Pata ushauri, michango, mawazo juu ya Ufugaji wa Samaki


tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
12,910
Likes
15,035
Points
280

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
12,910 15,035 280
  • Fahamu aina za mbolea za kurutubisha mabwawa na jinsi ya uwekaji mbolea
  • Na kwa wale wanaotaka kufuga samaki na kuku kwa wakati mmoja pia tunatoa huduma hiyo kama vile kujua idadi ya kuku .
  • Fahamu namna ya uchimbaji wa mabwawa katika maeneo mbalimbali.
  • Vile vile tunandika mpango kazi (business plan ) ya kukuwezesha kufahamu faida ya ufugaji samaki utaipata vpi
Tupigie cmu no 0759678821 au 0625939789
mkuu hebu niambie nataka kufuga samaki, niambie ni chakula gani napaswa kuwapa, kujua magonjwa nk?
 
Joined
Dec 9, 2017
Messages
26
Likes
3
Points
5

Nyamtukila

Member
Joined Dec 9, 2017
26 3 5
Utangulizi

Kitu muhimu cha kuzingatia wakati wa ufugaji wa samaki ili kuongeza uzalishaji ni kuwalisha samaki chakula ambacho kipo kamili (balanced diet). Mfugaji hapo nyumbani unaweza kutengeneza chakula chako hapo nyumbani kama upon a malighafi zifuatazo pumba za mahindi pamoja , mashudu , dagaa,pumba za mchele katika mchanganyiko maalamu ambao utatoa chakula bora kwa ajili ya kuwalisha samaki wako


Jinsi ya kuwalisha samaki

Baada ya kutengeneza chakula chako kwa ajili ya samaki, hakikisha unasimama katika pembe moja yapo ya bwawa la samaki na fanya kurusha chakula kwa kutumia mkono wako katika muda maalumu ambao huo muda ndio utakuwa muda maalamu kwa samaki kula chakula chao.

Baada ya kurusha chakula anza kutazama kama samaki watakikubali chakula ulichowapa hii itajidhirisha kwa samaki kula chakula na wao watajenga mazoea kuibuka muda huo kuja kula chakula na katika pembe husika uliyowarushia samaki…. Na kwa kawaida samaki huchukua takrabi dakika kumi na tano kula chakula.

Muda wa kuwalisha samaki

Kwa kawaida tilapia (sato) hutumia muda mwingi kunywa maji na hula chakula kidogo sana kwa kuwa huwa na matumbo madogo. Na kwa kawaida unatakiwa kuwalisha sato katika muda wa saa4 asubuhi na saa10 jioni hii ni kwa sababu joto la maji pamoja na kiwango cha oxygen (dissolved oxygen) huwa juu sana.

Na hakikisha unazingatia muda ambao unautu ia kuwalisha samaki na sehemu husika ambayo uitumia kuwalisha samaki na mtu ambaye hutumika kuwalisha samaki anatakiwa kuwepo muda wote na aipende kazi yake.

Faida za kuwalisha samaki kwa kutumia mkono

Kuna njia mbalimabli ambazo mfugaji anaweza kuzitumia kwa ajili ya kuwalisha samaki lakni mkulima anashauriwa kuwalisha samaki kwa kutumia mkono ili kuweza kuwaangalia kama samaki wako katika hali nzuri(afya) kwa kuwaangalia jinsi wanavyokula kwa kawaida samaki wanapoona chakula hufurahia na huwa katika staili fualni hivi ya kupigania chakula nje ya hapo ukiona samaki hayuko katika hali hiyo jua kuwa kuna tatizo…

Vifuatavyo huweza sababisha samaki wasiweze kula chakula kama hapo mwanzo:

  • Maji ya bwawa yaweza kuwa baridi
  • Kiwango cha oxygen (dissolve oxygen) kipo chini
  • Samaki wanaweza kuwa wagonjwa
  • Samaki baadhi wanaweza kuwa wamekufa
  • Chakula kinaweza kuwa kizito ambavyo yaweza pelekea kuzama chini

Kiwango cha chakula anachokula samaki

Wewe kama mfugaji unashauriwa kuwa na record ni samaki wangapi ambao wapo kwenye bwawa lako kwa kawaida pale unapoweka fingerling katika bwawa lako ni vyema kuwa na record sahihi umeingiza vifaranga wangapi wa samaki katika bwawa lako hii itakupelekea wewe mfugaji kujua ni kiwango gani cha chakula kinahitajika kuwalisha samaki katika bwawa lako:

Hapa chini nimeambatanisha jedwali ambalo litakupa mwanga ni kiwango gani cha chakula kinahitajika katika kila umri..


View attachment 621374

Imeandaliwa na

theriogenology


Doctor of Veterinary Medicine


Karibuni kwa maswali na Huduma
heb nisaidie, cjaanza kufuga samaki lakin natak kufaham kitaalam samaki hula kias gani cha chakula kwa siku nzima?
 

theriogenology

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Messages
6,238
Likes
9,780
Points
280

theriogenology

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2016
6,238 9,780 280
heb nisaidie, cjaanza kufuga samaki lakin natak kufaham kitaalam samaki hula kias gani cha chakula kwa siku nzima?
8a2e640fc61dbab06248f206ab8d6bb7.jpg


Ukiangalia jedwali hapo juu inategemea na ukubwa wa samaki mkuu.....

Na mara nyingi unapowapa chakula samaki mara nyingi huwa wanakuja usawa ma maji kula chakula na ukitaka kujua kuwa wameridhika na chakula unapokuwa unarusha tena chakula kwenye maji hutowaona wakija juu kula chakula hapo ndipo utajua ya kuwa wametosheka na chakula mkuu....

Na ukiona kwenye jedwali hapo juu kwenye picha utaona kabisa samaki wa mwezi mmoja anakula kiasi cha gram 1 mpaka 2 na yule wa kuanzia miezi mitano anakula gram 4 za chakula...

Nadhani nitakuwa nimejaribu kukuelewesha mkuu....
 
Joined
Dec 9, 2017
Messages
26
Likes
3
Points
5

Nyamtukila

Member
Joined Dec 9, 2017
26 3 5
8a2e640fc61dbab06248f206ab8d6bb7.jpg


Ukiangalia jedwali hapo juu inategemea na ukubwa wa samaki mkuu.....

Na mara nyingi unapowapa chakula samaki mara nyingi huwa wanakuja usawa ma maji kula chakula na ukitaka kujua kuwa wameridhika na chakula unapokuwa unarusha tena chakula kwenye maji hutowaona wakija juu kula chakula hapo ndipo utajua ya kuwa wametosheka na chakula mkuu....

Na ukiona kwenye jedwali hapo juu kwenye picha utaona kabisa samaki wa mwezi mmoja anakula kiasi cha gram 1 mpaka 2 na yule wa kuanzia miezi mitano anakula gram 4 za chakula...

Nadhani nitakuwa nimejaribu kukuelewesha mkuu....
Ahsant san mkuu, nafikir sikuweka sawa swali, nilikuwa nalenga zaid ufugaji wa samaki katika matenki, maana katika mabwawa samaki hupata pia chakula cha asili, sasa je kwa hawa wa kwenye matenki (intensive aquaculture) wanalishwa kias gani?
 

Forum statistics

Threads 1,203,734
Members 456,939
Posts 28,126,895