Pata ushauri, michango, mawazo juu ya Ufugaji wa Samaki


M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Wana JF

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

Nawasilisha kwa michango yenu.

Nteko Vano Maputo

Penye nia pana njia

--------------------------
-----------------------------

Ufugaji wa mabwawa umepitwa na wakati,sasa ufugaji wa samaki ni AQUAPHONIC hii ndio mwisho miezi minne tu una sato wa nusu kilo.just google aquaphonic and learn for your self.

Kwa watakaopenda kuona how Aquaphonic work.siku nzuri ni weekend so Mtam na wengine wote interested tuwasiliane ijumaa ili tupange kama iwe jumamos au jumapili mje muone.

Bagamoyo Pale Chuoni wana mambwawa ya kawaida na wanauza Vitoto vya sato shillingi 50 kimoja. Kambale pia wapo. Kama kuna anayependa kwenda pale Bagamoyo Mbegani for study tour pia twaweza kupanga ila wao wanatembelewa working days tu.so inabidi iwe kati ya jumatatu to ijumaa working hrs.sisi vitoto vya kuanzia tulinunua Bagamoyo,lakini katika vitoto hivyo tutapata wazazi wa mbegu siku zijazo.

Katika ufugaji wa samaki kuna vitu muhimu vya kuzingatia.Samaki wanaokuwa kwa haraka ni Madume.Je utapataje Madume watoto? Ipo Dawa ambayo unaiweka katika chakula cha samaki watoto,baada ya muda 99% ya hawa watoto samaki wanageuka Madume.Kisha wewe unaendelea kuwalisha kama kawaida.

Samaki anaweza kula mchanganyiko wa chakula cha kuku lakini awezi pata virutubisho vyote kwani vingine vitapotea katika maji.
Hili pia ni tatizo kubwa hapa kwetu Tanzania juu ya ulishaji samaki ili wakue haraka. Samaki ili wakue haraka na kwa faida ya mfugaji chakula chake kinatakiwa kiwe katika mfumo wa pallets (kama vigololi vidogo size ya ulezi,mtama au zaidi) hii inamfanya samaki akila chakula katika mfumo wa pallets kumeza all food contents (minerals,protein,starch etc).

Mashine zipo za kutengeneza fish food,nikipata muda wakati nikiwa na PC ntaweza weka some docs za fish food,fish sex convention (how to do it),Aquaphonic and modern fish keeping ,nna docs nyingi sana za haya maswala but at this time nipo Mobile so siwezi attach kwa sasa


UFUGAJI WA SAMAKI

Tasnia ya ufugaji wa samaki inajumuisha ukuzaji wa viumbe vya kwenye maji (bahari na maji baridi) katika mazingira tofauti na yale ya asili. Lengo kuu ni kukuza kwa muda mfupi ili kujipatia lishe, kipato na kutunza mazingira ya bahari, mito, maziwa nk.
Ufugaji unagusa viumbe vya kwenye maji kuanzia mimea kama vile mwani, samaki wasio na mapezi (kaa-crabs, kambamiti-prawns, chaza-oyster, majongoo bahari nk) na samaki wenye mapezi (perege/sato, kambale, kibua, trout, chewa nk).

Aina ya ufugaji

Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo wake:

1. Huria (Extensive farming)

• Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba
• Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton, wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton)
• Hauitaji ubadilishaji wa maji
• Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa

2. Kati ya huria na nusu shadidi (Modified extensive)  Idadi ya samaki, 4-7 kwa mita ya mraba

• Chakula cha asili na chakula cha ziada huitajika
• Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako
• Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima

3. Nusu shadidi (Semi-intensive)

• Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25
• Chakula cha asili na cha ziada
• Huduma ya hewa ya ziada lazima
• Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm)

4. Shadidi (Intensive)

• Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba
• 100% chakula cha kutengenezwa
• Maji ni kuingia na kutoka
• Hewa ya ziada masaa yote
• Eneo linalotumika ni dogo ukilinganisha na mifumo mingine

Miundombinu ya ufugaji

Samaki wanaweza kufugwa katika miundombinu mbalimbali kama ifuatayo:

• Bwawa
• Kina 0.8-1.5m
• Ukubwa 100 mita za mraba- 1ha

• Matanki

Umbo-mstatili au mviringo nk
Kina 1-1.5m
Kipenyo kwa lile la mduara 3-10m
Ukubwa kwa la mstatili inategemea na uwezo lakini lisiwe kubwa ili kuhimili nguvu ya maji
Materials: Plastic, cement, chuma nk
NB: Simtank linafaa( Faida inapatikana kama utalitumia kwa intensive system)

Vizimba (Fish cages)
Huwekwa katika maji ya asili kama vile ziwani, baharini au katika bwawa. Vipo vinavyoundwa kwa local materials kama mianzi na vipo vya aluminium.

Eneo linalofaa kwa ufugaji

Baadhi ya maeneo yanayofaa ni yale mashamba ya mpunga, na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji. Zifuatazo ni sifa za maeneo yanayofaa:

1. Udongo: Mfinyanzi husaidia kupunguza gharama za ujenzi wa bwawa na maji kwakuwa linaweza kutuamisha maji na kuruhusu maji yasipotee. Likiwa la kichanga bwawa ni lazima lijengewe au kuwekwa nylon sheet ili kuzuia upotevu wa maji. Unaweza ukahamisha udongo wa mfinyanzi kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kuzuia upotevu wa maji (muone mtaalamu kwa ushauri zaidi juu ya mbinu ya kuhamisha udongo).

2. Chanzo cha maji ya uhakika
Eneo liwe na maji ya uhakika. Vyanzo vya maji ni kama vile mito, bahai, maziwa, chem chem., kisima, maji ya dawasco na mvua. Maji yasiwe na kemikali hatarishi kwa viumbe.

3. Miundombinu ya barabara: Inasaidia kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na samaki wakati wa kuvuna.
4. Eneo lisiwe na historia ya mafuriko ili kuzuia athari za mafuriko kwa miundombinu yako. Utatumia gharama nyingi katika kuimarisha miundombinu yako.Jamii/aina ya samaki
5. Eneo lenye mwinuko wa wastani husaidia katika ujenzi wa bwawa.
6. Miundombinu ya umeme ni sifa ya ziada hususan kwa mkulima wa kati na wajuu kwa ajili ya kutumika katika kuendesha visambaza hewa.
7. Ulinzi muhimu

Note: Aina ya eneo lako ndilo linaweza kukufanya uchague muundombinu gani wa kufugia utumie

Aina ya samaki unaoweza kufuga Tanzania kwa sasa
Maji baridi

Sato/perege, Kambale, Kambamiti wa maji baridi na Trout (maeneo ya baridi kama vile Iringa, Kilimanjaro Arusha na Mbeya) na samaki wa mapambo.

Maji bahari

Kambamiti wa maji bahari, mwatiko, chewa, kaa, chaza wa lulu

Upatikanaji wa Vifaranga vya samaki husika

Vyanzo vya vifaranga ni kutoka katika mito, bahari, maziwa na wale wa kuzalishwa katika vituo vya kuzalishia vifaranga.

Sato na Kambale

Vituo vya serikali Utapata sato wa kike na kiume mixed sex). Kingolwira –Morogoro, LuhiraSongea, Mbegani-Bagamoyo . Kifaranga huuzwa Tsh. 50-100 kwa kifaranga.

Vituo binafsi kama vile Faith aquaculture-Kibamba (DSM) (utapata monosex sato), PeramihoSongea (mixed sex). Monosex huuzwa Tsh. 200 kwa kifaranga, na mixed ni 100 kwa kifaranga.

Trout

Mayai huagizwa toka Marekani, Israel
Kambamiti wa baharini Alphakrust –Mafia.

Chakula cha samaki

Chakula cha asili

Hurutubishwa kwa mbolea ya wanyama kama vile kuku, ngombe, mbuzi nk. Kwa kiwango cha 1000kg/ha. Mbolea ya kuku ni kali hivyo unaweza punguza ikawa 250-500kg/ha.

Chakula cha kutengeneza

Samaki huitaji protein ili akuwe na kila samaki ana mahitaji yake hivyo ni species specific. Formula zipo kwa wale wanaotaka kutengeneza. Tanzania hakuna kiwanda kinachotengeneza. Ingredients zake ni kama vile dagaa, pumba, soya, unga wa ngano, unga wa muhongo nk.

Uvunaji

Kwa kawaida ni miezi 4-6 amabapo unapata 250-400g kulingana na ulishaji wako. Kwa prawns ni miezi 3-6 wanafikia 30-50g ambayo ni ukubwa wa soko.

Tathmini ya uchumi

Perege/sato Mfano:

Ukubwa wa bwawa ni 20m by 30m= 600 mita za mraba
Idadi ya samaki (7 kwa mita ya mraba) kwa monosex tu= 600 x 7=4200 fish
Uzito hadi kuvuna (4-6months)- 250g= 4200 x 250g= 1050kg (Nimesha convert gram to kg) Bei kwa kilo ni 6000-8000 kulingana na mahali= 6milion-8milion.

Gharama unazoweza kutumia
Ujenzi wa bwawa
Kuchimba kwa vibarua ni 500,000-600,000
Kuchimba kwa machine ni 1,000,000-1,500,000 kulinganana mahali ulipo

Kama udongo ni kichanga itabidi ujengee (kujengea ni gharama na inaweza ikafika 3.5-4m kwa gharama zote kuanzia kuchimba hadi kujengea).

Chakula
cha kutengeneza tani 1 inaweza kugharimu laki 7-9. Hapa ili uweze kuzalisha tani 1 ya samaki aina ya perege utahitaji tani 1-1.5 ya chakula.
Gharama ya vibarua 150,000-250,000 kwa mwezi.
Utakuwa na gharama ya chokaa kwa ajili ya kuua vidudu (laki 100,000-200,000), mbolea kuzalisha chakula cha asili (gharama ni 50,000).

Jinsi ya kuhudumia bwawa, kuandaa chakula nitaandaa tips zingine.
Ha Muji

*Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
jambo moja Rahisi sana kwako juu ya mabwawa ya Uvuvi ni kwa wewe kuwasiliana na Idara ya Uvuvi kitengo cha ufugaji viumbe kwenye maji pale Vertinary Temeke, Wizara ya maendeleo ya Uvuvi na Mifugo watakuelimisha vyema maana wao wamesome hayo mambo kwa kina, wanauzoefu wa miaka mingi, watakushauri na mbegu ya kupanda .....kama upo Morogoro nenda kule Kingorwila wanakituo chao pia.

Kumekuwa na ongezeko la wafugaji wanaolalamika kuwa samaki wao hawakui hasa tilapia.

Zifuatazo ni sababu zilizobainika kuwa ndio chanzo cha tatizo hilo:

1. Mfugaji kapata wapi hiyo elimu ya ufugaji

2. Idadi ya samaki wanaopandikizwa kwa mita ya mraba kwa mabwawa ya ardhini na kujengea kwa cement. Kiwango halisi ni vifaranga 5-7 kwa mita ya mraba kwa aina ya monosex na 1-3 kwa mixed sex na sio 10-20 kama inavyoelekezwa na baadhi ya watoa elimu.

3. Chakula feki kinachouzwa mitaani. Watu wanatumia tu pumba na kuwadanganya wakulima kuwa ni chakula special. Nunueni chakula kilichokuwa na label inayoonesha ingredients na percentage yake ikiwemo chapa ya tbs.

4. Ulishaji wa chakula. Wakulima wanalisha chakula kiasi kidogo. Kopo dogo la uhai sio kipimo jamani. Samaki anakula 1/3 ya uzito wakee au lisha mpaka uone hakuna samaki anahangaikia chakula ktk bwawa.

5. Uzito wa samaki mmoja ndani ya miezi 6 ni 200-400 g tena hiyo 400 uwe umefanya management ya nguvu. Hii ni kwa bwawa la ardhini na kujengea. Sio kilo moja kama mnavyoamonishwa.

Hitimisho: Kabla ya kuanza kazi za ujenzi na ufugaji tembelea wataalam Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanapatikana Temeke vetenari
 
newmzalendo

newmzalendo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
1,370
Likes
90
Points
145
newmzalendo

newmzalendo

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
1,370 90 145
wazo zuri sana kufuga samaki kibiashara.
Mwaka jana nilianza utafiti jinsi ya kufuga,nashauri uende kunduchi,kuna kitengo cha ufugaji samaki,pia nina rafiki yangu ambaye ni mtaalamu wa samaki,ni PM ntakupa namba yake,na mpange jinsi ya kuonana awe anakupa ushauri.
Fuga samaki wa ziwa victoria-Sato etc kwani wateja ni wengi na pia utakuwa na gharama ya usafiri from kibaha to DAr,
wish u all the best in ur project
 
N

Namdawa

Member
Joined
Oct 13, 2009
Messages
36
Likes
4
Points
0
N

Namdawa

Member
Joined Oct 13, 2009
36 4 0
kuna wakati nilieleza kuwa nilihudhuria semina ya ufugaji wa samaki kwa kweli nami nilivutiwa sana na waalimu ambao walikuwa wanatoa mada.Kweli kama mtu unataka kufanya biashara ya samaki lazima kweli uwe umedhamiria sana na kuipenda biashara hii (INTEREST).

kwani kama unataka kufuga samaki angalia mazingira yako kama ulivyosema.Umesema kuna maji mengi tu na ninaamini kuwa yanatuama ndio maana ulipochimba wakati wa kiangazi hayakukauka.kwa maana nyingine hapo kwenye eneo lako kuna udongo wa Mfinyanzi ambao unafaa sana kwa kilimo hiki cha samaki.Japo pia unaweza kulijengea vema tu cement na kwa utaalamu bado ukafuga.

Lakini pia unaweza kutengeneza bwawa lako katika vyanzo vya maji vya uhakika kama vijito,chemichemi au mifereji.Pia kwenye udongo unaofaa,eneo lenye mwinuko wa wastani pia lililo karibu na unakoishi kwani bwawa lako linatakiwa kuwa karibu na wewe ili uweze kulilinda na pia kuliangalia kwa namna nyingi kama kulisha chakula n.k pia liwe kwenye eneo lenye miti ili kuleta kivuli.

Hii ni kwa manufaa ya wengine.Kuna umuhimu sana wa kuhudhuria semina hizi zinazotolewa kwani Zinajenga sana na unaendelea kuwasiliana na waalimu wako siku zote.Hawa Africa Upendo Group ndio wanaoendesha semina hizi.kuna njia za kupima udongo kama unafaa.Pia kabla ya kuweka samaki unapaswa kurutubisha bwawa lako vema.yaani liwe na vyakula vya asili vya utosha.unarutubisha kwa kutumia vitu mbalimbali kama mbolea mimea n.k baada ya muda unaweza kupanda vifaranga vyako na kuwapa chakula na mbolea na kuleta ile rangi nzuri ya kijani katika maji na hewa.Samaki anakula vyakula vya kawaida sana ambavyo vinapatikana kirahisi na nikidogo tu bila gharama yoyote kubwa.Hata wadudu bado ni chakula kwao.

samaki hawatakiwi kuwekwa kwenye kina kirefu sana ni kama mita moja tu kwenda chini na inategemea unataka ukubwa gani kama 10 kwa 10 wanaweza kukaa hata samaki elfu kumi hata laki kutegemea na aina ya samaki.Nile-Tilapia ni mbegu nzuri sana kwa biashara hasa ukinzingatia leo kuwa wengi wa wafanya biashara hasa mahotelini wanahitaji gramu 250 ukiwa ndicho kipimo kizuri kwa wateja wengi katika mahotel.utalamu wa kufuga Cat fish au kambale ni tofauti sana kwani wale wanaishi ardhini na huzaana sana wakati wa mvua na mafuriko.Hwazai kabisa kama utawafuga kama hawa samaki wengine.
 
N

Namdawa

Member
Joined
Oct 13, 2009
Messages
36
Likes
4
Points
0
N

Namdawa

Member
Joined Oct 13, 2009
36 4 0
Yaani kambale ni samaki mtamu ajabu Malila umesema.Yaani usipime.

Umenikumbusha pasaka nilienda kwetu toka nimefika hadi naondoka ni supu ya asubuhi chakula cha mchana ama jioni lazima kambale pia awepo pembeni tena ukimpata mwenye mayai yake yaani we acha tu.Tulikula na ndugu zangu hata Nyama haikupata soko sana pasaka hii ni siku ile tu ya jumapili pilau kwa sana.

Ninachozungumzia hapa ni ufungaji wake na maongezeko kuzaliana ndio tatizo.Wanazaa sana na watoto wanatawanyika ama kufa kwa wingi wao lakini bado wanazaa sana.

Cha msingi ni kuwafahamu vema na jinsi ya kuwafunga kutegemeana na Mabwawa uyawekeje ili wazaane
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Yaani kambale ni samaki mtamu ajabu Malila umesema.Yaani usipime .Umenikumbusha pasaka nilienda kwetu toka nimefika hadi naondoka ni supu ya asubuhi chakula cha mchana ama jioni lazima kambale pia awepo pembeni tena ukimpata mwenye mayai yake yaani we acha tu.Tulikula na ndugu zangu hata Nyama haikupata soko sana pasaka hii ni siku ile tu ya jumapili pilau kwa sana.
ninachozungumzia hapa ni ufungaji wake na maongezeko kuzaliana ndio tatizo.Wanazaa sana na watot wanatawanyika ama kufa kwa wingi wao lakini bado wanazaa sana.Cha msingi ni kuwafahamu vema na jinsi ya kuwafunga kutegemeana na Mabwawa uyawekeje ili wazaane
Nimetangaza bingo kwa machalii fulani kwamba mtu akiniletea kambale hai hata kama ni mdogo vipi nampa buku tano. Nawatafuta sana hawa samaki. Nimepata sato ila kambale bado. Mategemeo ni makubwa,nikishindwa kuwapata mitaani,nitawafuata mbegani,wapo kule.
 
M

mjukuu2009

Member
Joined
Jul 6, 2009
Messages
91
Likes
0
Points
13
M

mjukuu2009

Member
Joined Jul 6, 2009
91 0 13
Shukurani Muanzisha mada, hii mada ni nzuri sana.

Mimi nilitaraji huu wakati hii serikali inaubiri ''kilimo kwanza'' ndio tungekuwa tunapata Makala mbali mbali za kilimo,ufugaji wa wanyama,samaki.lakini wapi TV lao la TBC ni siasa na redio zao zote ni siasa tu ili CCM ishinde. Ukienda kwenye chuo cha kilimo akuna ata sehemu unaweza pata makala za kilimo na ufugaji,yani mambo ayapo kama inavyotakiwa kwa kilimo kwanza.

Mimi nilitarajia wizara ya kilimo itakuwa ata na makala moja kila week kwenye magazeti yote kwa ajili ya kuamasisha na kufundisha watu juu ya kilimo lakini amna same to wizara ya Magufuli amna kitu. Wengine tunapenda kufuga lakini atuna elimu hiyo sasa aka kaela tulikonako kadogo tunaogopa tusijekingiza kwenye ufugaji ikala kwetu.:sick:
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Mkuu unaendeleaje na samaki kama ulivyoelezea hapo juu. Nimevutiwa sana na moyo wa kushare na wengine vitu vyako.. it is so positive
Nisamehe sana,nilikuwa vijijini kwa muda mrefu kidogo kwa ajili ya mambo yetu haya ya kilimo. Miezi mitatu iliyopita niliweka sato 26 vifaranga,mpaka jana tumerecord sato mmoja kafa,kwa hiyo imenipa nguvu kwamba bwawa langu liko mahali sahihi kabisa kilichobaki ni maboresho,hasa aina ya chakula.

Mwezi juni nilipata Kambale 52,nimewaweka ktk visima vidogo,huku nasubiri bwawa jipya likae sawa,yaani lijijenge kupokea wageni. Kwa mwezi mzima sasa hakuna kambale aliyekufa. Nitakwenda Mbegani/ kunduchi nikachukue shule zaidi ili nifuge kwa wingi. Hapo nitapata mbegu ya kuuza. Mwaka jana kigogo mmoja alikosa mbegu ya kambale,tulitafuta sana bila mafanikio.

Pili,pale Kinguruila gerezani pana mbegu ya samaki inauzwa kwa bei nzuri sana,kifaranga kimoja Tsh 30/ sio 300 kama huku Mkuranga. Contact za mhusika nimepata,kwa aliye tayari aniambie nimpe.

Kwa ujumla ninafurahia kufaulu mtihani wa kwanza,yaani pilot trial niliyofanya.
 
W

wakumbuli

Senior Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
148
Likes
0
Points
33
W

wakumbuli

Senior Member
Joined Aug 20, 2009
148 0 33
Nimefurahi sana kupata changamoto na wadau katika sekta hii,Kwanza kabisa kuna vitu vya kuzingatia katika utengenezaji wa bwawa.

1.Aina ya Udongo lazima uwe wa Mfinyanzi
2.Maji means uhakika wa maji
3.Sehemu yenye muinuko kidogo
4.Mimea iliyozinguka eneo lako sbb kama kuna miti mingi ndege watakusumbua
5.Njia za mawasiliano means barabara ukizingatia hiyo ni bidhaa inayoharibikia haraka zaidi

BWAWA UNAWEZA KULICHIMBA LENYE UKUBWA TOFAUTITOFAUTI KULINGANA NA UKUBWA WA ENEO HUHUSIKA NA ENEO LAKO LILIVYO,ILA UNASHAURIWA KUCHIMBA BWAWA LENYE UMBO LA MSTATILI

Ni vyema ukamtafuta mtaalamu wa maswala ya uvuvi Makao makuu DSM,NA MIKOANI PIA WAPO WATAALAM WA UVUVI ili uambatane naye kwenye eneo husika sbb vipimo vitabadilika kulingana na eneo.

USHAURI HYUWA NI BURE HAKUNA GHARAMA YOYOTE SSB HILO NI ENEO LAKE LA KAZI
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Nashukuru kwa msaada wa material hizi, ni lazima tubobee ktk shughuli hizi lakini tukiwa na maarifa na elimu juu ya jambo tunalotaka kubobea nalo. Natumia makala hizi kurekebisha makosa madogo madogo ya kazi ambazo mimi nimefanya tayari na jamaa zangu nitawasaidia wasifanye makosa ( kwa mfano,kujua shughuli za jirani yako ili zisije kukuharibia quality ya samaki nk).

Kabla hatujaingia ktk ujenzi wa bwawa ni vizuri pia utuambie aina ya samaki unaotaka kuwafuga ndugu( Nile perch,Tilapia,kambale,sato,kitoga au blackbassa) Kuna samaki hawataki matope wanataka clear water na wengine wanaweza kuishi ktk tope,pili lazima ujue PH ya hapo unapotaka kujenga bwawa,vinginevyo utajenga na samaki hawatazaliana. Angalia udongo wenyewe kama una capilarity kubwa au la.

Mwisho ni kwamba angalia aina ya samaki unaotaka kuwafuga growthrate yake ikoje na mwisho ni soko la samaki hao. Ukikamilisha utafiti huo rudi tukupe nondo mkuu.
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Mkuu, tupo wote kwenye ukulima. Nimepata eneo kubwa linaofaa sana kwa ufungaji wa samaki, lipo kijiji cha Mwanzo Mgumu, nipo kwenye matayarisho, nikianza nitakutafuta. Bado nina wasiwasi kama tunao wataalamu wa kilimo cha samaki, kama wapo uzoefu utakuwa ni mdogo kwani hakuna wafugaji wakubwa.
Watalaam wapo kibao,ila wanakaa ofisini tu. Wengine wapo pale Temeke ofisi za kilimo,wengine Kunduchi chuoni pale, wengine wapo pale Kinguluira magereza ( hawa hata mbegu wanayo), wengine wapo SUA morogoro. Mwanzo mgumu si baada ya kupita Chanika kwa mbele kidogo unaingia kushoto unaiacha njia ya kwenda Nzasa? Ni maeneo mazuri sana kwa kilimo. Mimi niko Marogoro/Mfuru mwambao/Msorwa.

Ni vizuri tukiwa na utamaduni wa kutembeleana,unaweza kujifunza zaidi kwa kuona wengine wanafanya nini. Nitakwenda Kinguluira kufuata mbegu ya pelege.
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Mkuu Malila, hongera sana. Napenda sana mindset yako... najitayarisha, nikiwa tayari nitakutafuta.
Hii nchi ni ya ajabu sana,

week jana nilikwenda ktk kituo cha elimu ya ufugaji samaki Kinguruila sio chuo cha samaki pale SUA, kipo kinguruila. Wapo wataalamu wa kutosha vibaya,elimu bure. Nilitumia muda wa saa sita hivi pale kituoni. Nikanunua na mbegu ya kambale Clarius hybrid. Kituo kina aina mbili tu za vifaranga.sato na kambale. Jamaa ni wakarimu hadi raha.

Ila vifaranga vya Kambale ni haba sana kwa sababu vinasakwa na wengi, mimi nilitaka kununua vyote,wakanikatalia, ikabidi niwaachie kidogo. Vinginevyo ufugaji wa samamki uko vizuri,nilikutana na mkulima mmoja toka Maneromango,yy alinunua vifaranga 500 aina ya sato.
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Malila

Asante kwa taarifa, Kinguruila kama sikosei ipo Morogoro lakini sikumbuki ni katika barabara ya Iringa au Dodoma. Santo ni aina ya samaki ambaye anakuwa kwa kasi ya ajabu na wanapatikana kwa wingi sana kwenye mto Kilombero.
Kinguluira iko Morogoro barabara ya Dsm, ukishapita Moro junior Seminary kama unakuja DSM toka Moro,kuna kimji kinafuata, unapomaliza kimji kushoto na kulia yanaanza mashamba ya mkonge. Sasa linapoanza shamba la kushoto kwako kuna njia inaingia kushoto na kuna kibao kimeandikwa kituo cha samaki au uliza wale madogo wa pikipiki,kwamba nataka kwenda FAO, ni buku moja kwa pikipiki.

Niliahidi huko nyuma kuwa nitatoa feedback ya jaribio la ufugaji. Nilianza jaribio may 2010, na sasa ni miezi sita imefika. Niliwaweka sato ktk fishpond isiyo na outlet wala inlet. Wamekuwa na kufikia kiwango cha kuliwa na wamezaliana vizuri sana. Pamoja na kwamba nilipata darasa la kutosha toka Kinguluira,sikubadilisha mazingira ya bwawa lile. Desemba nitakwenda Kinguluira ili nichukue mbegu bora na nifugie ktk mazingira yanayokubalika kitalaam, lakini bwawa lingine nitaendelea kutumia mbegu niliyozalisha pale kwangu ili nione matokeo baada ya miezi sita mingine, hawa ni sato sio Kambale.

Nawatia shime,mwenye nafasi afuge samaki, mbegu zipo nyingi.
 
Slave

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Messages
5,317
Likes
741
Points
280
Slave

Slave

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2010
5,317 741 280
niliwahi kusikia kwamba unatakiwa kupanda samaki wawili kila mita 1kwa 1mean kwa mita 10 unatakiwa upandikize samaki 20 je mpaka unakuja kuvuna ikiwa utafuata ushauri wa kitaalamu unaweza kuvuna samaki wangapi? Na je eneo lenye mchanganyiko wa mfinyanzi na kichanga linafaa?
 
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
10,148
Likes
1,675
Points
280
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
10,148 1,675 280
je? Bwawa la cement halifai.na je hao samaki wakufugwa wanachukua muda gani mpaka kufaa kuvuliwa?
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
je? Bwawa la cement halifai.na je hao samaki wakufugwa wanachukua muda gani mpaka kufaa kuvuliwa?
Samaki wa biashara mara nyingi hufikia market size ktk kipindi cha miezi sita (sato zaidi). Kimsingi unatakiwa kuangalia ukuaji wa samaki wako kila wakati ili wafikie market size, sato wanaweza kufikia size hiyo bila taabu sana ukilinganisha na kambale, nikipata muda wa kambale nitauweka hapa. Kama unafuga kwa matumizi binafsi,size inayopendeza macho yako ndio nzuri.


Bwawa la saruji unaweza kulitumia kwa kufugia samaki pia,lakini sharti uwaone watalaam ili wawe na wewe kuanzia ktk hatua za ujenzi. Kumbuka virutubisho toka ardhini haviwezi kuwafikia samaki kirahisi kupitia kuta za saruji.
 
Mtego wa Noti

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Messages
2,263
Likes
270
Points
180
Mtego wa Noti

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2010
2,263 270 180
Samaki wa biashara mara nyingi hufikia market size ktk kipindi cha miezi sita (sato zaidi). Kimsingi unatakiwa kuangalia ukuaji wa samaki wako kila wakati ili wafikie market size, sato wanaweza kufikia size hiyo bila taabu sana ukilinganisha na kambale, nikipata muda wa kambale nitauweka hapa. Kama unafuga kwa matumizi binafsi,size inayopendeza macho yako ndio nzuri.


Bwawa la saruji unaweza kulitumia kwa kufugia samaki pia,lakini sharti uwaone watalaam ili wawe na wewe kuanzia ktk hatua za ujenzi. Kumbuka virutubisho toka ardhini haviwezi kuwafikia samaki kirahisi kupitia kuta za saruji.
Nilishakuwa na plan ya kufuga samaki ila nikawa nashindwa kufahamu costs involved na hata ivo sikuwa vyema kibajeti ingawa shamba la kuweza kufanyia hiyo buisness lipo. Eneo langu ni shamba la kawaida lakini vilevile lina bonde ambalo maji huwa yanatiririka seasonally hasa masika. huwa nalima mpunga katika bonge hili na wakati wa masika kwa kweli maji huwa yanafurika sana ingawa mvua zinapoisha, kiasi cha maji hupungua na kubakia kama vijisima vidogovidogo.
Swali,..Je naweza kutengeneza fish pond katika eneo la namna hiyo? I mean humohumo bondeni au niweke hiyo fish pond pembeni kidogo ya hilo bonde ingawa slope inakaribia 5%. vilevile eneo hilo hakuna source ingine ya maji zaidi ya hicho kijibonde ambacho ni seasonal ingawa ukichimba unaweza kupata plenty of water kwa chini. Ni feasible kuweza kutumia maji ya ku-pump kutoka ardhini kwa kutumia waterpump?
Naombeni ushauri katika hili,....JF is great.....
 
Mtego wa Noti

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Messages
2,263
Likes
270
Points
180
Mtego wa Noti

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2010
2,263 270 180
Nilishakuwa na plan ya kufuga samaki ila nikawa nashindwa kufahamu costs involved na hata ivo sikuwa vyema kibajeti ingawa shamba la kuweza kufanyia hiyo buisness lipo. Eneo langu ni shamba la kawaida lakini vilevile lina bonde ambalo maji huwa yanatiririka seasonally hasa masika. huwa nalima mpunga katika bonge hili na wakati wa masika kwa kweli maji huwa yanafurika sana ingawa mvua zinapoisha, kiasi cha maji hupungua na kubakia kama vijisima vidogovidogo.

Swali,..Je naweza kutengeneza fish pond katika eneo la namna hiyo? I mean humohumo bondeni au niweke hiyo fish pond pembeni kidogo ya hilo bonde ingawa slope inakaribia 5%. vilevile eneo hilo hakuna source ingine ya maji zaidi ya hicho kijibonde ambacho ni seasonal ingawa ukichimba unaweza kupata plenty of water kwa chini. Ni feasible kuweza kutumia maji ya ku-pump kutoka ardhini kwa kutumia waterpump?
Naombeni ushauri katika hili,....JF is great.....
 

Forum statistics

Threads 1,251,467
Members 481,746
Posts 29,772,987