Pata habari: Kumbe mtu anayesumbuliwa na sukari anaweza akasahau tatizo lake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pata habari: Kumbe mtu anayesumbuliwa na sukari anaweza akasahau tatizo lake.

Discussion in 'JF Doctor' started by health, Oct 5, 2012.

 1. health

  health JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  KISUKARI NI NINI
  Kisukari ni ugonjwa utokanao na ongezeko la chembechembe za sukari (glucose) katika damu. Ongezeko hili husababishwa na;
  - Mwili kushindwa kutengeneza homoni ya insulin
  - Kutengeneza insulin isiyo bora
  - Kushindwa kuitumia insulin inayotengenezwa mwilini (insulin resistance)
  Aina za Kisukari
  Ziko aina kuu tatu
  1. Aina ya kwanza (type 1)
  2. Aina ya pili (type 2)
  3. Kisukari wakati wa ujauzito (Gestational Diabetes Mellitus)
  Aina ya kwanza (Type 1)
  •Hii ni aina ya kisukari kinachotokea tangu utotoni
  •Mtoto hushindwa kutengeneza homoni ya insulin kwa sababu mwili hushambulia kimakosa seli zinazotengeneza insulin katika ogani ya kongosho (pancreas)
  •Ugonjwa huu hutokea kutokana na urithi wa kijenetikali
  •Tiba yake ni mgonjwa kuendelea kutumia matibabu ya insulin maisha yake yote.

  Aina ya pili (Type Two)
  •Hii hutokea mara nyingi ukubwani kwa sababu ya
  - Mwili kushindwa kutengeneza insulin sahihi
  - Mwili kushindwa kutumia insulin iliyotengenezwa tayari (insulin resistance)- hii hutokana mara nyingi na unene kupita kiasi.
  - Vilevile ugonjwa huu una tabia ya kurithiwa.
  Aina hii ya kisukari ndio hatari zaidi kwani
  - inachangia zaidi ya 70-80% ya wagonjwa wote
  - inazidi kuongezeka kwa sababu watu hawapo makini na lishe na aina ya maisha wanayoishi (kutofanya mazoezi) inapelekea watu wengi kuwa na unene uliopindukia (obesity) na hivyo kusababisha mwili kushindwa kutumia insulin yake (insulin resistance) na hivyo kupata kisukari.
  * Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia aina ya pili ya kisukari imeathiri watoto wengi kuliko aina ya kwanza.
  Dalili za Kisukari
  •Kuna dalili nyingi za kisukari, muhimu ni pamoja na
  1. Kunywa maji mengi mara kwa mara
  2. Kula chakula kingi kupindukia
  3. Kukojoa mara kwa mara
  4. Kupata ganzi katika mikono na miguu
  5. Mwili kuchoka haraka
  Madhara ya ugonjwa wa Kisukari
  •Yapo madhara ya muda mfupi na ya muda mrefu
  •Ya muda mfupi ni pamoja na kupoteza fahamu na hata kufa (ketoacidosis), kupungukiwa na electrolytes
  •Ya muda mrefu ni pamoja na athari katika moyo, mfumo wa fahamu, macho na figo.
  •Kupungukiwa nguvu za kiume ni tatizo la msingi katika jamii.

  Matibabu ya ugonjwa wa kisukari
  •Matibabu ya ugonjwa huu yapo katika njia mbili kuu
  - matibabu kwa matumizi ya dawa za hospitali
  - matibabu kwa kuboresha aina ya maisha yaani mazoezi, kupunguza uzito na kutumia lishe bora
  Kuboresha aina ya maisha
  •Mbinu hii ina umuhimu mkubwa katika matibabu ya kisukari kama ilivyo kwa dawa za hospitali hivyo ni vyema mgonjwa akafanya vyote…..
  - mgonjwa azingatie dawa zake za hospitali
  - mgonjwa afanye mazoezi walau kwa dk 30 kwa siku
  - mgonjwa azingatie lishe bora hasa kwa kutumia bidhaa za nyongeza ya lishe (supplements)
  FOOD SUPPLIMENTS NDIZO ZINAZOWEZA KUSAIDIA KUONDOKANA NA HILO TATIZO SABABU HURUDISHA SELI HAI ZOTE ZILIZOKUFA NA KUFANYA SUKARI KUBAKI NORMAL.
  Kwa msaada huo tuwasiliane kwa email: ishealthy@hotmail.com
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  haya mkuu asante kwa somo nimekupata
   
 3. M

  Mjasiriamali1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,318
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Si useme tuu foreverliving mbona unazunguka sana? Wafanyabiashara kuwa doctors.hahahaha!!!!!!!!!!!
   
 4. a

  amigooo Senior Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni vema kama binadamu anaweza kujitambua kiafya. Napenda sana hiyo elimu watu kuwa nayo. Mtu yeyote anayeweka comments ambazo hazijui kawaida ni mjinga na anahitaji kupewa elimu pia.
   
Loading...