Pata kuyafahamu yaliyo jiri ndani ya riwaya ya nafasi ya wakati

NOTA

New Member
Dec 18, 2014
2
0
SEHEMU YA KWANZA
Masimulizi ni zaidi ya tafakari.Sikushangazwa kwani hata michirizi ni zaidi ya mistari iliyonyooshwa kwa rula na mjuvi wa taaluma ya uchoraji kwani hutumia ustadi wa hali ya juu kutaka kukonga nyoyo na kuvuta umakini wa anaowatumikia katika kazi yake. Huwezi amini siku ile kukutana na hali ambayo ilikuwa si rahisi kutofautisha kichochoro na barabara kwani kila pahala palikuwa hapatoshi. Hapakuchaguliwa maneno ya kunenwa wala namna ya kusimama ili kuweza kufikisha ujumbe kwa mkubwa wala kwa mdogo, kwani kila mmoja alionekana mwenye kuchachamaa baada ya Mfalme wa ugaibuni sayari ya sita kutengeneza sifa mbaya za Mfalme Misechela wa tatu kwa lengo la kutaka kumng’oa kwenye kiti chake. Hali ile ilitokana na kuona mfalme Misechela wa tatu anapata sifa kubwa ya kuwakinga Wanawingu la Buluu na mvua mbalimbali zenye kubebwa na pepo haribifu na zenye machukizo kupitia miamvuli inayotengenezwa na Mfalme wa ugaibuni sayari ya sita ambaye alikuwa hanufaiki kiuchumi na Mfalme Misechela wa tatu. Katika kuhakikisha anamngoa Mfalme Misechela wa tatu katika kiti chake Mfalme wa ugaibuni sayari ya sita aliwaagiza wataalamu wamuandalie sumu mbalimbali zitazo ambatanishwa kwenye mvua ya mawe watakayo itengeneza, ambayo itakwenda kuchana chana mwamvuli ule unaompatia sifa njema Mfalme Misechela wa tatu katika ardhi ya Wingu la Buluu na kuwafanya Wanawingu la Buluu waishi maisha waliyo ya furahia kwa miaka tangu walipo jitoa kwenye mikono ya Mfalme wa ugaibuni sayari ya sita kwa kutawaliwa kinyama na kudhalilishwa na kuachwa masikini wa kutupwa. Mfalme wa ugaibuni sayari ya sita kauli yake ni moja “siwezi kumuacha adui yangu anayepinga maendeleo yangu, kwa kumnyonya kupitia ukoloni mamboleo anufaike kupitia sifa ya mwamvuli wangu unao walinda watuwake na kila aina ya dhiki iletwayo na mvua kisha yeye ajenge jina lake”. Mkubwa hakumheshimu mdogo wala mdogo hakumheshimu mkubwa ni tafrani tupu ilikuwa, kila kona ni minong’ono na makelele ilitosha kuita ni siku ya pepo za sintofahamu ndani ya ardhi ile iliyozoeleka kujawa na utulivu, amani na mshikamano licha ya kuwa wana dhiki nyingi kila kona. Kilicho saidia siku ile hali ile kutodumu kwa siku nyingi ilikuwa ni mfumo wa undugu waliochaguliwa kuishi kwa miaka mingi sana iliyopita. Mfumo wakindugu ulipelekea kila mmoja ajione kama ni mmiliki wa hisa za ardhi ile. Hivyo kila mmoja alijisikia huru kuwa askari, mwanajeshi hata jasusi ilimradi mali yake na hisa zake zisipotelee hewani. Utulivu ule na amani vilivyotanda ndani mithili ya wingu zuri katika anga la ardhi ya kijiji kile cha wingu la Buluu. Kila kona wingu lile lilianza kuingiliwa na tabaka dogo la wingu jeusi lenye uwezo wa kubadilisha sifa ya kijiji cha wingu la Buluu kuachana njiapanda na matarajio ya walio wengi ndani ya kijiji cha Wingu la Buluu. Lengo lake lilikuwa kutaka kudondosha mvua ya mawe ilimradi tu wampatie majeraha mfalme Misechela ambaye alikuwa hajafungamana na jamii ile ya sayari ya sita huko ugaibuni walio tengeneza wingu lile jeusi lenye tindikali yenye uwezo wa kuunguza kila mali na amani iliyomea katika ardhi ya wingu la Buluu, cha ajabu haikuwa miezi ya mvua wala si karibu na miezi ya mvua kilikuwa ni kipupwe na Wingu la Buluu bado lingali shwari katika kila pembe yake .Shwari hiyo ikisawiri maisha ya kila mmoja. Siyo kama wingu lile kwamba lilipotea njia bali lilidhamiria kwenda kutibua kila aina ya amani iliyopatikana ndani ya ardhi ili kongwe iliyojulikana kwa jina la ardhi changa kutokana na uduni wake kiuchumi baada ya kunyonywa na kuzolewa na wenye kujijali wa sayari ya sita huko ugaibuni na kuchukua kila kilicho kuwa kizuri ambacho kingeweza kuwatoa kwenye jina hilo la dharau la ardhi changa licha ya ukongwe wake. Wachambuzi wa kisiasa walivyolichunguza wingu lile waliona ni wingu hatari kwani mvua inayokuja nayo ni mvua ya kemikali ya tindikali iliyosababishwa na binadamu, lakini hawakubaini roho ya hasidi gani imebeba ile kemikali zizalishwayo na husuda inayoweza kuharibu kila utaratibu wa ardhi ya kijiji kile cha Wingu la Buluu. Kwani makazi, vyanzo vya ajira,huduma za jamii, mazao na bei zake vitaelekea kutaka kuharibiwa, kila aina ya vyanzo vya taaluma pia vitaliwa kama mchwa washambuliavyo mbao za sofa kwa uvungu na hapatakuwa na mzalishaji mali wala uzalishaji mali. Vita vitatokea katika kuung’oa utawala ule uliowafanya Wanawingu la Buluu wajivunie maisha bora na ya amani, kwani watoto, wanawake, wazee na hata vijana wakiume watateseka sana na hata kufa kwani hatopatikana mshindi kwa miaka mingi. Wataalamu wa hali ya hewa na wanaharakati walitoa taarifa kwa wanajamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama radio, magazeti, runinga na mitandao ya kijamii inayoshabihiana na simu za mikononi wakitoa tahadhari juu ya athari zitakazotokana na anguko la wingu lile dogo jeusi.Vyombo vyote vya habari vilisisitiza kuwa wingu litaleta mapinduzi ya utawala na kupelekea kupata utawala mpya usio na tija kwao ambao utaleta uongozi wenye kupelekea kuathiri mandeleo kutokana na kuendesha kijiji cha Wingu la Buluu kwa matakwa ya Mfalme wa ugaibuni sayari ya sita,kwani fedha itashuka thamani,anguko la uchumi litatokea,kilimo kitakuwa cha hasara kwani maneno yatakuwa mengi kuliko matendo kupelekea hata maslahi ya mkulima kupotea,viwanda vya ndani vitakufa kwa uendeshaji dhaifu utakaotokea, na sera mbovu zitatungwa zenye kuambatana na kukaribisha viwanda vya nje kutawala soko la ndani la viwanda, utegemezi utaongezeka utakaopelekea kukosa maamuzi binafsi ya kimaendeleo, hivyo ajira binafsi na serikalini itakuwa ni jazanda. Walisisitiza sana umakini kwani waliweka angalizo vya kutosha kama ngoma juani, walisema hivyo maisha yatakuwa si yale tena tuliyoyazoea ndani ya Wingu la Buluu au kama ya jirani zetu kwa Chifu Mwanga wenye kuendesha kila yao kwa kumlenga mwanasayari ya saba wa kawaida kwa kunufaishana wote wa mijini na mashambani ndani ya kijiji na kupiga vita matabaka ya kila namna yenye kumfanya mmoja aonekane bora zaidikuliko wengine na kuheshimu misingi ya asili na chimbuko la kila mmoja. Licha ya watu wa Chifu Mwanga kuwa na tabia ya ukavu kwa mambo ya kipumbavu kama tabia unaa ambayo mara nyingi hawaipi nafasi hata kidogo kwa kuipiga vita , kwao haikuwa rahisi kuangamiza wingu jeusi la Mfalme wa ugaibuni sayari ya sita alipojivika unyambi kwa kutaka kudondosha wingu lake jeusi lenye kemikali ya tindikali ya kuonndoa amani na roho ya utu kwa kuwapandikizia chuki wanasayari ya saba wa Chifu Mwanga alipojaribu kutaka kupandikiza chuki ya kung’olewa kwake, walifanikiwa kutokana na kuwa na uzalendo na ardhi yao iliyowakuza na kupuuzia mbali mitego na fitina za Mfalme wa ugaibuni sayari
 
Back
Top Bottom