Pata ufahamu na elimu dhidi ya ugonjwa wa Mafindofindo (Tonsils)

Ukiona kwa siku mbili ushauri wa Dr Lizzy haujakufaa uende hospital mapema ukachukue antibiotic. Mafindofindo ni ugonjwa hatari sana, usiuchukulie kiwepesi hasa kama yanakupata mara kwa mara.
 
Kunywa Pen-V 2*3 kwa siku for five days. Ila ukianza tu kumeza let's say asubuhi na mchana unaweza ukajidanganya umepona jioni usiendelee kwa jinsi utakavyopata nafuu ghafla. Pole.
 
Tonsil husababishwa na sababu nyingi tu . Pia husababishwa na upungufu wa white blood cells katika mwili ambazo cells hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kazi lymph zinavimba na husababisha Tonsils.

Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata tonsils kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata tonsils, mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.

Wakati unapokuwa na tonsils muhimu zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote vikali, zaidi utumie maji ya moto

Dawa za tonsils ni : kama ni mtumiaji wa dawa za chemicals basi epincilin inasaidia sana kuondosha tonsils.

Dawa nyengine
ambayo mimi binafsi naipendelea hii zaidi kwani inafanya kazi mara moja : Kamua ndimu moja katika glass yako kisha tia maji ya Uvuguvugu (warm water) na baadae tia vijiko vinne vidogo vya asali na kijiko robo cha chumvi kuroga uzuri na unywe pole pole

Au Dawa hii Jaribu pia Dawa ya TONSILS ni kusukutuwa maji yaliokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala Tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto.

Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia.

Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako.

Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya kazi na mdomo uko wazi basi pia unaweza kuumwa na Tonsils.

Vile vile kutoka nje kwenye joto kisha ukaingia pahala baridi huwa inasababisha Tonsils na maradhi mengine kama flu na kuumwa na kichwa..n.k

Tumia kisha unipe FeedBack. P.h.D. MziziMkavu
 
wakuu huu ugonjwa wa TONSES unasababishwa na nini? Na nini tiba yake,kuna dada yangu anaumwa sana hii kitu akitumia dawa inaisha but ndani ya kama wiki tatu hivi inarudi tena! Msaada please!!!!
 
Ni uvimbe katika Tonsils za kwenye koo na husababishwa na virus au bacteria. Unatibika kwa dawa kutegemeana na aina ya mdudu hasa wale bacteria. Moja ya bacteria maarufu wanaitwa streptococcal.

Inapotokea ugonjwa kujirudia basi mgonjwa hufanyiwa operesheni ndogo inaitwa tonsillectomy, yaani wanaondoa tonsil. Hii inazuia kujirudia rudia ambako kunaweza kuleta complications. Wadudu kama strept wanaweza kusababaisha kitu kinaitwa peritosillar absess(Quinsy) na kuweza kusababisha mambo kama infection katika damu (septicaemia), au sehemu nyingine kama figo na moyo.

Ingawa complication hutokea nadra lakini huwezi jua hiyo nadra itatokea wapi. Ikimtokea mtu wako sio nadra ni madhara kamili.
Ningekushauri uwaone wataalam(ENT) ukiwaeleza kujirudia rudia kwa hali hiyo na kama zipo kumbu kumbu wapelekea ili wabaini ukubwa wa tatizo.
 
Asante mkuu! kwahiyo inamaana hayasababishwi na kunya au kula viu vya baridi!
Dhana hii ya vitu baridi imeenea sana, hakuna mahali kwenye medical iterature imeelezwa. Haina ukweli.

Ni Bacteria au virus. Kama ni virus huwa 'self limiting' kwasababu hakuna dawa ya kutibu virus.
Mara nyingi huwa ni bacteria ambao wanatibika kwa dawa za kawaida kabisa. Tatizo ni pale kunapokuwa na usugu na kujirudia rudia.

Kinachotokea hapo ni kuwa hao bacteria wanaweza kupata access kwa kwenda sehemu nyingine na huko wakasababisha madhara makubwa zaidi. Hiyo ndiyo inaitwa complication.

Kwa medical terminology, complication ni matokeo ya tatizo fulani. Kwa mfano bacteria wakitoka kwenye tonsils na kuingia katika damu halafu kutua katika figo na kusababisha 'Glomerulonephritis', basi maradhi ya figo ni complication ya untreated tonsilitis.
 
Antibiotics might help. Ni vizuri akaonana na daktari.

Alafu inashauriwa kunywa vitu vya baridi sana (tofauti na tulivyokua tunaambiwa zamani) au vya moto sana.
 
Antibiotics might help. . .
Ni vizuri akaonana na daktari.

Alafu inashauriwa kunywa vitu vya baridi sana (tofauti na tulivyokua tunaambiwa zamani) au vya moto sana.
Asante lizzy,!
 
nawashukuru sana wachangiaji hapo juu. ukienda kwenye hospital zetu unagombezwa kwa nguvu
zote kwa nini unatumia vitu vya baridi tena unaambiwa uache kabisa.

Mie huwa vitu vya baridi situmi kabisa lakini ndio kila mara sindano na antibiotics
kama hii mada ilikuwa inanihusu vile.

leo ndio ninaonana na Dr wa ENT niweze pata ufafanuzi na tiba halisi
 
nawashukuru sana wachangiaji hapo juu
ukienda kwenye hospital zetu unagombezwa kwa nguvu
zote kwa nini unatumia vitu vya baridi tena unaambiwa uache kabisa
mie huwa vitu vya baridi situmi kabisa lakini ndio kila
mara sindano na antibiotics
kama hii mada ilikuwa inanihusu vile
leo ndio ninaonana na Dr wa ENT niweze pata ufafanuzi na tiba halisi
Uje na feedback mkuu! Tutashukuru sana...
 
wakuu huu ugonjwa wa TONSES unasababishwa na nini? Na nini tiba yake,kuna dada yangu anaumwa sana hii kitu akitumia dawa inaisha but ndani ya kama wiki tatu hivi inarudi tena! Msaada please!!!!

Tonsillitis: An infection of the oral pharynx and tonsils by streptococcus.

Tonsillitis is an inflammation of the tonsils most commonly caused by viral or bacterial infection. Symptoms of tonsillitis include sore throat and fever. While no treatment has been found to shorten the duration of viral tonsillitis, bacterial causes are treatable with antibiotics. It usually takes around three weeks to recover.
 
Uje na feedback mkuu! Tutashukuru sana...

mkuu sikuweza kupata tiba ameshauri ili kuweza kupata vipimo/tiba kamili unatakiwa kwenda zikiwa zimevimba
nitatoa mrejesho nyuma nitakapofanikiwa kwa hili
 
Tiba ya vidonda vya koo

chukua Vitunguu maji kiasi kumi au vinane, uviponde halafu Uchanganye na maji kiasi kikombe cha chai kimoja Ukoroge viziru Uvichuje halafu Unywe vijiko vitatu kila siku asubuhi, mchana na jioni vijiko vitatu.

Au tumia Dawa hizi zitakusaidia
Jinsi ya kutibu vidonda vya kooni:
  • Sukutua maji ya chumvi yaliyo vuguvugu
  • Mumunya dawa za koo, usiwape watoto inaweza kumnyonga akimeza kwa bahati mbaya.
  • Muulize mfamasia wako akuuzie kipulizo (spray) cha kutuliza uchungu kooni.
  • Ikiwa koo linawasha au limekauka, pumua mvuke wa maji moto itakusaidia.
Please Give me your feedback.
 
Jamani sasa naona mnataka kuchanganya watu,mimi zilikuwa zinanisumbua sana zamani na sikujua nini kinasababisha,nikashauriwa na doctor mmoja niache kutumia vitu vya baridi,nilipoacha nazo zikaniachia na mara mojamoja nikijisahau nikatumia kitu cha baridi kali lazima kesho yake zinanikamata,sasa hayo maneno ya kuwa vitu vya baridi havina madhara mimi naona kwa upande wangu sikubaliani nayo,labda mtupe ufafanuzi wa kina.
 
Heshima mbele wana JF.

Naomba kuuliza swali:

Hivi mtu anapofanyiwa upasuaji "operation" ya tonsils halafu akang'olewa je kuna uwezekano wa ugonjwa kurudi tena? make kuna rafiki yangu alifanyiwa upasuaji mwezi wa nne kufika mwezi wa 7 zikarudi ikabidi akafanyiwe upasuaji tena.

Je, inawezekana hiyo?
Pole emecka kwa kuchelewa kuja hapa...unajua tena internet mpaka ofisini! Madaktari 'choka-mbaya'!

Tonsils zinapotolewa kwa upasuaji (Tonsilectomy) zinapaswa kutoka/kung'olewa zote pande zote mbili....huwa haibaki hata moja. Na kwa sababu ziko kwenye kama kifuko hivi (sac) ni rahisi basi kuzichomoa nzima nzima isibaki hata kidogo. Na zinapotolewa, basi huwezi tena pata ugonjwa wa kuvimba na kuuma Tonsils yaani 'Tonsilitis'.

Kwa kweli sijui ilitokeaje kwa rafiki yako akaugua tena na kulazimika kufanya operation kwa mara ya pili (sijawahi kuona hilo katika uDaktari wangu). Labda hiyo operation ya kwanza haikuwa Tonsilectomy...sijui...check uwe na uhakika. Na kama ilikuwa tonsilectomy, ina maana Daktari alitoa tonsil moja akaacha nyingine? au alitoa zote but not completely?...Highly unlikely!
 
Back
Top Bottom