Paskal Mayala mbona hudadavui kuhusu chuki hii inavyoenea utawala huu?

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Paskali fahamu kuwa hata kabla sijaamua kujiunga rasmi JF nimekuwa nikisoma sana nyuzi zako. Mara nyingi umekuwa ukianzisha nyuzi ambazo na mimi nakuwa nimezifikiri na hivyo unakuwa umeniwasilishia kwa hakika. Lakini sio zile nyuzi ambazo sometimes zinafanya usieleweke.

Leo Paskali naona nikukumbushe tu kwa uzi wenye mtindo wa swali kwa sababu najua wewe ni "msoma trend" wa mambo ambayo huyaandika. Vipi tukiangalia suala la chuki katika nchi yetu - trend yake inaendaje? Paskali hujaandika kuhusu hili! Kwa nini? Unaogopa ama?

Anyway - Nakuuliza Paskali vipi mwelekeo wa jamii yetu kushikana na kuwa wamoja na kuipinga chuki dhidi yetu trend yake ikoje tangu uongozi huu uingie?

Paskali unaonaje matendo ya kwa mfano kupotea kwa wananchi na Serikali kuwa kimya kimya kimya kimya kimya sana - hayakuzi chuki katika nchi yetu?

Paskali matukio kutopepelezwa ya watu kupigwa risasi na mengine kutangazwa kufanyiwa upelelezi fasta ya watu kuhisiwa kupewa sumu - hayaleti chuki ya kuonesha upendeleo dhidi yetu?

Paskali vipi utaratibu kwa mfano wa kuijali jamii yetu mfano kuongeza mishahara kwa wafanyakazi - hii haijaleta chuki dhidi ya jamii yetu?

Paskali - vipi uendeshwaji wa siasa zetu ulivyo - Uchaguzi wa Serikali za mitaa ulivyofanyika mwaka jana na kupiga pin shughuli za kisiasa za wazi kwa upinzani tu wakati wa chama tawala wakijimwambafai - hii haijaleta chuki dhidi yetu?

Paskali - kubwa kuliko unaonaje kitendo cha Chama Tawala kwenda kumtoa yule Mwanachama wao aliyecross kutoka Chadema kwa kumlipia faini na kisha Polepole kuongea kwa Kiingereza kuitangazia dunia kuwa nao mwanachama wao alikuwa kafungwa - hii haijaleta chuki katika nchi yetu?

Paskali - unaonaje pia undugunaizesheni uliiooneshwa na Rais kwa Mheshimiwa Msigwa wakati akijua yeye Rais ni baba wa WaTanzania wote, haashirii kuwa wengine wakome wenyewe huko jela ila Ndugu yake Msigwa atoke - hii haijaleta chuki katika jamii yetu?

Paskali - ukiwa kama Mwanasheria unaonaje pia kuwa Hakimu angeweza tu kutamka kuwa kama wahukumiwa katika adhabu waliyopewa wanaamua kulipa faini awape muda wa kulipa faini na wakishindwa ndiyo wakamatwe kwenda jela na yeye akaamua waende kwanza jela na kisha walipe faini wakiwa huko huko jela ni kama wametumikia adhabu zote hizo kwa pamoja - yaani wameenda jela siku kadhaa halafu na wamelipa faini yote - hili halizidishi chuki katika jamii yetu?

Ndugu yangu Paskali ni mengi yanafanyika ambayo yanaashiria kukuza chuki badala ya kuleta amani na upendo katika nchi yetu. Hata kama kuna mipango mizuri ya kukuza uchumi wetu inatekelezwa lakini jamii inayojaa chuki ndani ya mioyo yao ni hatari sana huko mbeleni.

Kwangu mimi wewe ni kama unaongoza kujadili hoja rahisi na za maana katika Jukwaa hili lakini naona katika kuangalia mambo ya amani na upendo katika nchi yetu kwa kiasi kikubwa unakwepa kujadili.

Kazi njema Kaka Paskali!

Tila Lila2
 
Tila-lila2,
Mkuu you make it my day, hii ndio JF inayotakiwa welldone mkuu! umeandika Facts sio siasa na huu ndio uandishi mzuri wa mada, kipengele cha Hakimu kimeniumiza mno hasa why hakimu aliwapeleka jela moja kwa moja wakati ile hukumu ina option ya kulipa faini? why hakuendeleza dhamana yao ili awape muda wa kulipa na kushindwa kwao ndio wapelekwe jela? ona sasa wametumikia adhabu zote mbili kwa pamoja,je huu sio uonezi ?

Huyu hakimu ni mtanzania wenzetu ana familia yake na bila shaka na watoto,je amesend message gani kwa taifa, je ni kweli ali apply his mind wakati wa kutoa hii hukumu? tatizo la kila watendaji kuteuliwa kisiasa haya ndio matokeo yake, wenzetu idara kama hizi watarajiwa wanaomba na kufanyiwa usaili, na wanaoshinda hupewa na nafasi na kuapishwa na jaji kwa kutumia katiba (ili walinde katiba sio mpangaji mkuu wa pale magogoni, ambaye baada ya 10yrs anaondoka, ila katiba itabakia)AGAIN MTOA MADA WELLDONE MKUU.
 
Wandugu,
Ujasiri wa kusema kuhusu uvunjaji wa sheria na katiba ya nchi unaofanywa na JIWE:Mbabe kutoka Chato, anaejua kila kitu, asiekosolewa, ANAEWANIA urais wa milele ingawa hataishi milele, ambae hashuriki, aliyejaa majigambo hewa, anaelazimisha kupendwa; tutamwonea bure. Huyu Pascal Mayala wa sasa ni wazi hana. Labda angekuwa yule wa wakati wa (kipindi cha TV) KITIMOTO
 
Wandugu,
Ujasiri wa kusema kuhusu uvunjaji wa sheria na katiba ya nchi unaofanywa na JIWE:Mbabe kutoka Chato, anaejua kila kitu, asiekosolewa, ANAEWANIA urais wa milele ingawa hataishi milele, ambae hashuriki, aliyejaa majigambo hewa, anaelazimisha kupendwa; tutamwonea bure. Huyu Pascal Mayala wa sasa ni wazi hana. Labda angekuwa yule wa wakati wa (kipindi cha TV) KITIMOTO

Yule wa kitimoto ndo alikuwa paskali, nadhani aliacha photocopy yake yeye akaingia mitini. :D :D :p
 
Huu ukabila umeota mimi. Juzi Kati kulikuwa na usaili wa wathamini.
Moja ya swali ulikuwa unaulizwa ni wewe kabila gani mara unatoka mkoa gani.
Haya Mambo yanayoendelea sio ya kufumbia macho kabisa.
Taifa hili ni letu sote inapaswa kuishi Bila kujua wew kabila gani na Kanda ipi wa dhehebu gani.
Watu waache ujinga wao.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom