Pascal Mayalla: Waandishi wa habari ni waoga nimewaalika tujadili hotuba ya Rais Magufuli wamepiga chenga na kuingia mitini

Kwa sisi Wakristo, kila jambo analofanya mtu ni kwa sifa na utukufu wa Mungu.
Mungu haruhusu mtu kufanya kazi nzuri kwa watu kwa sifa na utukufu wake.
Mh. Rais wetu ni mcha Mungu ndiyo maana ameruhusu mikusanyiko ya kumwabudu Mungu.
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yeye mwenyewe anafanya kazi kwa sifa na utukufu wa Mungu na anamsifu Mungu.
Viongozi ambao hawatambui falsafa hii ya kiroho, badala ya kumpa sifa Mungu kwa kutupatia kiongozi shupavu, wanampa sifa Mh. Rais bila kukiri uwepo wa Mungu.
Hahahah daah hiiìiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Pascal anasema kwa mfumo wa katiba ya Tanzania Rais ndio mwenye maamuzi ya mwisho na tamko lake ni sheria tofauti na nchi kama Marekani ndio maana anateua Jaji mkuu na Katibu wa bunge.
Paskal na wako watanzania wengi wana amini hivyo- na hapa ndio penye upotoshaji mkubwa kwani tuna ambiwa "hakuna mtu aliyepo juu ya sheria". Ukiamini alichosema Paskal basi utaona hakuna la ajabu waandishi kuingia mitini, lakini ukweli wa mambo tunaongozwa na katiba na sheria navyo havisemi hicho alichosema Pascal. Tunashindwa kuwa na institutions imara matokeo yake ndiyo hayo. Cha ajabu Pascal ni mwanasheria na anataka sisi tuamini hivyo.
Pascal anasema Ummy Mwalimu ni waziri wa kupigiwa mfano kwa sababu madaktari bingwa watano waliokuwa wasaidizi akiwemo Naibu waziri wa afya wametumbuliwa lakini yeye pekee ambaye siyo daktari kitaaluma ndio amebakia.
Pascal hapa ametufahamisha vizuri cha yaliyotokea. Sasa ukitaka kulijadili hili lazima ujiulize kwa nini professionals watano wa vyeo vya juu kabisa serikalini watumbuliwe. Kwangu binafsi inaashiria kutokubaliana na matakwa ya wakubwa. Na wao ndiyo yamewakuta kwa mfano ni vigumu kwa professionals kukubali data ziminywe, wakati wakubwa hawataki data itolewe. Hapo basi.......
 
Kwani ni lazima kualika waandishi wa habari wanaoishi Tanzania pekee? Ungeweza hata kualika waandishi wa kigeni wenye uelewa wa mambo ya Tanzania au hata waandishi wa Kitanzania wanaoishi nje ya Tanzania. Pia ungeweza hata kutoa nafasi kwa watanzania wa diaspora ambao wangeweza kuchangia mada vizuri kabisa, kuna huduma za Skype, Zoom au hata Google Meet ambapo ungeweza kuunganisha watu LIVE.
 
Out of mada
Hivi mkono wa kushoto Pascal Mayalla umamatatizo. Tangu nimeanza kumfuatilia huwa nauona haupo active.
Hata hapa muda huu nauona hivyo.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
😂

Wabongo bhana, watoto shule mwl Wao akiwa anaulemavu, akiri Yao hushika zaidi muonekano wa mwl Wao kuliko kile anachofundisha, na wewe uko vilevile ka mtoto wa chekechea

Pumbavu wewe
 
Mjadala wa leo katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari kinachorushwa mubashara na Star tv mada ni Hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa anawaapisha wateule wake.

Pascal Mayalla anasema aliwaalika waandishi wa habari katika mjadala lakini wote wameingia mitini.
Pascal anadai waandishi wetu ni wajanja wajanja kwenye mitandao tu lakini inapofika kwenye mijadala huru ni kunguru na waoga kupitiliza, wanafunga plasta midomoni.

Pascal anasema kwa mfumo wa katiba ya Tanzania Rais ndio mwenye maamuzi ya mwisho na tamko lake ni sheria tofauti na nchi kama Marekani ndio maana anateua Jaji mkuu na Katibu wa bunge.

Pascal anasisitiza kuwa Rais Magufuli ni mtu mwenye maamuzi sahihi yaani yeye ni master diplomat ndio maana Rais Trump wa USA sasa anaiga kutoka Tanzania ikiwemo kufungulia makanisa.

Kadhalika majirani zetu wamejifunza kutoka kwetu na sasa wamefungua mipaka tena kwa kufuata masharti yetu kwamba madereva wetu watapimwa hapa nchini.

Pascal anasema Ummy Mwalimu ni waziri wa kupigiwa mfano kwa sababu madaktari bingwa watano waliokuwa wasaidizi akiwemo Naibu waziri wa afya wametumbuliwa lakini yeye pekee ambaye siyo daktari kitaaluma ndio amebakia.

Pascal anasema waziri Ummy anafuata zaidi uhalisia kuliko matakwa ya kitaaluma ndio maana amekuwa akieleweka zaidi kwa Rais Magufuli.

Mjadala umemalizika, shukrani Dotto Bulendu kwa kazi nzuri ya kuongoza kipindi.

Kipindi kiko hewani, karibu.

Maendeleo hayana vyama!
Wanamjua sana kuwa ni mnafiki
 
Athari za huu ugonjwa unazijua? Unajua unavyomkaba mgonjwa mpaka anashindwa kupumua. Kwa nini useme serikali inafanya maigizo?
Chagu , nilidhani ktk hili la ugonjwa utauacha unafki , Lakini daahh !!. Hivi unaamini virusi vimepungua ?! Vimepungua Je wakati hata kuongelea Corona machoni pa mtawala ni hatia !!.

Chagu , maabara yetu wenyewe tumeifanya kama ya wengine ?!

Chagu, ukitaka kujua virusi havijapungua ni kisa cha madereva wetu ktk nchi za jirani .

Odhis *
 
Jaduong kwanza naomba utambue huu ugonjwa ni hatari. Mtu kama ana Covid-19 anaweza akaendesha gari kilomita mia? Maana huu ugonjwa unashambulia mfumo wa kupumua. Kwenye ishu ya madereva kulikuwa na mchezo mchafu. Jana kuna masuala yamewekwa sawa.
 
Huu ugonjwa umemchukuwa jirani yangu mwema naujua vizuri. Lakini hatukutakiwa kuukrashi taratibu za kitaalamu (WHO). Kusema mawazo ya kitaalamu ni ya mabeberu is not right.

Odhis *
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom