Pastor Faustin Munishi(Malebo) aitolea nje ccm na Mary Nagu..

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,941
Ilikuwa ni katika tamasha la injili lililofanyika hapa Katesh Manyara kama ninavyomnukuu kutoka kwenye fb page yake:

POST 1:
Munishi Faustin DailyNews
KASHFA YA CCM KUUA WANAHABARI NI DOA KUBWA KWA SERIKALI YA KIKWETE. JE SABUNI GANI ITATOA DOA HILO? JE NI MARY NAGU?

Serikali ya CCM inakabiliwa na SCANDAL. ya Polisi wake kuua mwanahabari. Walitaka kutumia Tamasha la nyimbo za Injili kupooza moto unaowawakia CCM. Walimtaka Mchungaji anichagulie wimbo nitakaoimba. Walitaka niimbe ule usemao wanahabari ni wanafiki. Nikawaambia Nina ratiba ya nyimbo nitakazoimba na sikuwaambia ni wimbo upi.

SONGOMBINGO IKAANZIA HAPO. Sikubaliani na Serikali katika kuua mwanahabari akiwa kazini. Hata kama alikosea CCM walipaswa
kumfikisha mahakamani siyo kumuua. Kuutumia wimbo wangu kujaribu kuuonyesha umma kwamba ilikuwa sahihi kwa serikali kuua
mwanahabari siyo sahihi. Na CCM kuutumia wimbo wangu kama fimbo kuchapa wanahabari siyo sahihi.

Ningekubali masharti TBC TV YA TAIFA wangerusha Live. lakini hivi niliwagomea hata habari Leo hawataandika tena. Na mchezo umeishia hapo. Munishi hanunuliki na huwezi kumtumia kwa maslahi yako asijue.

Na hapa AKIBEZA tabia ya wanasiasa kujifanya wanaharaka wawapo kwenye tafrija mbalimbaki

POST 2:Munishi Faustin DailyNews

Waziri anapoudhuria ghafla ya kidini na kuomba kuondoka mapema kabla ibada kumalizika. Kwanza anavuruga ratiba. Inabidi Mchungaji akatize ibada amsindikize. Mchungajiakitoka na mgeni wake mwanasiasa ibada inapoteza mwelekeo. Washirika wanabaki na mbwembweza mwanasiasa kuingia na kutoka. Jesi ingekuwa vyema kama mwanasiasa ameamua kuja. kanisani akae hadi mwisho wa ibaada?

Au wanasiasa wana haraka kuliko Mungu? Nazungumza kumhusu WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk Mary Nagu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la kusifu na kuabudu Wilaya ya Hanang¡¯ mkoani Manyara.
 
Huu ni uamuzi mzuri kwa Pastor.
Maana unaposhirikiana na mwizi, fisadi na muuaji, moja kwa moja na wewe unashiriki dhambi zake zote alizozifanya.
Maana watu wawili hawawezi kuwa pamoja na kushirikiana bila kupatana katika mambo yao yote.
 
Ni hatarii na uzuri wa munishi sio mnafiki hata huko kenya huwa hamung'unyi maneno kwa watawala
 
Watu wa Mungu wanatakiwa waonyeshe njia kama ulivyofanya na si kujikomba kwa wanasiasa njaa
 
Waziri anapoudhuria ghafla ya kidini na kuomba kuondoka mapema kabla ibada kumalizika. Kwanza anavuruga ratiba. Inabidi Mchungaji akatize ibada amsindikize. Mchungajiakitoka na mgeni wake mwanasiasa ibada inapoteza mwelekeo. Washirika wanabaki na mbwembweza mwanasiasa kuingia na kutoka. Jesi ingekuwa vyema kama mwanasiasa ameamua kuja. kanisani akae hadi mwisho wa ibaada? Au wanasiasa wana haraka kuliko Mungu? Nazungumza kumhusu WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji na
Uwezeshaji Dk Mary Nagu
anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi kwenye tamasha la
kusifu na kuabudu Wilaya ya
Hanang¡¯ mkoani Manyara.

Mkuu eleza vizuri, hiyo ilikuwa hafla AU Ibada?

Kwa vyovyote vile kama ni Ibada, pengine huyo Mchungaji hajapitia mafunzo ya kuendesha Ibada.
Hairuhusiwi kabisa kukatisha Ibada iliyoanza kwa shughuli nyingine yoyote, sembuse kumsindikiza mwanasiasa.

Kama ulichoandika ni kweli basi hapo si Ibada bali mkutano wa wanasiasa na waumini tu.
 
Ilikuwa ni ibada ambapo iliimbtana na tamasha la nyimbo
Mkuu eleza vizuri, hiyo ilikuwa hafla AU Ibada?

Kwa vyovyote vile kama ni Ibada, pengine huyo Mchungaji hajapitia mafunzo ya kuendesha Ibada.
Hairuhusiwi kabisa kukatisha Ibada iliyoanza kwa shughuli nyingine yoyote, sembuse kumsindikiza mwanasiasa.

Kama ulichoandika ni kweli basi hapo si Ibada bali mkutano wa wanasiasa na waumini tu.
 
Kila ccm wanapoingia wanatolewa mbio kama mbwa mwizi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom