Pata ufahamu na elimu dhidi ya ugonjwa wa Mafindofindo (Tonsils)

Habari zenu ndugu zangu...samahani naomba msaada kwa yeyote mwenye kujua dawa ya koo maana leo siku ya tatu mate nameza kwa shida...linakerekata balaa nameza Pen V ndo ata dalili

Kiongozi, nenda hospitali. Jamvini watu huja kuomba msaada baada ya hospitali kufeli.
 
Kiongozi,hospitali nilienda toka juzi maana ziliniletea homa kali sana ikabd Dr. alimpumzishe Wardn...nkachomwa sindano na drip juu baada ya hapo nkaambiwa ninunue hizo Pen V lkn naona hali bado japp joto limepungua

Pole sana. Mimi sio Dr. ila kama ulikuwa na homa na una maumivu makali kwenye koo inawezekana una pharyngotonsillitis. Lakini ni muhimu kujua kama chronic au recurrent (huwa unaumwa mara kwa mara).

Dawa uliyoambiwa kunywa ya Pen V ni sahihi, inatakiwa unywe kila baada ya masaa nane kwa siku kumi, na inatakiwa iwe ya gram 500 au mbili za gram 250. Lakini pia Amoxillin au Erthromycin ingefaa pia.

Kawaida ukimeza antibiotic kwa siku tatu ukaona hupati nafuu, unashauriwa urudi hospitali ili Dr. akubadilishie dawa.
 
Kuna dawa ya kienyeji inatibu kabisa hiyo takataka na Kamwe hutaumwa tena tonsils, rudi hospital wakishindwa kabisa nitafute.
 
Habari zenu ndugu zangu...samahani naomba msaada kwa yeyote mwenye kujua dawa ya koo maana leo siku ya tatu mate nameza kwa shida...linakerekata balaa nameza Pen V ndo ata dalili
Dawa yake mkuu ni mswaki piga kwenye koo mpaka damu itoke
 
Sukutua maji ya uvuguvugu yenye chumvi ilikolea vibaya, 1x3,baada ya siku mbili lete mrejesho.
Kama ulivyo shauriwa na wana Jf nami nasema rudi Tena Hosp umweleze doctor kua tatizo bado linaendelea. Yeye sasa ataangalia katika kumbukumbu zake za dawa alizokuandikia ili akubadirishie
 
Usidanganywe we rudi Hosp achana na mawazo tata kama umemeza Penv hujapona hizo unazoshauriwa ndo utapona? Ngoja nikuambie ndugu dawa huwa zina ukoo kama ulivyo wewe kwa hiyo.

Hiyo Ampiclox ni familia ile ile ya alikotoka huyo pen v. Na shule yao moja na mwalimu wao ni mmoja kwa hiyo Nayo haitokusaidia nenda akakubadirishie dawa doctor wako akupe familia nyingine
 
Pole sana mkuu mtoa mada....

Nakupa dawa, dawa ambayo mimi hutumia pia, na kuna mdau kadokeza hapo juu....

Mm nilitumia hii dawa kama mara 3 na sikumbuki kuumwa tena huo ugonjwa!

Binafsi nilikua nikiona dalili usiku, najua kabisa kesho kukikucha vidonda vinafumuka...

So nachemsha maji ya moto kiasi na weka chumvi ya kutosha hasa, mpaka radha ya maji inakua ya uchungu, baadaye unaacha yapokee kidogo, angalau kama umoto wa chai, then nasukutua yale maji nahakikisha yanapita kila sehemu mdomoni, natema....nasukutua maji mengine kama trip 3 then nalala.......kesho ni mzima.

Trip moja nilichelewa mpaka vidonda vikatoka, niliacha yapoe sana then nilisukutua hivyo hivyo kwenye vidonda kwa siku 2 then siku ya 3 niko fresh....

Mkuu tumia hii dawa, mimi ndo dawa natumia, (ulithi wa bibi).
Utakuja kuleta mrejesho hapa!
 
Back
Top Bottom