Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

mimi niayo sehem mzuri kwa ufugaji wa Samaki ni Kisemvure Mkranga nauza nitafute 0655841348
 
Ndio ina wezekana kutengeneza katika eneo hilo..Unajua samaki wanataka maji na hua yana pungua kila siku kwa sababu mbali mbali kama evaporation.

Kwa swala la mvua zikiisha maji kupungua na kubaki ivo vijisima ni laxima viwe na maji ya kutosha maana lazima uwe na steady supply ya maji.

Na swala la kufurika ilo bwawa au mabwawa wahitaji kujengea na uchimbe mifereji ya ku divert maji sehemu nyingine ili yasi pite ndani ya bwawa otherwise samaki watatoroka na hayo maji yanayo furika.

Ninge kushauri kujengea mabwawa hayo kama ni wa biashara maana hata uvuaji una kua ni rahisi zaidi,Na pia changamoto ya vyura una ikwepa.chura ni adui mkubwa wa samaki sana sana vifaranga kabla havija kua.

Hope iyo ita kusaidia.
 
Habarini...nina samaki wakubwa waku fugwa washafikia mda wa kuuzwa wana mwaka na kitu.Wapo wengi na natafuta soko la kuwatoa wote...

Yapo mabwawa mawili makubwa yote ya kuvunwa.Ambae ana jua ama clue anicheki kwa message.Asanteni
 
Habarini...nina samaki wakubwa waku fugwa washafikia mda wa kuuzwa wana mwaka na kitu.Wapo wengi na natafuta soko la kuwatoa wote...

Yapo mabwawa mawili makubwa yote ya kuvunwa.Ambae ana jua ama clue anicheki kwa message.Asanteni

Upo mkoa gani?
 
Ni ule upumbavu wa kuamini kila kitu kinachosemwa ukitoa wanavosema watanzania.
Mkuu mimi Sina Ushabiki nachoweza sema kile nachokifahamu. Watu wanachukulia kama kwamba ni Ubishani wa ligi fulani no. Tunaweza kuendelea kwa vitu fact na sio kupoteza watu Maboya.

Naona Jamaa kana kwamba anakutetea kwa kusema kwako ati kuwa nimedharau na namkubali Mhindi aliyenipa Somo la ufugaji wa Samaki kwa Njia bora na zisizo na ghaarma za uendeshaji, anyway kama tumeshindwa kuendelea kwa kushauriana its fine sina neno kizuri kila anayesoma anapata mwanga fulani na kuweza kuchagua kipi bora kwake au kipi anaweza kukiafford mwenyewe... Ila Mimi Nashauri tufuge ili tuwe Matajiri na sio kuganga Njaa.

Mimi nilifika kiwandani pale vingunguti ambapo ndio naweza sema wao ndio big dealer kuhusu Samaki na wanafuga huko Mafia, so nina mifano Hai sio maneno maneno.
 
N
Uchimbaji wa bwana unategemea na ukubwa wa bwawa,ukitaka kazi na bwawa likae vizuri inakuhitaji uwe na excavators ila pia wapo watu wanachimba ila wanachukua mda mrefu sana. Kwa mfano nimechimba na excavator size ya 43mx15m kwa shilling 700,000 arusha.
Naomba nifahamishe ulipo hapa Arusha nijekutembelea hilo bwawa namba zangu ni 0784887159.
 
MUONGOZO WA JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI (ARTIFICIAL FEED) SATO (PELEGE).

Jinsi ya kuweza kupata au kutengeneza chakula kilichobeba virutubisho vyote muhimu ya vyakula mjumuisho wa virutubisho muhimu ambavyo vitasaidia samaki katika ukuaji wake mzuri bila matatizo. Hakikisha chakula unachotengeneza kinakuwa na virutubisho vifuatavyo ili uweze kufahamu vyema ni vitu gani ambavyo vinabeba virutubisho hivyo:

· Protein, ( kiini rishe)

· Carbohydrate (wanga)

· Fat /lipid (mafuta)

· Vitamin (vitamin)

· Minerals (madini)


· Viritubisho hivyo vitano ni muhimu kwa samaki kwa sababu kila moja ina kazi yake ndani ya mwili wa samaki husika ambaye anafugwa.

· Chakula cha samaki hutengenezwa kulingana na aina ya samaki husika : mfano samaki aina ya Nile Tilapia (sato, pelage) Grouper (cehewa) mwatiko ( milk fish) Cat fish (kambale) mchanganyiko wake huwa tofauti tofauti

· Muongozo huu ni maalumu ni kwa ajili ya samaki aina Tilapia (sato, pelage)

MAHITAJI

v Fish meal ( unga wa dagaa) protini ya mnyama

Uwe umesagwa kwenye hali ya ungaunga (powder form ) kazi kubwa ya protein hii ni kufanya mwili kukua vizuri ,protini hii huitajika kwa wingi zaidi hasa kipindi ambacho samaki huwa mdogo na katika lika la samaki mzazi.

v soya bean(soya lishe) protini ya mmea

hii nayo ni aina protini ambayo hufanya kazi ya kuimalisha mwili na kukua kwa samaki vizuri,pi protini hupayikana katika mimea jamii ya mikunde,unachemsha kidogo,unazianika mpaka zikauke alafu unazizaga ili ziwe kwenye hali ya unga unga,hutumika kwa wingi katika cha samaki anapo kuwa mdogo sana kipindi anachofikia kuwa mzazi(broder fish)

v rice bran,maize bran (pumba za mpunga,pumba za mahindi).

Hiki ni chakula jamii ya wanga (carbohydrate) ambayo hufanya kazi ya kuongeza nguvu ndani ya mwili wa samaki,pumba lazima ziwe zimesagwa vizuri na kuwa katika hali ya unga unga ili kumpa nafuu samaki katika ulaji wake,huchanganjwa zaidi kipindi ambacho samaki yupo katika lika la kati (grow out).tunapendekeza sana kuanza kutumia pumba za mpunga ni nzuri zaidi ila kama hazipatikani unaweza pia kutumia pumba za mahindi

v Cassava flour,wheat flour (unga wa mhogo,unga wa ngano)

Hii nayo ni aina mojawapo ya chakula aina wanga ambayo husaidia katika kumpa samaki nguvu ndani ya mwili wake,kazi nyingine husaidia kuviunganisha virutubisho vyote kuwa kwenye sehemu moja (single compound) hivyo humfanya samaki kula virutubisho vyote kwa wakati moja,tunapendekeza kuanza kutumia unga wa mhogo ila kama haupatikani basi unaweza kutumia unga wa ngano.

v Copra meal,sun flower cake (machicha ya nazi,mashudu ya alizeti).

Hii ni aina mojawapo ya virutubisho aina ya mafuta ambayo hufanya kazi ya kunenepesha mwili wa samaki vizuri.

v Vitamin mineral mix,premix and D.I GROW .

Hivi ni aina za vitamin na madini ambayo hufanya kazi ya kuimarisha mifupa na kulinda mwili wa samaki kwa ujumla dhidi ya magonjwa na mashambulio mengine,endepo vitamin mineral haipatikani katika mazingira yako unaweza kutumia premix ya kuku wa kisasa ya kukuzia kwa ya kukuzia samaki wako kwa sababu vitamin na madini yake yanafanana katika utengenezaji wa chakula,na hiyo pia kama haipatikani unaweza pia kutumia D.I GROW kwa ajilia ya kutengenezea chakula chako.

KIWANGO KINACHOHITAJIKA KATIKA UCHANGANYAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI AINA YA NILE TILAPIA.

KANUNI (namba ziko katika asilimia)

1.UNGA WADAGAA=18.25

2.SOYA LISHE=25

3.PUMBA ZA MPUNGA/MAHINDI=36.42

4.MACHICHA YA NAZI,MASHUDU YA ALIZETI=10

5.UNGA WA MHOGO/NGANO=6

6.VITAMIN MINERAL MIX,PREMIX AND D.I GROW=4.33

MFANO TUNATENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI CHA KILO HAMSINI (50 KG).

*namba ya 50,000 kilo ambazo zipokwenye gram hivyo zimebadilishwa kuwa kwenye kilogram.

1.Unga wa dagaa :18.25÷100×50,000=9.125 kg

2.soya lishe:25÷100×50,000=12.5 kg

3.pumba za mpunga/mahindi:36.42÷100×50,000=18.21

4.unga wa mhogo/ngano:6÷100×50,000=3kg

5.machicha ya nazi,mashudu ya alizeti:10÷100×50,000=5kg

6.vitamin
mineral mix,premix.D.I GROW:4.33÷100×50

,000=2.165kg

7.mchanganyiko huo huchanganjwa na maji nusu ya uzito wa chakula,mfano chakula unachotengeneza kilo 50 changanya na maji lita 25.

*lakini maji unaweza kuongeza maji endapo mchanganyiko wako bado ni mkavu sana,na pia unaweza kuanza kuweka maji taratibu mpaka pale utakapo ona mchanganyiko wako unakuwa unashikana shikana,mchanganyiko usiwe na maji mengi sana na usiwe na maji kidogo sana yawe ya wastani.

*usianike chakula chako kwenye jua unapoteza virutubisho vyako katika njia ya mvuke,anika kivulini ili zikauke na upepo.

*hifadhi chakula chako mahali salama ili kisiweze kuoza na kutoa fangasi au ukungu mweupe ambao hutokea kwenye chakula samaki.

*endapo unahitaji kutengeneza chakula kidogo yaani mfano wake unataka kutengeneza chakula cha kilo 25 basi unagawa kwa mbili,machicha ya nazi kilo 5 basi una gawa kwa 2,(2÷5)=2.5kg hivyo chakula cha kilo 25 unaweka machicha ya nazi kilo 2.5

*endapo unahitaji kutengeneza chakula kingi zaidi basi unazidisha mara mbili yake mfano unataka kutengeneza chakula cha kilo 100.pumba za mpunga kwa kilo 50 unaweka kilo 18.21 je kilo 100 naweka kiasi gani?unazidisha mara mbili 18.21 ×2=36.48.hivyo unajua chakula cha kilo 100 unaweka pumba za mpunga kilo 36.48.

*lishia samaki wako chakula hiki mara mbili kwa siku asubuhi katika hali ambayo kiwango cha jua hakijawa kikubwa na jioni juu linapokuwa limepungua.

*kiwango cha kulishia samaki wako njia rahisi ni siku mbili za mwanzo ndizo zitatoa majibu samaki wako wanahitaji kula kiasi gani,kama siku ya kwanza uliweka kiwango kadhaa wakabakisha basi kesho yake punguza kipimo mpaka uone sasa chakula unachowapa kinawatosha na hawabakishi.
 
Kama Mimba ya Binadamu...

Idea Zingine unaweza kugeuka Masikini kwa muda mfupi.... Gharama zote hizo siku unavuta unaishia kulipa madeni... Deal kama hizi uwe na kipato kingine cha kuendesha Maisha

Kama Mimba ya Binadamu...

Idea Zingine unaweza kugeuka Masikini kwa muda mfupi.... Gharama zote hizo siku unavuta unaishia kulipa madeni... Deal kama hizi uwe na kipato kingine cha kuendesha Maisha


Mwazoni unapo weka vifaranga aina ya sato ndo utatakiwa usubiri mpaka miezi minane (8) ndo uvune samaki lakini baada ya hapo utakuwa unavuna kila baada ya miezi mitatu mitatu
 
Mwazoni unapo weka vifaranga aina ya sato ndo utatakiwa usubiri mpaka miezi minane (8) ndo uvune samaki lakini baada ya hapo utakuwa unavuna kila baada ya miezi mitatu mitatu
Biashara Pasua hiyo... na unatakiwa uwe na mtaji mkubwa sana ili kuwa millionea au sio kwa kutafuta pesa ya kula tu
 
Mimi natafuta soko la samaki wa maji chumvi, kamba kochi, changu, pweza, prawns etc mwenye kuhitaji anipm
 
Back
Top Bottom