATI ZAMANI NILIAMINI KUWA KAMBALE NI WA MAJI JOTO.Ati sehemu kama Mbeya Kwenye Baridi baridi waeza funga samaki aina ya Sato.!?
Mimi ninao Hawa samaki naatafuta soko niwauze nawapatajeKaribu sana kiongozi.
Samaki huugua mara kwa mara?Maelezo mazuri ila umesahau kuongelea magonjwa yanayonyemelea samaki na tiba zake.