pata gesi ya kupikia isiyohitaji gharama za ujazaji milele kutoka simgas kwa ofa maalum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

pata gesi ya kupikia isiyohitaji gharama za ujazaji milele kutoka simgas kwa ofa maalum

Discussion in 'Matangazo madogo' started by simgas1, Aug 7, 2012.

 1. s

  simgas1 Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Simgas Tanzania Limited ni wauzaji na watengenezaji wa mitambo ya gesi inayotumia mabaki na taka za vyakula. Mitambo hiyo ina muonekano kama wa simtank wa lita 2000 ambao utakaa nje ya nyumba yako. Eneo linalohitajika kuweka huo mtambo ni approximately 2 x2 meters. Ndani ya mtambo huo kuna bacteria maalumu waitwao methanogenic bacteria ambao watafanya kazi ya kumeng'enya mabaki na taka za vyakula na mmeng'enyo huo utazalisha methane gas kwa ajili ya kupikia. Mabaki na taka za vyakula ni kama; maganda ya nyanya, viazi , ndizi zote mbivu na mbichi, mihogo, maganda ya mboga za majani, maganda ya matunda aina zote isipokuwa machungwa, limao na passion vilevile ukoko wa ugali,ukoko wa wali pamoja na vipolovipolo vyote.

  Simgas Tanzania Limited inaweletea kwenu gas mpya iitwayo gas 2000 yenye tanki lenye ujazo wa lita elfu mbili. hii ni baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika bidhaa yetu ya awali inayoitwa gas 550. Tofauti na gesi 550 ambayo ni mahususi kwa ajili ya matumizi ya familia ndogo, gesi 2000 inakidhi zaidi matumizi ya familia kubwa pamoja na migahawa na hotel saizi ya kati. Zinahitajika kuanzia kilo nne tu za taka kwa siku pamoja na maji lita arobaini na utaweza kujipatia gesi ya kupikia kwa masaa manne mfululizo kwa kuwasha moto mkubwa kabisa na plate zote mbili. gesi ikiisha baada ya masaa manne itajijaza yenyewe baada ya masaa mengine matano...hauhitaji kulisha tena kulisha ni mara moja kwa siku.

  Simgas watakuuzia mtambo wa gesi 2000 watakupa na jiko la plate mbili buree pamoja na huduma ya kuletewa na kufungiwa mtambo. Guarantee ni miaka miwili

  gesi 2000 inagharimu shiling 950000 lakini Simgas Tanzania LTD inatoa ofa kwa wateja mia moja wa mwanzo, hii ni kwa wateja wa Dar es Salaam tu. Utalipa sh 50000 tu na utafungungiwa mtambo na kila mwisho wa mwezi utahitajika kulipa sjh. 50000 tu, hii itamchukua mteja miezi 18 kumaliza deni lote. (ni nzuri eeh) Ukichelewa itakugharimu kulipia sh 950000 yote ili kupata mtambo

  Kwa kununua tafadhali wasiliana nami moja kwa moja kupitia simu yangu ya kiganjani 0714519831. Mimi naitwa Upendo ni sales team leader wa simgas. tembelea tovuti yetu Welcome to SimGas

  Ahsanten
   
 2. M

  MTK JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  "Zinahitajika kuanzia kilo nne tu za taka kwa siku pamoja na maji lita arobaini na utaweza kujipatia gesi ya kupikia kwa masaa manne mfululizo"

  May this is good for the environment! but it is too laborious and inconvinient to operate in a household! the way I see it ni kama household haiwezi ku-generate taka kiasi hicho then ama watakosa nishati ua walazimike kuajiri mkusanya takataka with all its attendat unpleasantness that task carries with it!!
  Je hamuwezi kuingia makubaliano na halmashauri za miji mbali mbali ili muwe agents wa kukusanya taka ngumu na laini then mnaproccess hiyo gas na kuipaki kwenye cylinders the put in retail outlets ili mlaji aondokane na kadhia ya kukusanya takataka!
   
 3. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  That is a good idea. They may work on it and it can contribute alot on enviromental conservation.
  Thanks
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Tunashukuru Kamanda wetu!


  Hii ni issue kwa jinsi Nchi yetu inakoelekea!

  Nambari lengwa nimeichukuwa kwa mawasiliano zaidi!

  Pamoja sana!
   
 5. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ni kitu nzuri, ila wasiwasi wangu ni kuwa watanzania wangapi can afford 950,000/=
   
 6. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mkuu kama una kaa dar kwa siku unatumia mkaa wa sh ngapi?? kila kitu watu ni kulalamika jamani sasa afanye huduma bila faida??
   
 7. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Lita arobaini za maji ni kila siku au ni za kuanzia tu.
   
 8. bank

  bank Senior Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamamani mkaa umepitwa na wakati sana tunakushukuru mkuu kwa taarifa
  Hebu tuwaunge mkono wajsiriamali anwabunifu wetu wa tz kwa mawzo badala ya kulalamika bei kubwa tu.

  Ila hilo tank halitoi harufu???
  May god bless our peple
   
Loading...