Passport: Maombi ya Hati ya Kusafiri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Passport: Maombi ya Hati ya Kusafiri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mtu kitu, Apr 28, 2011.

 1. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Mimi ni raia wa Tanzania ambae kwa sasa nipo nchini Ureno, nimepoteza paspoti yangu iliotolewa mwaka 2005(hizi mpya), jambo linalonitatiza ni kuwa hawa balozi wetu hawataki kunisaidia!

  Wanasema lazima niende Paris ili nikafanye maombi mapya na kuchukuliwa alama za vidole, lakini mwaka 2005 nilichukuliwa finger print, Je ni lazima kila mtu anapotaka passpoti achukuliwe alama? Huu si mchezo umekuwa kwa maana wenzetu wakichukuliwa basi huwekwa kwenye data base. Kuna msaada gani wa kisheria mnaoweza kunipa wenzangu??

  ============
  ============

  Yapo mambo ambayo huwaumiza watu vIchwa yumkini yakiwa ni mambo madogo na ya kawaida. Tatizo mara nyingi huwa ni taarifa. Taarifa zikimfikia mtu ndipo huhisi jambo ambalo alikuwa halijui kuwa ni jepesi.
  Lakini kabla ya taarifa mtu huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu.

  Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la anasa au ufahari tena isipokuwa ni jambo ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida ya kila siku ya walio wengi. Hii ni kutokana na kukua kwa biashara za kimataifa, mawasiliano, utalii,usafirishaji na kila kitu ambacho husababisha watu kutoka nchi moja hadi nyingine.

  Kwasasa kuwa na pasipoti hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo muhimu sana. Yumkini usisubiri ikutokee safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana na pasipoti. Pasipoti inayo manufaa mengi lakini moja ni kuwa pasipoti ni mali kama mali nyingine. Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama mali nyingine inavyoweza kumdhamini mtu.Pasipoti ni amana tena amana ya kuaminika. Ni kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze pasipoti na namna ya kupata pasipoti.

  1. PASIPOTI HUOMBWA NA MWOMBAJI LAKINI HUBAKI MALI YA SERIKALI.

  Hakuna mtu mwenye umiliki wa kudumu wa pasipoti. Kwa mujibu wa sheria licha ya kuwa pasipoti hutolewa kwa jina na maelezo ya mwombaji,hati hiyo hubaki kuwa ni mali ya serikali. Hii ndio sababu serikali huweza kumnyanganya mtu pasipoti panapo jambo fulani. Ni kwakuwa pasipoti ni mali yake. Wewe mwombaji uliyepewa pasipoti unayo haki ya matumizi na uhifadhi wake lakini mmiliki mkuu ni serikali.

  2.ILI KUPATA PASIPOTI UNAHITAJI KUWA NA VITU HIVI.

  ( a ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha mwombaji.Cheti cha kuzaliwa ni hivi vyeti vya kawaida ambavyo hutolewa mahospitalini au mamlaka nyingine baada ya kuzaliwa kwa mtu. Katika kipindi hiki wapo wengine wamekwisapata vyeti vya uraia. Cheti cha uraia chaweza kutumika kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa. Pia tumesema hati ya kiapo. Hii hutolewa kwenye ofisi za wanasheria. Mwombaji huwa anaapa pamoja na mambo mengine kuthibitisha kuwa taarifa anazozitoa ni za kweli kwa dhati yake. Pia tukasema vyeti vya uraia wa kuandikishwa. Hivi wanavyo raia wa Tanzania ambao si wa kuzaliwa. Katika kuomba kupata pasipoti nao hutakiwa kuwa navyo.

  ( b ) Cheti cha kuzaliwa, hati ya kiapo au cheti cha uraia wa kuandikishwa cha
  mzazi au wazazi wa mwombaji. Hapo juu tumeona vitu kama hivihivi lakini ilikuwa ni kwa mwombaji wa pasipoti mwenyewe. Hivi hapa sasa ni kwa ajili ya mzazi wa mwombaji. Vile vitu vyote alivyowasilisha mwombaji pale juu ndio vilevile anavyopaswa kuwasilisha mzazi wa mwombaji. Si kwamba mzazi mwenyewe ndio anapeleka vitu hivyo hapana, wewe mwombaji ndio unabeba vitu hivi kwa niaba ya mzazi. Hapa mzazi ni yeyote anaweza kuwa baba au mama.Lengo lake ni kutaka kujua historia fupi ya nasaba ya mzazi wa mwombaji.

  ( c ) Inahitajika picha ya hivi karibuni ya pasipoti size. Sharti kubwa waliloweka hapa ni kuwa picha hiyo isiwe katika fremu. Fremu hapa si tu ile fremu ya kawaida tuliyoizoea bali pia hata pasipoti kuwa na maringo au mapambo ya kuzungushia pembeni nayo ni fremu kwa maana hii. Pasipoti iwe mnyooko(plain) isiwe na mbwembwe zozote.

  ( d ) Iwapo mwombaji ana umri wa chini ya miaka kumi na nane (18), wazazi walezi wawasilishe ridhaa ya maandishi. Nyaraka hii ya ridhaa ya maandishi huandaliwa na mwanasheria.Hii ni kusema kuwa utaratibu wa mtu mzima aliyevuka miaka kumi na nane ni tofauti na mtu aliye chini ya miaka hiyo katika kupata pasipoti. Baada ya kukamilisha vitu hivi kama nilivyoeleza basi hatua inayofuata ni kufuata utaratibu huu chini.

  3.FOMU ZA MAOMBI HUPATIKANA WAPI.

  Ofisi za uhamiaji ndipo zilipo fomu za maombi ya pasipoti. Hii ni popote Dar es salaam au mikoani. Suala la msingi ni kuwa ofisi hiyo iwe ya uhamiaji utapata fomu hizo. Utachukua fomu hiyo utaijaza na baada ya kuijaza itawasilishwa kwa mkurugenzi wa uhamiaji. Aidha suala jingine la msingi ni kuwa fomu hii itawasilishwa sambamba na nyaraka zote zinazotakiwa kama ilivyoelezwa hapo juu.

  4.BEI YA PASIPOTI NI KIASI GANI.

  Ada rasmi ya kupata pasipoti ni fedha za Kitanzania kiasi cha shilingi 50,000/=( Elfu hamsini tu). Aidha kwakuwa wanasheria ndio hushughulika na kutafuta pasipoti basi bei yao haiingizwi katika ada rasmi ya serikali kama nilivyoieleza hapo juu.

  5.UNAWEZA KUOMBWA VIAMBATANISHO VYA ZIADA.

  Jambo jingine ni kuwa safari zimeainishwa kwa namna mbalimbali.Ukisoma nyuma ya fomu ya maombi utaliona hili. Kutokana na hilo wakati mwingine waweza kuombwa viambatanisho vya ziada. Hii ni kutokana na utofauti wa safari. Hii ni kusema kuwa yawezekana mwombaji akaombwa viambatanisho viitwavyo viambatanisho “maalum”. Hivyo basi mtu asishangae kukutana na kitu cha namna hiyo.

  MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
   
 2. L

  Leornado JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa na tatizo kama lako, nilijuta na ninaendelea kujuta kwenda ubalozini kutafuta solution.

  Kama ulivyoelezwa, ilinilazimu kusafiri hadi ulipo ubalozi kuchukua finger prints na kujaza fomu. Wakaniambia baada ya wiki sita pasipoiti itakuwa tayari. Huwezi amini nilikaa zaidi ya mwaka bila ya kuletewa pasipoti, ukifuatilia hawaishi visingizio, mara muhusika kasafiri au piga baada ya nusu saa.Kilichonivunja nguvu ni waliponiambia wameshindwa kufatilia kama naweza nifatilie mwenyewe wizara ya mambo ya ndani au kama nina ndugu niwatume Dar wakanifuatilie.

  Nashukuru sheria za nchi niliyokuwapo pasipoti haikuwa na umuhinu sana.

  USHAURI: Kama una ndugu Dar, watumie data zako na pesa kidogo za process wizarani, utapata pasipoti yako fasta na cheap. Ila ukienda Paris, utaingia gharama ya hotel, usafiri, chakula na bado pasipoti yako ichukue mwaka kufika kama ilivyokuwa kwangu.

  Balozi zetu zipo kama urembo hawana msaada wowote ule kwa watanzania.
   
 3. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hilo ni kweli balozi zetu ni uhuni hawana msaada kabisa ni kama hapa china ni aibu ubalozi nikama wa ukoo fulani hawataki kutusaidia ukiwa natatizo sijui wako kwa ajili ya nani kama sio kuwakilisha nchi yetu au matumbo yao
   
 4. frozen

  frozen Senior Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Habari great thinkerz! Plz napenda kufahamu inaweza kumchukua mtu siku ngapi kupata passport ya kusafiria? Na inaweza kugarimu kiasi gani kuanzia kujaza form mpaka kupata pass yenyewe kwa hii ofisi yetu ya uhamiaji?
  Asanteni
   
 5. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Unaweza kupata kwa muda wa wiki moja tu, na bei yake shilingi elfu hamsini
   
 6. frozen

  frozen Senior Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nashukuru mkuu, kwa upande wa fomu,nazipata pale pale uhamiaji ? Asante sana
   
 7. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nenda ofisi yoyote ya uhamiaji au kwa mkuu wa wilaya uchukue form. Kuna sehemu za kujaziwa na watu kama mawakili na mdhamini pamoja na kubandika stamp za TRA then unawapelekea jamaa uhamiaji wanazipitia na kama ziko poa unaruhusiwa ukalipie then utapewa risit na watakwambia ni baada ya muda gani ukachukue passport yako ila najua siku hizi wameboresha huduma zao haitazi wiki 2!
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Elfu hamsini ndio bei na hii unaweza kuchukua hata miezi miwili,ila kama una hela laki na nusu ni siku mbili tu unapata kila kitu.
   
 9. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Yes 50,000 ndio bei halisi,
  But andaa kitu kama 150,000-200,000 na utaipata fasta,but sio siku2,ni kuanzia siku 4,pale kulasini kuna usumbufu mkubwa na foleni balaa.kua makini pia kunamatapeli,kama upo tayari ni mp nikupe mtu akusaidie.
   
 10. m

  mbutalikasu Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka ni kweli huduma zimeboreshwa sana ila kweli pale kurasini kuna foleni wewe ukitaka nenda ofisi za kinondoni, posta au temeke na uende moja kwa moja ofisini hadi kaunta nje kuna matapeli wengi sana na pia fomu zinapatikana uhamiaji tu na wala si kwingineko hata kwa mkuu wa wilaya hakuna kama kweli unahitaji sema nikupe mtu hapo k/ndoni au temeke
   
 11. a

  ammah JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mkuu ni wiki mbili tu...hakuna longolongo tena siku hizi.
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Fanya haya yafuatayo:

  1. Nenda ofisi za uhamiaji na uchukuwe fomu za maombi ya passport.

  2. Soma maelekezo na uzijaze kwa usahihi

  3. Nenda Mahakamani na uwaone makarani wa mahakimu na uwawezeshe kiasi cha pesa isiyozidi 10,000/= watakugongea muhuri wa hakimu kwenye hati ya kiapo iliyopo kwenye hizo fomu zako na watakubandikia pia stamp duty za thamani isiyopunguwa shilling 1000/= au kama una wakili wako anaweza yeye akakugongea huo muhuri wake kwenye hati ya kiapo badala ya kwenda mahakamani

  4. Ili kuepuka na longolongo za watu wa uhamiaji itabidi uattach na invitation letter kutoka kwenye nchi za ulaya au USA, hii itakusaidia kuepuka urasimu usiokuwa na mantiki. (naweza kukusaidia kipengele hiki online kama bado wewe ni mgeni hapa mjini)

  5. Jitahidi katika hao wazamini wako wawili wawe wanamiliki passport na utoe photocopy za passport zao uattach kwenye maombi yako (hizi ni strong supporting docs )

  6. uwe na cheti chako cha kuzaliwa na vyeti vya wazazi wako kama wanavyo na kama hawana uandae shilling 10,000/= kwa kila mmoja ili karani wa mahakama awaandalie Affidavit zao ambazo zitatumika kama vyeti vyao vya kuzaliwa, ila wewe mwenyewe cheti cha kuzaliwa ni lazima.

  Kama utafuata muongozo huo niliokupa basi hesabu umeshapata passport ila unasubili tarehe ya kuchukuwa tu.

  N:B, Msaada wangu online hautaji kulipia any consultation fee. vijisenti vyangu vinanitosheleza.
   
 13. N

  NIMIMI Senior Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inategemea na aina ya pasi unahitaji kwa ajili ya safari, maana kuna kama ifuatavyo;
  1. Emegency travel document (ETD) ama Shahada ya Safari ya DHARURA imeanishwa nchi unazoruhusiwa kusafiria Yaani KENYA, UGANDA, MALAWI, DRC, RWANDA, BURUNDI, ZAMBIA, &MSUMBIJI
  na bei yake ni Tsh. 10,000tu. Fomu zapatikana palepale ofisini unatakiwa kuwa na Picha 3ppt size blue background, cheti cha kuzaliwa cha mwombaji, cha mmoja kati ya wazazi wako, stempu za Tra 2 endapo utatumia viapo, barua kutoka serikali za mtaa.

  2. Pasipoti ya Kawaida (ORDINARY PASSPORT) Bei yake ni TSh 50,000tu bila chenga na pasi hii inakuwezesha kusafiri kwenda popote duniani, chamsingi uwe na viambata nilivyovitaja hapo mwanzo na barua ya uthibitisho wa safari yako na ni ndani ya siku 7 (saba) tangu kupokelewa kwa ombi lako unapata pasi yako, na uharaka wa pasipoti yako inategemea udharura wa safari yako na tatizo pia, mfano unaumwa mahututi unatakiwa ukatibiwe nje pasipoti yako inawezekana kuipata siku hiyohiyo.

  3. PASI YA AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN PASSPORT) Bei yake Tsh 15,000tu na inakuwezesha kusafiri katika nchi wanachama na inakuwezesha kufungua akaunti ya akiba katika nchi wanachama.

  Kumbuka ETD haitolewi makao makuu Kurasini na Epukana na Madalali na matapeli nenda moja kwa moja kwa afisa uhamiaji katika sehemu husika hasa ofisi za uhamiaji, pia uwanja wa ndege, bandarini na vituo vya kutokea na kuingilia ni vya uhamiaji, isipokuwa hakuna Pasipoti yeyote inayotolewa katika sehemu tajwa. Itangaze nchi yako kwa kutumia pasipoti ya nchi yako.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  [h=6]BBC Swahili
  [/h][h=6]Karibu katika Dira ya Dunia uko nami Wazir Khamsin na Suluma Kassim.Leo hii Tanzania yaorodheshwa miongoni mwa nchi zilizoshindwa kukabiliana na biashara haramu ya pesa,chama cha upinzani DRC chatishia kuwavua ubunge wanachama iwapo watahudhuria vikao vya bunge bila idhini.[/h]
   
 15. Nelsweeter

  Nelsweeter Senior Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakikisha uwe na safari ya kweli, sio safari magumashi. Kama huna barua za mwaliko za uhakika lazima wakulambe hela. Kama utasema unaenda kwa ndugu Ulaya au US watataka ulete uthibitisho wa residence permit ya ndugu yako au uraia wake ili wajue anaishije huko ng'ambo. Kuwa makini na huyo jamaa ayetaka kukutengenezea barua ya mwaliko, utapigwa maswali utashindwa kujitetea kwani hiyo barua utakuwa huijui vizuri. Kuna jamaa namfahamu anajuta mpaka sasa.
   
 16. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
 17. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Siyo kweli jamani sasa hivi pasport hazina usumbufu kupata. Mimi nilipeleka pale mambo ya ndani - upande wa uhamiaji ilikuwa maombi ya mtoto wangu sikumfahamu mtu. Wakaniambia nirudi baada ya wiki mbili lakini nilipoenda nikakuta ilishatoka baada ya siku 5 tu.
   
 18. Stahmy Junior

  Stahmy Junior Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wadau kwa mwenye upeo naomba mnisaidie..Gharama ya kupata hati ya kusafiria au paspoti kwa hapa kwetu Tanzania ni shilingi ngapi?
   
 19. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,377
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka nililipa Tshs 50,000/= na kupata ya miaka 10, na kama utataka ya muda nadhani ni tshs 15,000/=:spy:
   
 20. Stahmy Junior

  Stahmy Junior Member

  #20
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nashukuru 50,000 ni kila kitu bila gharama za pembeni au kuna vitu unalipia awali? we ulipata mwaka gani
   
Loading...