Pasha zaidi ya lita 100 kwa wakati mmoja - na maji hukaa siku tatu!

Jul 6, 2016
14
13
Ensol tunawaletea kwenu huduma mpya ya kifaa cha “Solar Water Heater”

Hiki kifaa kimeletwa kwenu maalum kuhakikisha unapunguza gharama za kuchemsha maji kwa ajili ya kuogea na shughuli zingine za jikoni.

v Ondoa gharama za umeme na gesi

v Inapatikana katika ujazo kuanzia lita 100

v Garantii mpaka miaka 5

v Inatunza maji ya moto mpaka siku 3

Inafaa kwa matumizi ya Nyumbani, Hoteli, Nyumba ya Wageni, Hospitali n.k

Kwa mdau yeyote mwenye swali, maoni au unahitaji ufafanuzi wowote, naomba uliza hapa kwenye mada hii na utajibiwa moja kwa moja.

Kwa maelezo zaidi naomba piga namba ya simu piga namba +255-22-2460-100 AU +255-786 630066

Ensol Tanzania

Solar WH.jpg
 
Ensol tunawaletea kwenu huduma mpya ya kifaa cha “Solar Water Heater”

Hiki kifaa kimeletwa kwenu maalum kuhakikisha unapunguza gharama za kupasha maji kwa matumizi mbali mbali kama vile chai, ya kuoga, ya kunawa (hii kwa migahawa na hoteli zinazojali wateja), na matumizi mengine yote.

Unaponunua kifaa hiki cha “Solar Water Heater” inakunufaisha kwa namna mbali mbali kama vile;

1. Kupasha maji zaidi ya lita 100 kwa wakati mmoja.

2. Kuondoa gharama za umeme na gesi linapokuja suala la kupasha maji.

3. Inatunza maji ya moto hadi siku tatu.

Kwa mdau yeyote mwenye swali, maoni au unahitaji ufafanuzi wowote, naomba uliza hapa kwenye mada hii na utajibiwa moja kwa moja.

Kwa maelezo zaidi naomba piga namba ya simu piga namba +255-22-2460-100 AU +255-786 630066

Ensol Tanzania
Sh ngapi?
 
Mkuu inaonekana hiki kifaa ni kizuri ila kuna mambo hujayaweka sawa.

Unazungumzia kuapsha tu au kuchemsha kabisa kwa centigrade 100 ??

Maana nachojua kupasha maana yake inakuwa partial heating.

Kingine bei zako zikoje??

Maana hujaeleza bei pia ambayo ni itu muhimu sana katika kujitanganza.
Asante sana Asigwa, mfumo huu ni wa kuchemsha maji mpaka centrigrade 80, na zinapatikana katika ujazo tofauti, kuna za kuanzia tanki la lita 100, 150 na 200.
bei zake nazo zinatofautiana kutokana na huo ujazo, mfano Tanki la lita 100 ni shilingi 785,000/, lita 150 ni shilingi 995,000/ na za lita 200 ni 1,350,000/. Gharama nyingine inayoongezeka hapo ni ufundi ambayo ni shilingi 150,000/ kwa mifumo yote.
 
Na je kama sehemu bado haijapigwa plasta mnatakiwa kupitisha mabomba yenu au mnatumia system gani??
 
Na je tank zenu zinatumika tofauti na tank kama izi za kiboko au simtank?
 
N
Kwa hiyo mkuu nikishalipa gharama kama ulivyoainisha hapo mnakuja lkufunga? Je unaweza kuweka picha aina ya matank mliyo nayo
Ukishalipa unafungiwa mara moja, kama upo maeneo ya Dar Es Salaam ni siku mbili tu tunakufikishia mfumo wako na kuifunga, siku ya kwanza ni kwa ajili ya kufanya site visit.
OKOA.jpg

Tank ni hilo linaloonekana sehemu ya juu.
 
Duh hii safi sana mkuu. Kwa hiyo inabidi kuwe na bomba la kupeleka maji juu huko
 
Na je kama sehemu bado haijapigwa plasta mnatakiwa kupitisha mabomba yenu au mnatumia system gani??
Asante kwa swali zuri, kazi yetu haihusishi kazi ya bomba (plumbering) sisi tunaishia kukuwekea bomba ambalo lita leta (supply) maji ya moto katika miundombinu yako.
 
Duh hii safi sana mkuu. Kwa hiyo inabidi kuwe na bomba la kupeleka maji juu huko
Ndio, inabidi kuwe na mabomba mawili kuelekea juu, moja itabeleka maji ya baridi, na moja itachukuwa maji ya moto kuleta kwenye matumizi ndani ya nyumba yako.
 
Ndio, inabidi kuwe na mabomba mawili kuelekea juu, moja itabeleka maji ya baridi, na moja itachukuwa maji ya moto kuleta kwenye matumizi ndani ya nyumba yako.
Kwa hiyo hapa ilihitaji ushiriki wenu kabla ya kuchimbia mabomba au inakuwaje
 
Ninauliza swali, hivi maji yakikatika kwa siku tatu hivi itakuwaje? Si litaungua maana hakuna maji baridi yanayoingia? Au itabidi kuacha kutumia maji ya moto ili yale yaliyopo yaendelee kulinda tank mpaka ya baridi yatakapokuja. Je mna office zenu Mbeya?
 
nasikia pia mnafunga solar, kwa gharama gani naweza kufungiwa solar ya kuendesha friji, taa, na tv?
 
Kwa hiyo hapa ilihitaji ushiriki wenu kabla ya kuchimbia mabomba au inakuwaje
Hii ni sababu nyingine ya kukufanya utumie mfumo wetu wa kuchemsha maji, mfumo wetu hata kama kukiwa hakuna maji wenyewe hauna wasiwasi ya kuungua, unavumilia katika hali zote na ndio maana tunaku guarantee miaka mitao (5).
Hatuna ofisi Mbeya ila tuna mafundi wa kufunga hii mifumo hapo jijini Mbeya, unaweza kuagizia mfumo na sisi tunakuunganisha na fundi wetu hapo anakuja kukufungia.
 
nasikia pia mnafunga solar, kwa gharama gani naweza kufungiwa solar ya kuendesha friji, taa, na tv?
Ndio tunafunga solar pia, tunatoa huduma za solar za ku pump maji, umeme, taa za barabarani, back up system na kuchemsha maji.
Tutakachohitaji kutoka kwako ni vitu gani unahitaji kuwasha na kwa muda gani ili tuweze kufanya sizing. unaweza kuwasiliana nasi kupitia info@ensol.co.tz. au piga simu 0715049997
 
Back
Top Bottom