Pata kitu hapo, kupumzika katika kitanda chako cha nyumbani

Princess21

JF-Expert Member
Oct 15, 2015
272
266
Naamini baada ya ya siku ndefu kutafuta riziki, na baada ya siku ndefu kuongea na watu tofauti, kukasirishwa na watu tofauti na wakati mwengine inafika mda mwili wako unakuwa umechoka unachohitaji na kupumzika katika kitanda chako cha nyumbani.

Wengi nimesikia wakisema huwawia vigumu kupumzika vizuri kitanda kingine tofauti na alichonacho nyumbani sababu ni kwamba labda godoro la nyumbani ni zuri kuliko sehemu nyengine ama tu ukilala nyumbani unapumzika vizuri zaidi ukiwa pembeni ya mtu aliyekaribu na moyo wako.

Ndio swala la chumbani linapoingia, sehemu ya kulala hupaswa kukufanya uchovu uliokuwa nao wote kutoweka, chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi vya kufanya hata hewa isiingie, sijui viatu, kapu la nguo chafu, ma vengine vingi.

Hupendeza chumba chako cha kulala kiwe na kitanda tu peke yake, lakini kwa watu ambao nyumba zao ni ndogo basi kabati ndani ya chumba sio vibaya lakini muda wote liwe limefungwa, na hata kama umeweka viatu kwenye chumba chako basi hakikisha kabla hujavipeleka chumbani viatu vyako unaviweka kwanza sehemu ya hewa nje ili uvundo na jasho viweze kutoka ndio uvipeleke chumbani, na wenye makapu ya nguo chafu chumbani akikisha makapu hayo yanamifuniko kuzuia harufu mbaya ya nguo zilizovaliwa siku za nyuma kabla ya kufuliwa.

Chumbani mambo mengi sana hufanyika ukiacha kulala, hata kupumzika tu na mwenzi wako mkiongelea mambo fulani ya maisha yenu kwahiyo hutaki kufanya hivyo na harufu mbaya ikiwapitia pembeni.
 
naamini baadaya ya siku ndefu kutafuta riziki, na baada ya siku ndefu kuongea na watu tofauti, kukasirishwa na watu tofauti na wakati mwengine inafika mda mwili wako unakuwa umechoka unachohitaji na kupumzika katika kitanda chako cha nyumbani.. wengi nimesikia wakisema huwawia vigumu kupumzika vizuri kitanda kingine tofauti na alichonacho nyumbani.. sababu ni kwamba labda godoro la nyumbani ni zuri kuliko sehemu nyengine ama tu ukilala nyumbani unapumzika vizuri zaidi ukiwa pembeni ya mtu aliyekaribu na moyo wako..

ndio swala la chumbani linapoingia, sehemu ya kulala hupaswa kukufanya uchovu uliokuwa nao wote kutoweka, chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi vya kufanya hata hewa isiingie, sijui viatu, kapu la nguo chafu, ma vengine vingi.

hupendeza chumba chako cha kulala kiwe na kitanda tu peke yake, lakini kwa watu ambao nyumba zao ni ndogo basi kabati ndani ya chumba sio vibaya lakini muda eote liwe limefungwa, na hata kama umeweka viatu kwenye chumba chako basi hakikisha kabla hujavipeleka chumbani viatu vyako unaviweka kwanza sehemu ya hewa nje ili uvundo na jasho viweze kutoka ndio uvipeleke chumbani, na wenye makapu ya nguo chafu chumbani akikisha makapu hayo yanamifuniko kuzuia harufu mbaya ya nguo zilizovaliwa siku za nyuma kabla ya kufuliwa.

chumbani mambo mengi sana hufanyika ukiacha kulala, hata kupumzika tu na mwenzi wako mkiongelea mambo fulani ya maisha yenu. kwahiyo hutaki kufanya hivyo na harufu mbaya ikiwapitia pembeni.
Hebu tupia kapicha ka chumba chako cha kulala ili tuendelee,isije kuwa unalala stendi ya basi halafu unataka kutuzingua sisi wanakijiji tunaolala kwenye nyumba za msonge na majani.
 
mhmhmhmh vyumba vya kibongo navyovijua mimi wengi wao kila kitu ni humo humo ukitaka kupanda tu kitandani lazima upande meza ndio ufike kitandani
Cha kwako kiko vipi Cessy? au ndio ile dizaini ya kila kitu humo humo yaani unapikia humo humo na jiko la mchina, unaanika underwears humo humo,na ndoo ya plastic ya amboni ndio toilet humohumo kwa kuogopa kukabwa au kubakwa uani usiku,hebu dadavua basi mamishuu.
 
Cha kwako kiko vipi Cessy? au ndio ile dizaini ya kila kitu humo humo yaani unapikia humo humo na jiko la mchina, unaanika underwears humo humo,na ndoo ya plastic ya amboni ndio toilet humohumo kwa kuogopa kukabwa au kubakwa uani usiku,hebu dadavua basi mamishuu.
Natamani ukione acha tu utafurahi na roho yako unaweza ukasahau shida zako zote
 
Natamani ukione acha tu utafurahi na roho yako unaweza ukasahau shida zako zote
Duuh sasa tunapanga vipi ili nije nikione? maana mimi nilikuwa na binti mmoja mtaamu sana ila chumba chake ndio kilikuwa kama nilivyoeleza.
 
Hapa Mwanza kuna wataalamu ukitaka aje akudisainie chumba chako cha kulala na kukiweka sawa, ila bei zao ziko juu kidogo kama 25,000,000/= za kitanzania ila chumba kina safiii na chenye mvuto na ladhwa haswaaaaaaaaaaaa
 
Vyumba vingi, hasa vya sisi wakazi wa darisalama vinasikitisha. All in one.
 
Back
Top Bottom