Paschal Haonga: Wabunge wa CCM wapitisha kishabiki marekebisho katika sheria ya fedha

Mhere Mwita

Verified Member
Jan 24, 2012
235
1,000
Nimesikitishwa sana na marekebisho katika Sheria ya fedha ya Serikalikali za mitaa sura 290 yaliyoletwa na Serikali Jana Bungeni na kupitishwa kishabiki na Wabunge wa C.C.M.Marekebisho ya sheria hii yanalenga kuwatoza kodi Wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi mfano mama lishe,wauzaji wa mitumba wadogo,wauza mazao ya Kilimo wadogo kama mboga mboga,ndizi,matunda nakadhalika.Wabunge wa UKAWA tulitimiza wajibu wetu wa kuwatetea Watanzania lakini uchache wetu ndani ya Bunge ukatuponza na hatimaye Wabunge wa C.C.M wakapitisha.Watanzania wenzangu Bajeti ya 2017/2018 ni hatari kwa Watanzania masikini kwa kuwa pia kuhamishia ada ya mwaka ya leseni ya Magari kwenye mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa kutaongeza ugumu wa Maisha Mara dufu ukilinganisha na hali ya sasa.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,283
2,000
Hoja inaweza kuwa nzuri lakini uandishi wako haujaitendea haki hoja yako. Uwasilishaji mbovu.
 
Transcend

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
20,278
2,000
More loads

Add more loads...

Load them...

Yaani hizi kodi zitauwa watu..
 
ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
2,058
2,000
Nafikiri bado haitoshi,ccm ilipaswa ianzishe hata kodi ya kulipia pumzi,kwamba kila unapopumua unalipia,labda ingesaidia kuwaamsha watanzania kutoka kwenye usingizi wa pono waliolala.

Mtanzania ni kiumbe wa ajabu sana kuwahi kutokea kwenye "planet earth", ni mtanzania pekee awezaye kubebeshwa Mzigo mzito wa kodi tena usioendana na mrejesho wa huduma za jamii anazopatiwa,lakini baadae anarubuniwa kwa kupewa kofia,kanga,tisheti na sinia la ubwabwa,huku akitumbuizwa na kibwagizo cha " acha waisome namba" na akaichagua tena ccm!

Sitaki kuuamini sana utafiti wa TWAWEZA uliotuambia kuwa ccm inakubalika zaidi miongoni mwa watu duni,wasio na Elimu na aina zote za makinikia ya Lumumba,lakini kwa namna "wehu"walivyojitokeza kusifia na kupongeza ripoti za makinikia huku wakiisifu ccm ambayo ndiyo iliyotia saini uzalishaji wa takataka ziitwazo makinikia ambazo tunaombwa sote tuungane kuzipigania,nalazimika kuyaamini matokeo ya utafiti huo.
 
Bekabundime

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
2,004
2,000
Nimesikitishwa sana na marekebisho katika Sheria ya fedha ya Serikalikali za mitaa sura 290 yaliyoletwa na Serikali Jana Bungeni na kupitishwa kishabiki na Wabunge wa C.C.M.Marekebisho ya sheria hii yanalenga kuwatoza kodi Wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi mfano mama lishe,wauzaji wa mitumba wadogo,wauza mazao ya Kilimo wadogo kama mboga mboga,ndizi,matunda nakadhalika.Wabunge wa UKAWA tulitimiza wajibu wetu wa kuwatetea Watanzania lakini uchache wetu ndani ya Bunge ukatuponza na hatimaye Wabunge wa C.C.M wakapitisha.Watanzania wenzangu Bajeti ya 2017/2018 ni hatari kwa Watanzania masikini kwa kuwa pia kuhamishia ada ya mwaka ya leseni ya Magari kwenye mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa kutaongeza ugumu wa Maisha Mara dufu ukilinganisha na hali ya sasa.
Serikali yangu ni ya wanyonge,sitakubali mama Ntilie asumbuliwe na askari wa jiji wala kulipishwa kodi za kijinga,Serikali yangu mgambo wa jiji watafute kazi.
 
Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,585
2,000
Kwani yale ma 108trl ya ACACIA yanaenda wapi?

Acha waweke hadi kodi za macho ukiangalia unatoswa ushuru hadi akili iwakae sawa sawa hawa raia huku mitaani...
 
singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
4,368
2,000
Na miaka sijatumia mafuta ya taa acha wakazwe mpaka tukiimba wimbo tunaimba wimbo mmoja.
 
balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,574
2,000
The Govt corrupt hukusanya kodi kwa wachuuzi na wanyonge huku minara ya diamond ikiondoka freely in JKN voice sasa!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom