Passport: Maombi ya Hati ya Kusafiri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wana jamvi nauliza mwenye uelewa wa jinsi ya kupata passport kubwa na gharama zake halisi na zisizo halisi na njia zake halali na zisizo halali lakini iwe ni passport halali ya kusafiria
 
Intentional passport uwe na kilo 2 kwa shot kat
Direct n kilo 1 uisubirie
Kwa 1 months
 
pasport ni 50K no any usumbufu kama umejaza form vizuri na kusubmit documents zote wanazotaka na unapata not less than 14days
ukikutana na wahuni uko wakakupiga aya umeamua mwenyew
NB: magu alivyoingia nilisikia vitabu vilidimika watu wakawa wanapigwa cha juu otherwise ni 50k
 
pasport ni 50K no any usumbufu kama umejaza form vizuri na kusubmit documents zote wanazotaka na unapata not less than 14days
ukikutana na wahuni uko wakakupiga aya umeamua mwenyew
NB: magu alivyoingia nilisikia vitabu vilidimika watu wakawa wanapigwa cha juu otherwise ni 50k
Mkuu nipe mwongozo natakiwa kuwa na nini na nini ili niwe nimekamilika na ili nisipigwe nianzie wapi msaada tafadhali
 
Mkuu nipe mwongozo natakiwa kuwa na nini na nini ili niwe nimekamilika na ili nisipigwe nianzie wapi msaada tafadhali
kama uko dar, nenda hapo migration posta mpya hapo karibia na exime bank chukua form au INGIA KWENYE WEBSITE UDOWNLOAD IYO FORM then kaijaze vizuri na izo few documents watakazoziitaji ukimaliza rudisha pale kama iko ok utaambiwa ukalipie the rest unasubiria passport yako usisahau kupiga picha nzuri yenye utambulisho wa sura yako
masikio
forehead
macho
kidevu
colour ya picha sidhani kama wanashida kama walivyo wa visa
hope nimejitahid kidogo kukuelewesha ninachoelewa karibu tena
 
si kweli. msipende kutanguliza rushwa kwenye kila jambo, badilikeni watanzania. mimi nilipata passport ndani ya siku 2 na sikuombwa rushwa hata kidogo na mimi ni mtoto wa mkulima tu
Mkuu mimi nataka kusafiri kwaajili ya Masomo na biashara pia, sasa hata fomu zao naona wameweka orodha ndefu sana ya sababu, Je, nikitaja sababu yoyote na nikapata permanent passport labda ya binafsi naweza pia kuitumia hata kwa ajili ya masoko nk ?

Any help ?

Matola warumi
 
Mkuu mimi nataka kusafiri kwaajili ya Masomo na biashara pia, sasa hata fomu zao naona wameweka orodha ndefu sana ya sababu, Je, nikitaja sababu yoyote na nikapata permanent passport labda ya binafsi naweza pia kuitumia hata kwa ajili ya masoko nk ?

Any help ?

Matola warumi
Ndio unatumia tu passport kwa safari zozote za nje baada ya kupewa
 
kama uko dar, nenda hapo migration posta mpya hapo karibia na exime bank chukua form au INGIA KWENYE WEBSITE UDOWNLOAD IYO FORM then kaijaze vizuri na izo few documents watakazoziitaji ukimaliza rudisha pale kama iko ok utaambiwa ukalipie the rest unasubiria passport yako usisahau kupiga picha nzuri yenye utambulisho wa sura yako
masikio
forehead
macho
kidevu
colour ya picha sidhani kama wanashida kama walivyo wa visa
hope nimejitahid kidogo kukuelewesha ninachoelewa karibu tena
Ahsantee mkuu
 
Passport zipo kwa ukata xa hvi shortly haztolewi kwa commona labda wagonjwa wanajesh na wafanyakazi Wa serikali waliotumwa kikaz ndo maana lazma uwe na dau la kutosha kuipata
Kwa nini wanazibania, wanataka tufanye nini sasa wakati tunataka kujilipua nje tukabebe box.
 
Mimi ni raia wa Tanzania ambae kwa sasa nipo nchini Ureno, nimepoteza paspoti yangu iliotolewa mwaka 2005(hizi mpya), jambo linalonitatiza ni kuwa hawa balozi wetu hawataki kunisaidia!

Wanasema lazima niende Paris ili nikafanye maombi mapya na kuchukuliwa alama za vidole, lakini mwaka 2005 nilichukuliwa finger print, Je ni lazima kila mtu anapotaka passpoti achukuliwe alama? Huu si mchezo umekuwa kwa maana wenzetu wakichukuliwa basi huwekwa kwenye data base. Kuna msaada gani wa kisheria mnaoweza kunipa wenzangu??

============
============

Yapo mambo ambayo huwaumiza watu vIchwa yumkini yakiwa ni mambo madogo na ya kawaida. Tatizo mara nyingi huwa ni taarifa. Taarifa zikimfikia mtu ndipo huhisi jambo ambalo alikuwa halijui kuwa ni jepesi.
Lakini kabla ya taarifa mtu huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu.

Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la anasa au ufahari tena isipokuwa ni jambo ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida ya kila siku ya walio wengi. Hii ni kutokana na kukua kwa biashara za kimataifa, mawasiliano, utalii,usafirishaji na kila kitu ambacho husababisha watu kutoka nchi moja hadi nyingine.

Kwasasa kuwa na pasipoti hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo muhimu sana. Yumkini usisubiri ikutokee safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana na pasipoti. Pasipoti inayo manufaa mengi lakini moja ni kuwa pasipoti ni mali kama mali nyingine. Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama mali nyingine inavyoweza kumdhamini mtu.Pasipoti ni amana tena amana ya kuaminika. Ni kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze pasipoti na namna ya kupata pasipoti.

1. PASIPOTI HUOMBWA NA MWOMBAJI LAKINI HUBAKI MALI YA SERIKALI.

Hakuna mtu mwenye umiliki wa kudumu wa pasipoti. Kwa mujibu wa sheria licha ya kuwa pasipoti hutolewa kwa jina na maelezo ya mwombaji,hati hiyo hubaki kuwa ni mali ya serikali. Hii ndio sababu serikali huweza kumnyanganya mtu pasipoti panapo jambo fulani. Ni kwakuwa pasipoti ni mali yake. Wewe mwombaji uliyepewa pasipoti unayo haki ya matumizi na uhifadhi wake lakini mmiliki mkuu ni serikali.

2.ILI KUPATA PASIPOTI UNAHITAJI KUWA NA VITU HIVI.

( a ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha mwombaji.Cheti cha kuzaliwa ni hivi vyeti vya kawaida ambavyo hutolewa mahospitalini au mamlaka nyingine baada ya kuzaliwa kwa mtu. Katika kipindi hiki wapo wengine wamekwisapata vyeti vya uraia. Cheti cha uraia chaweza kutumika kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa. Pia tumesema hati ya kiapo. Hii hutolewa kwenye ofisi za wanasheria. Mwombaji huwa anaapa pamoja na mambo mengine kuthibitisha kuwa taarifa anazozitoa ni za kweli kwa dhati yake. Pia tukasema vyeti vya uraia wa kuandikishwa. Hivi wanavyo raia wa Tanzania ambao si wa kuzaliwa. Katika kuomba kupata pasipoti nao hutakiwa kuwa navyo.

( b ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha
mzazi au wazazi wa mwombaji. Hapo juu tumeona vitu kama hivihivi lakini ilikuwa ni kwa mwombaji wa pasipoti mwenyewe. Hivi hapa sasa ni kwa ajili ya mzazi wa mwombaji. Vile vitu vyote alivyowasilisha mwombaji pale juu ndio vilevile anavyopaswa kuwasilisha mzazi wa mwombaji. Si kwamba mzazi mwenyewe ndio anapeleka vitu hivyo hapana, wewe mwombaji ndio unabeba vitu hivi kwa niaba ya mzazi. Hapa mzazi ni yeyote anaweza kuwa baba au mama.Lengo lake ni kutaka kujua historia fupi ya nasaba ya mzazi wa mwombaji.

( c ) Inahitajika picha ya hivi karibuni ya pasipoti size. Sharti kubwa waliloweka hapa ni kuwa picha hiyo isiwe katika fremu. Fremu hapa si tu ile fremu ya kawaida tuliyoizoea bali pia hata pasipoti kuwa na maringo au mapambo ya kuzungushia pembeni nayo ni fremu kwa maana hii. Pasipoti iwe mnyooko(plain) isiwe na mbwembwe zozote.

( d ) Iwapo mwombaji ana umri wa chini ya miaka kumi na nane (18), wazazi walezi wawasilishe ridhaa ya maandishi. Nyaraka hii ya ridhaa ya maandishi huandaliwa na mwanasheria.Hii ni kusema kuwa utaratibu wa mtu mzima aliyevuka miaka kumi na nane ni tofauti na mtu aliye chini ya miaka hiyo katika kupata pasipoti. Baada ya kukamilisha vitu hivi kama nilivyoeleza basi hatua inayofuata ni kufuata utaratibu huu chini.

3.FOMU ZA MAOMBI HUPATIKANA WAPI.

Ofisi za uhamiaji ndipo zilipo fomu za maombi ya pasipoti. Hii ni popote Dar es salaam au mikoani. Suala la msingi ni kuwa ofisi hiyo iwe ya uhamiaji utapata fomu hizo. Utachukua fomu hiyo utaijaza na baada ya kuijaza itawasilishwa kwa mkurugenzi wa uhamiaji. Aidha suala jingine la msingi ni kuwa fomu hii itawasilishwa sambamba na nyaraka zote zinazotakiwa kama ilivyoelezwa hapo juu.

4.BEI YA PASIPOTI NI KIASI GANI.

Ada rasmi ya kupata pasipoti ni fedha za Kitanzania kiasi cha shilingi 50,000/=( Elfu hamsini tu). Aidha kwakuwa wanasheria ndio hushughulika na kutafuta pasipoti basi bei yao haiingizwi katika ada rasmi ya serikali kama nilivyoieleza hapo juu.

5.UNAWEZA KUOMBWA VIAMBATANISHO VYA ZIADA.

Jambo jingine ni kuwa safari zimeainishwa kwa namna mbalimbali.Ukisoma nyuma ya fomu ya maombi utaliona hili. Kutokana na hilo wakati mwingine waweza kuombwa viambatanisho vya ziada. Hii ni kutokana na utofauti wa safari. Hii ni kusema kuwa yawezekana mwombaji akaombwa viambatanisho viitwavyo viambatanisho &[HASHTAG]#8220[/HASHTAG];maalum&[HASHTAG]#8221[/HASHTAG];. Hivyo basi mtu asishangae kukutana na kitu cha namna hiyo.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
Mkuui kweli kama umepoteza Passport itabidi utoe Repoti kituo cha Polisi kisha upeleke Maombi yako Paris au Rome Italy na hiyo Sheria ya kuchukuliwa alama za vidole ipo nchini Tanzania tangu kulipo tokea Matatizo ya Ugaidi nchini Amerika mnamo Mwaka 2001 Marekani ndio aliye anzisha Sheria hiyo sasa na hapo kwetu tunaiga mambo ya Amerika kila wanacho kifanya. Kama huko Ureno hakuna Ubalozi wa Tanzania. Tafuta Form ya Maombi y Passport toka nyumbani Tanzania uletewe huko Ureno Ujaze form na kupiga alama zako za vidole na kutuma Maombi yako ya Passport Mpya Ubalozini nchini Italy au Mjini Paris bila ya hivyo huwezi kupata Passport Mpya. Mmi huku nilipo hakuna Ubalozi wa Tanzania tunatumia Ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Italy mjini Rome.
 
Wapendwa naomba kuuliza,,,ukiwa na mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 2 na unataka kusafiri nae pia unahitaji kumkatia passport?maana mimi nina passport yangu ya miaka 10 na bado miaka 6 ndo ita expire na ninahitaji kusafiri na mtoto nje ya Afrika na bado sijajua nifanyeje,,msaada tafadhali
 
Back
Top Bottom