Paschal Mayala atoa Ushauri wa bure kwa wana JF

mayala acha unafiki kuna maendeleo gani Tanzania hii zaidi ya taabu na shida mama zetu wanajifungua sakafuni. Kweli hii ni miaka 50 ya uhuni wa viongozi wa serikali.
 
Kuna maeneo tunaonekana tumeenda mbele, lakini tupime gharama ya hapo tulipofikia; je kuna uwiano?. Kama tumeuza madiini yote halafu tunajivunia barabara zitazobomoka baada yamiaka 5, ni sawa? Tumeuza uranium na Kigamboni kwa vyandarua, je huo uwiano ni sawa?. Ukichambua vizuri utagundua kuwa kweli tumesonga mbele lakini in the near future tutaanza kurudi nyuma - hatutakuwa na cha kuuza! Maana yake tumetumia raslimali zetu kuleta maendeleo yasiyo endelevu!
Maeneo mengine tumerdi nyuma kabisa; fikiria kama suala la kujitegemea! Tunajitegemea kwa lipi, tulimuondoa mkoloni ili tujitawale lakini bado tunatawaliwa, je hapo tumesonga mbele?
Kuna wakati (tanzanian industrialization) fulani viwanda vilijengwa ili tujitegemee, Nyerere alisema tusiuze mazao ghafi bali tuyasindike tuuze bidhaa zilizo kamili, Kwa pamba vikajengwa viwanda vya nguo; ili kuimarisha kilimo yakanunuliwa matrekta na kufunguliwa service centers; Kwa ngozi kikajengwa kiwanda cha viatu nk. Unaweza kutaja vingi; na tulipofikia hapo Nyerere akaona kuendelea kununa spea za viwanda hivyo ni ghali, ndipo kikaanzishwa kiwanda mama, Kilimanjaro Machine Tools, ili kizalishe mitambo ya viwanda.
Ndugu zangu vyote hivyo viko wapi sasa? - tuseme tunasonga mbele kweli?
Nina uhakika mtu kama Mkapa Benjamin akitaka kuwa mkweli kabisa, hakika atakuambia tumerudi nyuma.
Hivyo ndugu Mayala tunaposema hakuna maendeleo hatuna maana hakuna kilichofanyika. la hasha bali hapa tulipo sipo tulipotakiwa kuwa ukilinganisha na matumizi ya raslimali zetu na ulilinganisha na hapo ambapo tulishafikia, tukapapoteza.
 
Hivi kama kuna maendeleo tatizo ninin? Si yataonekana. Kama maendeleo yapo mtu hawezi kubisha. Mfano kama tuna ndege mia zinafanya safari zake dunian unaweza sema hakuna ndege siwatu watakuona kichaa. Kama tulianza labda na viwanda viwili sasa vimeongezeka na kuwa mia moja nani atabishana na ukweli kuwa tumeendelea. Kama tulikuwa na mabwawa ya kuzalisha umeme mawili na mpaka sasa yapo yamekarabatiwa hayajachakaa na kushindwa kuzalisha umeme na pia tukawa tumepanua aslimia ya watumia umeme mpaka labda 50% nani atapinga maendeleo ya wazi. Maendeleo sio kitu cha kuangalia kwa darubini maarumu wala huitaji maelezo ya wachumi yapo wazi kabisa. But ukikuta mtu anabishana kwa nguvu akisisitiza maendeleo yapo kana kwamba maendeleo ni kitu abstract ujue kuna tatizo kubwa.
 
Mayala hatupingi kila kitu,ila tujiulize nini maana ya maendeleo?nadhani hili ni tatizo kubwa sana kwa watanzania kujua dhana ya maendeleo,huwezi sema kuwa tumeendelea wakati kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele,ndivyo tunavyozudu kuua viwanda vyetu,taifa haliwezi kusema kuwa limeendelea huku halina uwezo wa kuzalisha bidhaa,taifa linaloagiza kila bidhaa toka nje ni taifa mfu,leo tunaagiza mpaka njiti za kuchokonolea meno,miaka ya 80 tulimudu kutengeneza viatu,mashati,magari pale kiwanda cha kijeshi cha Nyumbu,matairi ya magari(General Tyre),vibiriti,viatu vya raba aina ya bora,kandambili,nyuzi pale tabora,kanga za akina mama,vipuri vya magari!leo viwanda vyote hivi vimekufa,tungesema tumeendelea kama tungekuwa na viwanda zaidi ya hivi na hivi vingeongeza ubora wa bidhaa siyo kuviua na kuanza kuagiza bidhaa nje,taifa lililoendelea na linaloingia katika kundi la nchi za ulimwengu wa kwanza ni taifa lenye viwanda!sasa mayala anapodai umeendelea anaegeme upande gani?barabara tunazotambia,kuanzia mchakato,pesa,wataalamu na hata malighafi isipokuwa mchanga vimetoka kwa wafadhirim,leo mtanzania mpaka chupi anaagiza,sasa pasco anatudanganya nini?
 
Akiwa kwenye kipindi chake cha PPRA alikuwa akimhoji bwana Utoh wa ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za serikali.
Utoh kama nilivyotegemea kuwa anatetea mkate usiingie matope akaanza mapambio ya sifa za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akataja idadi ya vyuo vikuu na kilometa za lami zilizoongezeka.
Mayala akatoa wito kwa wanasiasa na wanahababi kuwa wasipinge kila kitu. Baadae kwa msisitizo na kwa umakini akasema, 'nawashauri nduguzangu na member wenzangu wa JF, tuwe wakweli mioyoni mwetu. Serikali imefanya mengi sio tupinge kila kitu. Tukubali tu kuwa tuna maendeleo'
Mkuu Mzito Kabwela, japo hili ni bandiko la zamani, lakini kuna baadhi ya hoja za msingi na za ukweli humu nitazitafutia muda nizijibu.
Msalimie Mkuu TTOZI BWEKA
P
 
Mkuu Mzito Kabwela, japo hili ni bandiko la zamani, lakini kuna baadhi ya hoja za msingi na za ukweli humu nitazitafutia muda nizijibu.
Msalimie Mkuu TTOZI BWEKA
P
Usisahau na hili tunakumbushana tu.
Matokeo shuleni: A - Vizuri sana, B - Vizuri, C - Wastani, D - Dhaifu, F - Fail
 
Back
Top Bottom