Pata faida kwa kufanya biashara ya Maziwa mtindi

MTEGULE

Member
Jul 16, 2021
15
21
ONGEZA KIPATO ZAIDI KWA KUSINDIKA NA KUFANYA BIASHARA YA MAZIWA MTINDI.

Watu wengi wamegubikwa na kutofahamu kiundani hasa kuhusu utengenezaji na ufanyaji biashara ya Maziwa mtindi na kushindwa kutumia fursa hii adhimu inayoweza kuongeza kipato zaidi katika maisha.

Maziwa ni malighafi ambayo inatokana na mifugo kama vile ng'ombe n.k.Tanzania inashika nafasi ya pili Afrika kwa ufugaji wa ng'ombe, Tanzania ina idadi ya ng'ombe zaidi ya millioni 24.3 na hizi ni takwimu za mwaka 2013. Na nchi ya kwanza kwa kuwa na ng'ombe nyingi ni Sudan.

Takwimu kutoka bodi ya maziwa inaeleza wastani wa unywaji wa maziwa mtu mmoja kwa mwaka umefikia lita 43.Lakini shirika la afya duniani (WHO) linapendekeza lita 200 kwa mwaka kwa mtu mmoja.

Kwa mantiki hiyo tunabainikiwa kwamba Tanzania inayo mifugo ya kutosha hasa ng'ombe hivyo upatikanaji wa maziwa upo kulingana na sehemu husika. Hivyo ni vyema kutumia fursa ya usindikaji wa maziwa ili kujiongezea kipato zaidi.

Hapa Tanzania ipo mikoa mbalimbali ambayo ina mifugo mingi hasa Ng'ombe. kutoka katika ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi imeweka wazi mikoa inayoongoza kwa ufugaji wa ng'ombe ikiwemo Dodoma,mbeya,manyara,Geita,Mwanza,mara,Arusha,Shinyanga,singida na Tabora.

Hapa mkononi ninao mfano uliohai ambapo unaweza kuanzisha kituo kidogo au kikubwa cha utengenezaji wa Maziwa mtindi kwa kutumia gharama ndogo..Mfano, Mkoa wa pwani ambayo haupo katika mikoa yenye mifugo mingi kutokana na takwimu, maeneo kama vile Chalinze,bagamoyo,mboga, mdaula,mbala,ubena,pingo na Lugoba haya ni maeneo ambapo kuna upatikanaji mzuri wa malighafi ya maziwa takribani mwaka mzima kutokana na uwepo wa wakulima na wafugaji wengi, na wafugaji wengi ni wamasai.

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUFUNGUA KITUO CHA USINDIKAJI WA MAZIWA MTINDI.

(i) Lazima uwe na ujuzi wa namna ya kuyatengeneza maziwa mtindi kwa namna iliyo bora kabisa.

(ii) Lazima uwe na eneo maalum (Kituo)kwa ajili ya kupokea maziwa kutoka kwa wafugaji.

(iii)Lazima uwe na vifaa kwa ajili ya Usindikaji(utengenezaji) wa maziwa kama vile Freezer(Jokofu), pipa la kuchemshia maji, Keni la kuchemshia maziwa,kipima joto (Thermometer) kwa ajili ya kupima joto la maziwa, kipimo cha maziwa kama yana maji(Lactometer), Ndoo ndogo za lita kumi na ndoo kubwa za lita ishirini kwa ajili ya kuhifadhia maziwa.

Hizo ni hatua tatu muhimu sana ambazo lazima uzingatie ili kuweza kufanya mchakato wa uzalishaji wa maziwa mtindi.

Mfano maeneo kama Chalinze, Bagamoyo, Mdaula, Ubena, Lugoba, Mboga, Pingo, Mbala, Vigwaza..Usafirishaji wa maziwa mtindi huwa ni kila siku kwani yapo magari maalumu kwa ajili ya usafirishaji na bei yake ni rahisi mnoo.

Soko la maziwa mtindi, kwanza lipo soko la ndani ambalo ni pale pale kituoni ulipofungua wateja huja kwa ajili ya kupata huduma unayotoa, pia soko la nje ambalo ni kusafirisha kutoka shamba(Kituoni) mpaka mjini..ambapo soko la uuzaji wa maziwa ni UBUNGO..mkabala na kituo cha mwendokasi cha UBUNGO-MAJI.

Bei elekezi ya uuzaji wa maziwa kutoka shamba mfano kipindi cha mvua nyingi mwezi wa pili mwishoni hadi mwezi wa sita mwishoni Lita maziwa mtindi huwa Tsh 1500/= na maziwa Fresh huwa ni 1200/= hiyo ni kwa bei ya jumla..na bei ya wakulima au wafugaji lita huwa ni Tsh 700/= hadi Tsh 800/=

Na kipindi ambacho maziwa hupungua kidogo ni msimu wa kiangazi kuanzia mwezi wa nane hadi mwezi wa kumi mwishoni ambapo bei ya maziwa mtindi huwa ni Tsh 1700/= kwa lita, na Tsh 1400/= kwa lita maziwa Fresh. Na bei ya wakulima au wafugaji shamba huwa ni Tsh 900/= hadi Tsh 1000/= kwa lita.

Lakini pia unaweza pata faida zaidi kwa kufungua sehemu yako ya biashara ya kuuza maziwa hapa hapa mjini ili kupata wateja zaidi na utauza kwa bei kuanzia Tsh 2000/= na kuelendelea kwa lita moja.

Hivyo ni kutokana na uwezo wako wa kupokea maziwa unaweza pokea lita 100 au 150 au 200 au 300 na kuendelea na kadri unavyopokea mzigo mkubwa na faida inaongezeka maradufu.

Maziwa mtindi ni hitaji kubwa mnoo kwa watu hivi sasa na upatikanaji wake umekua si wa kiwango kikubwa, na pengine wengi wetu hununua yale maziwa mtindi ya dukani ambayo athari zake zinafahamika..Tumia fursa hii kujiongezea kipato na kulinda afya za walaji.

Naomba kuwasilisha.
 
Shukurani zangu kwako mkuu lkn vp inachukua muda gani maziwa kuharibika tok uyapokee kutoka kwa mfugaji
Ni biashara ngumu. Jamii kubwa haija fahamu ubora wa mtindi baada ya kuyapika maziwa na ule mtindi asili, ambao huuzwa kwa bei ndogo.
 
ONGEZA KIPATO ZAIDI KWA KUSINDIKA NA KUFANYA BIASHARA YA MAZIWA MTINDI.

Watu wengi wamegubikwa na kutofahamu kiundani hasa kuhusu utengenezaji na ufanyaji biashara ya Maziwa mtindi na kushindwa kutumia fursa hii adhimu inayoweza kuongeza kipato zaidi katika maisha.

Maziwa ni malighafi ambayo inatokana na mifugo kama vile ng'ombe n.k.Tanzania inashika nafasi ya pili Afrika kwa ufugaji

Naomba kuwasilisha.
TANGAZO KWA WADAU WA MAZIWA KUHUDHURIA MAFUNZO YA MUDA FUPI

Fungua pdf chini kusoma tangazo hili na kumbuka malazi yatatolewa bure kwa mshiriki atakaye hitaji.
 

Attachments

  • lita Mafunzo ya Muda Mfupi-Maziwa.pdf
    419 KB · Views: 253
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom