Pata ufahamu na elimu dhidi ya ugonjwa wa Mafindofindo (Tonsils)

heshima mbele wanajf. naomba kuuliza swali. hiv mtu anapofanyiwa upasuaji "operation" ya tonsills halafu akang'olewa je kuna uwezekano wa ugonjwa kurudi tena? make kuna rafiki yangu alifanyiwa upasuaji mwezi wa nne kufika mwezi wa 7 zikarudi ikabidi akafanyiwe upasuaji tena. . je inawezekana hiyo?

Pole emecka kwa kuchelewa kuja hapa...unajua tena internet mpaka ofisini! Madaktari 'choka-mbaya'!

Tonsils zinapotolewa kwa upasuaji (Tonsilectomy) zinapaswa kutoka/kung'olewa zote pande zote mbili....huwa haibaki hata moja. Na kwa sababu ziko kwenye kama kifuko hivi (sac) ni rahisi basi kuzichomoa nzima nzima isibaki hata kidogo. Na zinapotolewa, basi huwezi tena pata ugonjwa wa kuvimba na kuuma Tonsils yaani 'Tonsilitis'.

Kwa kweli sijui ilitokeaje kwa rafiki yako akaugua tena na kulazimika kufanya operation kwa mara ya pili (sijawahi kuona hilo katika uDaktari wangu). Labda hiyo operation ya kwanza haikuwa Tonsilectomy...sijui...check uwe na uhakika. Na kama ilikuwa tonsilectomy, ina maana Daktari alitoa tonsil moja akaacha nyingine? au alitoa zote but not completely?...Highly unlikely!
 
Habari wakuu naomba kujua hivi tonsis inasababishwa na nini?na mtu anapomeza mate halafu shingoni panauma inakua tatizo ni nini na je ndiyo tonsis yenyewe au vp?naomba msaada kwa anayeelewa
 
inasababishwa na baridi ,au kutumia vitu vya baridi sana,vivywaji,muone doctor,inatibika tu ukipewa antibiotics.
 
Maumivu sehemu ya koo yanaweza yakawa yanasababishwa na uambukizi wa bakteria au virusi lakini mara nyingi zaidi virusi huwa sababu ya maumivu hayo. Tonsillitis ni moja wapo ya uambukizo huo zipo aina zingine.

Mara nyingi maumivu hayo hupotea yenyewe, ila iwapo yanakuwa na homa au maumivu makali kiasi cha kushindwa kula au yamedumu kwa zaidi ya siku tatu, basi ni wakati muafaka kumuona daktari.
 
Mkuu Baba mtata,

Tonsils ni moja wapo ya tissue zinazopatikana mwilini, kwa kawaida huwa zinakuwa nne..yaani katika Kinywa na Koo.Tissue hizi husaidia katika mfumo wa kuukinga mwili(hasa kinywa, koo) na magonjwa.

Tonsilitis, (yaani MAKORORO) hii ndiyo hasa tatizo na mara nyingi imekuwa ikiitwa kama visivyo kama vile "Tonsis, Tonsils, n.k" kumaanisha kuugua kwa Tonsils.

Tatizo la tonsilitis, inaweza kusababishwa kwa vitu mbalimbali zaidi ni vyema kujua umri, na utumiaji wa vyakula/maji , n.k

Si kila "kuumwa kwa koo" humaanisha tatizo la Tonsilitis, hata hivyo pamoja na kuwa na shida katika umezaji wa mate, huambatana na homa, kujisikia vibaya, pia inawezakana kubadilika kwa sauti(kuambatana kwa mafua n.k)

Kwa kufika hospitali,itajulikana hasa ni nini na kupata matibabu sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Baba mtata,mimi kipind niko mdogo huo ndio ulikuwa ugonjwa wangu,uwa unaisha na kurudi tena,lakin mwaka 1996 walienda kunifanyia upasuaji the aga khan hospital wakatoa,yako kama makohozi,lakin ni yanyama nyama,mpaka leo sijaumwa tena,ukitaka usiumwe tena maishan adi wayatoe,wasipoyatoa utakuwa unaumwa ukitumia dawa unapona kwa muda,harafu yanarudi tena,wakiyatoa uumwi tena
 
Habari wanajamvi,
Kijana wangu ana umri wa miaka mitano. Amekuwa akisumbuliwa na tatizo la tonsils kuvimba mara kwa mara. Tatizo hili lilianza kujitokeza akiwa na miezi takribani sita hivi. Wakati linaanza tatizo hili alikuwa akisumbuliwa na homa kali, mafua, kikohozi na pia alikuwa akikoroma sana usiku akiwa amelala (alikuwa anapata taabu sana ya kupumua).

Nimekuwa nikimpeleka kwa wataalamu wa magonjwa ya watoto na baadhi yao wamekuwa wakishauri yaondolewe kwa surgery lakini wengine wameshauri si vema kumfanyia surgery kwani hayajafikia hatua mbaya sana.

Kwa ushauri wa daktari bingwa kabisa wa magonjwa ya watoto amesema dalili za kuwa ugonjwa huo umefikia critical point ni pamoja na kucha kubadilika kuwa za rangi ya kibuluu, dalili ambayo kijana huyu hajafikia. Na pia kwa utaalamu na uzoefu wa bingwa huyo ni kuwa akifikia umri wa miaka 10-14 kuna uwezekano wa tatizo hilo kutoweka lenyewe.

Sasa tatizo hili limekuwa likijirudia mara kwa mara. Na mara zote daktari bingwa amekuwa akimpatia dawa ambazo akitumia tatizo linapungua kwa takribani 80%. Lakini huwa linajirudia katika kipindi cha wiki 2-4 baada ya kumaliza dawa.

Sasa naombeni ushauri wenu:
1. Nini suluhisho la tatizo hili?
2. Je ni kweli akifikisha umri huo uliotajwa tatizo hili linaweza kuisha?
3. Nini prons & cons za kufanya au kutofanya surgery?
4. Je surgery ya ugonjwa huu inachukua muda gani kupona? (Ukitilia maanani kidonda kipo katika njia ya chakula/hewa so kinakuwa katika disturbance ya mara kwa mara).

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Kwanza anatakiwa asitumie kabisa vitu vya baridi ice cream,cold water,na vitu vyote direct from fridges,maji awe anakunywa ya uvuguvugu kila anaposikia kiu,asilale na fan au air conditioner,hata kuishi mazingira yenye A/C kwa muda mrefu above 5 minutes.

Nina mtoto wa dada yangu yalimsumbua sana umri huo,alifuata masharti yakaja kumuachia,hivi sasa ni kijana mkubwa tu and he is ok,mtoto wa dada yangu mwingine naye alisumbuliwa sana akiwa na umri huo bahati nzuri mumewe alipata transfer ya kikazi S. Africa alipofika kule walimfanyia operation na akapona,sasa sijui huku Tanzania kama operation zao zina ubora wa kiasi gani kama itafikia stage ya operation.
 
pole mkuu,

Nilikuwa nasumbuliwa sana na ugonjwa huu hata dawa za antibiotic za kumeza hazikusaidia nikawa napata sindano za mishipa nikaagiziwa dawa za asili ambayo ni pilipili manga na binzari jinsi ya kutumia:
  • kijiko cha chai 1 binzari
  • kijiko cha chai 1 Pilipili manga
  • maziwa fresh 1/2 glass yenye moto
unachanganya unakoroga halafu unakunywa kama chai inaukali/ uchungu kiasi unatakiwa kunywa taratibu
nimekunywa kwa muda wa wiki 2 asubuhi na jioni.

kwa kweli imenisaidia angalau nimefikisha mwaka bila kupata hayo makitu na wakati mwengine nikisikia dalili nakoroga dawa yangu nakunywa.
 
Kwanza anatakiwa asitumie kabisa vitu vya baridi ice cream,cold water,na vitu vyote direct from fridges,maji awe anakunywa ya uvuguvugu kila anaposikia kiu,asilale na fan au air conditioner,hata kuishi mazingira yenye A/C kwa muda mrefu above 5 minutes,nina mtoto wa dada yangu yalimsumbua sana umri huo,alifuata masharti yakaja kumuachia,hivi sasa ni kijana mkubwa tu and he is ok,mtoto wa dada yangu mwingine naye alisumbuliwa sana akiwa na umri huo bahati nzuri mumewe alipata transfer ya kikazi S.Africa alipofika kule walimfanyia operation na akapona,sasa sijui huku Tanzania kama operation zao zina ubora wa kiasi gani kama itafikia stage ya operation.
Asante mkuu,
Kiukweli hayo uliyoyasema najitahidi sana kuyafuata, lakini ndo kama nilivyoeleza hapo juu tatizo linakuwa la kujirudiarudia.

Kuhusu surgery ya ugonjwa huo hapa kwetu hata mimi sina taarifa kama tunao wataalamu waliobobea katika operation za namna hiyo hasa kwa watoto.

Kuna jamaa yangu yeye mwanae alikuwa na nyama za puani. Zilikuwa zinamsumbua sana. Alipofikia miaka 2 madaktari wakamshauri ziondolewe kwa surgery. Bahati mbaya yule mtoto alikuja kupoteza maisha wakati wa operation. Ni risky sana operation za magonjwa haya. Ndo maana naomba wataalam wanipe ushauri hapa.
 
pole mkuu......nilikuwa nasumbuliwa sana na ugonjwa huu hata dawa za antibiotic za kumeza hazikusaidia nikawa napata sindano za mishipa nikaagiziwa dawa za asili ambayo ni pilipili manga na binzari jinsi ya kutumia
kijiko cha chai 1 binzari
kijiko cha chai 1 Pilipili manga
maziwa fresh 1/2 glass yenye moto
unachanganya unakoroga halafu unakunywa kama chai
inaukali /uchungu kiasi unatakiwa kunywa taratibu
nimekunywa kwa muda wa wiki 2 asubuhi na jionu
kwa kweli imenisaidia angalau nimefikisha mwaka bila kupata hayo makitu
na wakati mwengine nikisikia dalili nakoroga dawa yangu nakunywa
Thanks kwa ushauri BW. Nitaujaribu. Kuna watu wanasema huu ugonjwa unaweza kutoweka kabisa.
 
Thanks kwa ushauri BW. Nitaujaribu. Kuna watu wanasema huu ugonjwa unaweza kutoweka kabisa.

hata mie nilitakiwa kufanyiwa upasuaji KCMC lakini niliogopa nikaona bora kuendelea kuumwa
rafiki yangu tulisoma naye alifanyiwa upasuaji lakini baada ya muda yakarudia tena ikawa mbaya zaidi
sijui ilikuwaje kitaalam
ni kujaribu anaweza ikasaidia kama nilivyojaribu
 
Huyo mtoto mpige marufuku kushare vitu mdomoni kama vikombe,vijiko n.k.Kuna baadhi ya akina mama wanajidai wanawapenda watoto unakuta wakati wa kula wanatumia kijiko kimoja,mama akiwa na bacteria wsiomwathiri yeye wakiingia kwa mtoto wanamwathiri.Pia watoto wanaiba maji ya baridi na kunywa kwa siri,pia upate tiba mwafaka ya kumponyesha,kama tiba ni hafifu ujue zitajirudia rudia na pia baadae anaweza kusumbuliwa na moyo hapo baadae
 
Habari wanajamvi,
Kijana wangu ana umri wa miaka mitano. Amekuwa akisumbuliwa na tatizo la tonsils kuvimba mara kwa mara. Tatizo hili lilianza kujitokeza akiwa na miezi takribani sita hivi. Wakati linaanza tatizo hili alikuwa akisumbuliwa na homa kali, mafua, kikohozi na pia alikuwa akikoroma sana usiku akiwa amelala (alikuwa anapata taabu sana ya kupumua).

Nimekuwa nikimpeleka kwa wataalamu wa magonjwa ya watoto na baadhi yao wamekuwa wakishauri yaondolewe kwa surgery lakini wengine wameshauri si vema kumfanyia surgery kwani hayajafikia hatua mbaya sana.

Kwa ushauri wa daktari bingwa kabisa wa magonjwa ya watoto amesema dalili za kuwa ugonjwa huo umefikia critical point ni pamoja na kucha kubadilika kuwa za rangi ya kibuluu, dalili ambayo kijana huyu hajafikia. Na pia kwa utaalamu na uzoefu wa bingwa huyo ni kuwa akifikia umri wa miaka 10-14 kuna uwezekano wa tatizo hilo kutoweka lenyewe.

Sasa tatizo hili limekuwa likijirudia mara kwa mara. Na mara zote daktari bingwa amekuwa akimpatia dawa ambazo akitumia tatizo linapungua kwa takribani 80%. Lakini huwa linajirudia katika kipindi cha wiki 2-4 baada ya kumaliza dawa.

Sasa naombeni ushauri wenu:
1. Nini suluhisho la tatizo hili?
2. Je ni kweli akifikisha umri huo uliotajwa tatizo hili linaweza kuisha?
3. Nini prons & cons za kufanya au kutofanya surgery?
4. Je surgery ya ugonjwa huu inachukua muda gani kupona? (Ukitilia maanani kidonda kipo katika njia ya chakula/hewa so kinakuwa katika disturbance ya mara kwa mara).

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

POle sana Mkuu kwa tatizo la mtoto. Huu ugonjwa unasumbua sana,mimi nilikuwa muathirika wa tatizo hili nilipokuwa mtoto.Ila lilkuja kuisha lenyewe nilipofikisha 16 yrs, maana nilitakiwa mpk kufanyiwa operation.Ninachoshauri, mfuate masharti kama ya kutotumia vitu vya baridi,na nina imani litakuja kuisha lenyewe.Mimi nilisumbuliwa toka nina 4 yrs mpk 16 yrs,nilikuwa siumwi ugonjwa mwingine zaidi ya huo,na tiba yangu ilikuwa ni sindano
 
Nashukuru mkuu kwa ushauri wako. Nitaufuata. Nina imani Mungu atamsaidia atapona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom