Pata ushauri, michango, mawazo juu ya Ufugaji wa Samaki | Page 28 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pata ushauri, michango, mawazo juu ya Ufugaji wa Samaki

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Malila, Feb 26, 2010.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,479
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Wana JF

  Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

  Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

  Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

  Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

  Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

  Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

  Nawasilisha kwa michango yenu.

  Nteko Vano Maputo

  Penye nia pana njia

  --------------------------

  [​IMG]


  -----------------------------  *Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments
   
 2. BRAVO 2 ZERO

  BRAVO 2 ZERO JF-Expert Member

  #541
  May 5, 2016
  Joined: Jul 16, 2013
  Messages: 898
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  Njoo huku mile 35 kuna mtaalam anafanya hizo kazi atakuelekeza vizuri
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #542
  May 5, 2016
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 14,993
  Likes Received: 19,033
  Trophy Points: 280
  Mkuu hawa wana uzito gani na mmewafuga kwa muda gani??
   
 4. A

  Amenzi Buzinza Member

  #543
  May 5, 2016
  Joined: May 3, 2016
  Messages: 20
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  1. Unahitaji uwe na eneo lenye maji ya kutosha au uwe na kisima kirefu ambacho kina uwezo wa kutoa maji masaa yote.
  2.Upate mtalaamu mzuri wa kuchimba Kisima chenye Urefu wa mita 1.5 ( pref excavator).
  3. Ukishachimba inategemea aina ya udongo uliopo ( soil texture) kama sehemu ina chemi chemi ni nzuri unaweza tengeneza matuta tu halafu maji yakajaa yenyewe,
  4. Unapaswa kupata mbegu nzuri iliyoandaliwa vizuri na yenye kukua.
  5.ulishaji wa hao Samaki ni muhimu kuangalia sana hasa kipindi wanavyokuwa bado vifaranga
  Hayo ndiyo muhimu kwanza
   
 5. A

  Amenzi Buzinza Member

  #544
  May 5, 2016
  Joined: May 3, 2016
  Messages: 20
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  Hawa wana gm 480-500 tumewafuga miezi 8 sasa lakini hawa ni wazazi ndio maana wanakua taratibu kwa sababu tunavuna mayai Ili tupate vifaranga, kwa hiyo kila mara wiki wanasumbuliwa ingekuwa madume kwa ajili ya mboga yamkini wangekuwa wana uzito mkubwa hata gm 800 au zaidi
   
 6. Usangu

  Usangu JF-Expert Member

  #545
  May 5, 2016
  Joined: May 28, 2015
  Messages: 760
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 80
  Elimu zaidi wakuu. Mimi nataka nifuge Kambare na Sato
   
 7. A

  Amenzi Buzinza Member

  #546
  May 5, 2016
  Joined: May 3, 2016
  Messages: 20
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  Hii hapa ni picha ya hatchery yetu tunapoangulia mayai ya Samaki ili kipata vifaranga bora kabisa.

  ImageUploadedByJamiiForums1462460884.199265.jpg
   
 8. Amenn

  Amenn JF-Expert Member

  #547
  May 5, 2016
  Joined: Dec 21, 2015
  Messages: 636
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 80
  Tufundishen na kambale
   
 9. A

  Amenzi Buzinza Member

  #548
  May 5, 2016
  Joined: May 3, 2016
  Messages: 20
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  Aina ya ufugaji wa inchi kavu kwa namna moja au nyingine hautofautiani sana, tofauti ni jinsi ya kupata vifaranga vya Kambale
   
 10. kikonko

  kikonko JF-Expert Member

  #549
  May 5, 2016
  Joined: Aug 8, 2015
  Messages: 519
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Naweza fugia samaki kwenye simtank?.nahitaji kuanza kufuga
   
 11. A

  Amenzi Buzinza Member

  #550
  May 5, 2016
  Joined: May 3, 2016
  Messages: 20
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 5
  Kwenye Simtank watakufa oxygen haiwezi kuwa nyingi kaka!!!
   
 12. Averoes

  Averoes JF-Expert Member

  #551
  May 24, 2016
  Joined: Jan 30, 2014
  Messages: 959
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 80
  Kuna mtu mwenye muongozo wa ufugaji Prawns?
   
 13. N

  Nyasiro Verified User

  #552
  May 24, 2016
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 1,287
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hao wana umri gani? Naona wapo vizuri.
   
 14. f

  filonos JF-Expert Member

  #553
  May 31, 2016
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  mimi niayo sehem mzuri kwa ufugaji wa Samaki ni Kisemvure Mkranga nauza nitafute 0655841348
   
 15. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #554
  Jun 9, 2016
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,462
  Likes Received: 14,148
  Trophy Points: 280
  Kama mnataka mali
   
 16. c

  crissjohns Member

  #555
  Jun 10, 2016
  Joined: Aug 22, 2014
  Messages: 11
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Ndio ina wezekana kutengeneza katika eneo hilo..Unajua samaki wanataka maji na hua yana pungua kila siku kwa sababu mbali mbali kama evaporation.

  Kwa swala la mvua zikiisha maji kupungua na kubaki ivo vijisima ni laxima viwe na maji ya kutosha maana lazima uwe na steady supply ya maji.

  Na swala la kufurika ilo bwawa au mabwawa wahitaji kujengea na uchimbe mifereji ya ku divert maji sehemu nyingine ili yasi pite ndani ya bwawa otherwise samaki watatoroka na hayo maji yanayo furika.

  Ninge kushauri kujengea mabwawa hayo kama ni wa biashara maana hata uvuaji una kua ni rahisi zaidi,Na pia changamoto ya vyura una ikwepa.chura ni adui mkubwa wa samaki sana sana vifaranga kabla havija kua.

  Hope iyo ita kusaidia.
   
 17. c

  crissjohns Member

  #556
  Jun 10, 2016
  Joined: Aug 22, 2014
  Messages: 11
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Habarini...nina samaki wakubwa waku fugwa washafikia mda wa kuuzwa wana mwaka na kitu.Wapo wengi na natafuta soko la kuwatoa wote...

  Yapo mabwawa mawili makubwa yote ya kuvunwa.Ambae ana jua ama clue anicheki kwa message.Asanteni
   
 18. Dengue

  Dengue JF-Expert Member

  #557
  Jun 11, 2016
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 1,798
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Upo mkoa gani?
   
 19. c

  crissjohns Member

  #558
  Jun 11, 2016
  Joined: Aug 22, 2014
  Messages: 11
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Dar es salaam..
   
 20. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #559
  Jun 26, 2016
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,452
  Likes Received: 1,001
  Trophy Points: 280
  samaki gani broo
   
 21. c

  crissjohns Member

  #560
  Jun 26, 2016
  Joined: Aug 22, 2014
  Messages: 11
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Sato
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...