Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Nimesikitishwa sana na marekebisho katika Sheria ya fedha ya Serikalikali za mitaa sura 290 yaliyoletwa na Serikali Jana Bungeni na kupitishwa kishabiki na Wabunge wa C.C.M.Marekebisho ya sheria hii yanalenga kuwatoza kodi Wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi mfano mama lishe,wauzaji wa mitumba wadogo,wauza mazao ya Kilimo wadogo kama mboga mboga,ndizi,matunda nakadhalika.Wabunge wa UKAWA tulitimiza wajibu wetu wa kuwatetea Watanzania lakini uchache wetu ndani ya Bunge ukatuponza na hatimaye Wabunge wa C.C.M wakapitisha.Watanzania wenzangu Bajeti ya 2017/2018 ni hatari kwa Watanzania masikini kwa kuwa pia kuhamishia ada ya mwaka ya leseni ya Magari kwenye mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa kutaongeza ugumu wa Maisha Mara dufu ukilinganisha na hali ya sasa.