Pascally Mayega ndani ya kashfa nzito ya wizi wa kazi ya fasihi na kuiuza Kenya

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
3,465
2,000
Mwandishi wa habari nchini hasa habari za makala za kisiasa nchini kupitia magazeti ya Tanzania Daima na Jamhuri aliyejulikana kwa jina Pascally Mayega almaarufu kwa jina Mwalimu Mkuu wa Walimu nchini Tanzania amejikuta kwenye kashifa nzito ya wizi wa kuuza kazi au vitabu vya marehemu ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi paspo idhini ya familia.

Wakiongea kwa Mwandishi maalumu ndugu wa Mwandishi wa vitabu hivyo ambaye kwa sasa ni marehemu walidai kuwa ndugu yao aliyekuwa ni mtunzi wa vitabu mbalimbali vya Riwaya nchini Tanzania aliaga Dunia takribani miaka kumi na tisa iliyopita.

Wamemtaja mtunzi huyo ambae aliaga Dunia mwaka 2004 kwa Jina la Thomasi Kamugisha, wamedai kuwa ndugu yao alipoaga dunia baada ya kumaliza msiba wamfata ndugu Pascally Mayega kwa lengo la kutaka kujua kama alikuwa na mikataba yoyote na marehemu ndugu yao lakini bwana Pascally Mayega aliwafukuza kwa kuwatishia kuwakata mapanga.

Moja ya kitabu ambacho kinaonekana kuchapishwa BILA IDHINI YA FAMILIA NI RIWAYA YA KITU KIDOGO ilichapishwa MWAKA 2011, na kampuni ya SASA SEMA, chini ya longhorn publisher ya Kenya baada ya kuingia mkataba na kampuni hewa inayomilikiwa na Pascally Mayega inayojulikana kwa jina la MPB ENTERPRISES yenye makao makuu yake karbu na St. Mary's ya Mbagala.

Katika hali hisiyo ya kawaida kitabu hicho kilichapishwa nchini kenya na inasaidikiwa kuwa kiliuzwa Afrika Mashariki.

Wakizungumza kwa uzuni Mjane wa marehemu aliyeachiwa watoto watatu,amemlalamikia Bwana Pascally Mayega kwani alimfata mara nyingi ili ampe walau pesa ya kujikimu lakini aliishia kupewa vitisho.

"Mimi ni mjane,mme wangu alinichia watoto watatu, baada ya kifo cha mme wangu niliamua kufatilia hati miliki za baadhi ya vitabu vya mme wangu kwa huyu bwana ambae ni mkosoaji mkuu wa serikali zote zilizopita kwa kutaja makosa ya wenzake ili hali na yeye ni tapeli mkubwa lakini hakuniskiliza sasa nimepanga kwenda wizara ya Michezo,tamaduni na sanaa kutafta haki zangu swezi kubali mme wangu amelala kaburini huku wajanja wakiuza mawazo yake na kupata nguvu za kuisema serikali ili hali na wao ni majizi makubwa"

Nje ya riwaya ya Kitu kidgo vitabu vingine ambavyo vimetajwa kuwa Marehem Thomasi Kamugisha aliacha amevitunga ni kitu kidogo, harusi ya mwenda wazimu, safari ya mwalimu katoto, na sokoni Kariakoo.

Mwandishi wa habari hii aliwasiliana na ndugu Pascally Mayega dhidi ya kashifa hii nzito hakutoa ushirikiano mpka tunaenda studio zetu.
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
9,715
2,000
kuna watu wengi wana sifa kwa jamii lakini ukiwachunguza kwa undani wameoza ukweli utajulikana kama kweli ameuza kazi za mwenzake au zilikuwa kazi zake halali
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,851
2,000
Kidogo nidhani labda ni paschal mayala umetype vibaya kumbe ni paschal mwingine tofauti kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom