Pascal Mayalla: Waandishi wa habari ni waoga nimewaalika tujadili hotuba ya Rais Magufuli wamepiga chenga na kuingia mitini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Mjadala wa leo katika kipindi cha Jicho letu ndani ya habari kinachorushwa mubashara na Star tv mada ni Hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa anawaapisha wateule wake.

Pascal Mayalla anasema aliwaalika waandishi wa habari katika mjadala lakini wote wameingia mitini.

Pascal anadai waandishi wetu ni wajanja wajanja kwenye mitandao tu lakini inapofika kwenye mijadala huru ni kunguru na waoga kupitiliza, wanafunga plasta midomoni.

Pascal anasema kwa mfumo wa katiba ya Tanzania Rais ndio mwenye maamuzi ya mwisho na tamko lake ni sheria tofauti na nchi kama Marekani ndio maana anateua Jaji mkuu na Katibu wa bunge.

Pascal anasisitiza kuwa Rais Magufuli ni mtu mwenye maamuzi sahihi yaani yeye ni master diplomat ndio maana Rais Trump wa USA sasa anaiga kutoka Tanzania ikiwemo kufungulia makanisa.

Kadhalika majirani zetu wamejifunza kutoka kwetu na sasa wamefungua mipaka tena kwa kufuata masharti yetu kwamba madereva wetu watapimwa hapa nchini.

Pascal anasema Ummy Mwalimu ni waziri wa kupigiwa mfano kwa sababu madaktari bingwa watano waliokuwa wasaidizi akiwemo Naibu waziri wa afya wametumbuliwa lakini yeye pekee ambaye siyo daktari kitaaluma ndio amebakia.

Pascal anasema waziri Ummy anafuata zaidi uhalisia kuliko matakwa ya kitaaluma ndio maana amekuwa akieleweka zaidi kwa Rais Magufuli.

Mjadala umemalizika, shukrani Dotto Bulendu kwa kazi nzuri ya kuongoza kipindi.

Kipindi kiko hewani, karibu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Bora waingie mitini kuliko kwenda kusifia wasicho kuamini, wewe unafikiri wagonjwa wamepungua hospital bila kujuwa hali ya majumbani ukoje, ni sawa? Hatujui maabara inafanya kazi au bado inachekechwa, takwimu hamna mnajadili nini?

Waache wenzio usiwatie majaribuni, wengine hawawezi kujizuia kama wewe!
 
Back
Top Bottom