Pascal Mayalla niwie radhi ila nikuulize swali, unajua kuwa Ben Saanane tulikuwa naye humu tukijadiliana?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,879
Kwenye uzi huu

Uchaguzi 2020 - RC wa Mwanza, John Mongela avunja Mwiko wa Kampeni Kwa Kuongea Ukweli Bayana!, "Tukimpa Mitano Tena, JPM Kuigeuza Tanzania Nchi ya Maziwa na Asali"

jana nilikuwa member wa kwanza kuchangia na kwakweli nilikerwa na uzi wa ndugu yetu Pasco. Nilikerwa kwakuwa ni yule muumini wa "Hayajatokea kwangu na familia yangu hivyo hayanihusu"

Niwie radhi maana nilikuporomoshea mzigo mpaka mods wakaamua kuufuta, aidha niombe radhi kwa wote niliowakwaza!

Nina swali moja tuu kwa Pasco, nimeamua kuacha mengine lukuki najua anayajua.

Je, Pasco hujui kuwa Ben Saanane tulikuwa naye humu tukijadiliana? Nani wa kupaswa kuulizwa alipo Ben? Nani tuliyemkabidhi ulinzi na usalama wa watanzania wote? Kwanini hajali kuhusu Ben? Je, Kazi zake zina baraka kutoka kwa nani hadi hiyo Ulaya ije Tanzania?

NB: Hilo ni swali moja tu! Yapo mengi nimeyaacha na unayajua.

Ipo methali moja inasema "Mchuma janga hula na wakwao"
Usije ukajiaminisha kuwa wewe siyo "Wakwao" ukifikiria hivyo basi unafanya kosa kubwa kabisa!

Kumpa Magufuli miaka mingine mitano ni kuchuma janga! Tukubaliane kwa lugha ya kawaida kabisa kuwa Rais wetu amepungukiwa kiasi kikubwa mno cha ubinadamu! Huo ni ukweli! Tusiupinge kwa kuangalia ubinafsi wetu kwa muda huu! Tuangalie jamii nzima kwa miaka mitano ijayo!

Ndugu yangu Pascal Mayalla, nakusihi jikalie kimya tu kama walivyoamua kina barafu na Mzee Mwanakijiji. Hawa wameamua kuona aibu baada ya kutokujua uhalisia hapo kabla. Kumnadi Magufuli ni kukosa hofu ya Mungu! Usiruhusu hilo likatokea kwako!
 
Pasco kwa sasa hastahili attention mnayompa. Msome tu kawaida kama unavyowasoma buku 7 wengine. Huyu ni mtu aliyechagua upande wa waonevu kwa ajili ya tumbo lake. Wewe uliyechagua upande wa wanaoonewa Mungu atakubariki
 
Wewe na Chadema tokea Ben Saanane ametoweka mmechukua hatua gani kuhakikisha anarudishwa na hao mnaosema wamemteka? Mmeenda mahakamani? Mmeenda ofisi za Un? Au mnabaki kulalamika na kuwatusi watu kama akina Pasco.
 
Nyerere alisema simpendi Idd Amin kwasababu Idd Amin ni MUUAJI. Mtawala wetu ni MUUAJI. Pascal , niwie radhi sana, ukipata upenyo utakuwa KATILI wa kutisha! Kama huoni kuwa Watanzania wameteseka miaka 5, basi kuna something wrong in your head! Nimesoma mabandiko yake unaona kabisa kuwa huyu mtu bado hajapata mwanya, akiupata, siyo mtu kabisa! Pascal Mayalla
 
Nyie mnawataja kina Ben, Anzroy, Lwabeja(?) n.k sababu ni watu maarufu.

Ukweli ndani ya hii miaka mitano watu wengi wameumizwa vibaya mno, kuna waliofilisiwa, waliotekwa, waliopotea ama kufa kitatanishi, wengine walihasiwa, wengine wanaishi uhamishoni lkn kwa kuwa siyo maarufu hawazungumzwi kama hao wahanga wengine.

Tumwombe Mungu atamatishe ukatili uliotamalaki Tanzania.
 
Jambo la ajabu hao watu waliobomolewa nyumba zao ndo utawakuta wanacheza midondiko na sebene wakimsifia huyo kiongozi mkuu aliye wakana kuwa wao si wapiga kura wake. Kule kwa huyo kiongozi alisema wasibomolewe nyumba kwani wao ndo waliompigia kura. Oct 28 mkafanye kweli kwenye sanduku la kura ili kuondoa huu utawala.
 
Jambo la ajabu hao watu waliobomolewa nyumba zao ndo utawakuta wanacheza midondiko na sebene wakimsifia huyo kiongozi mkuu aliye wakana kuwa wao si wapiga kura wake. Kule kwa huyo kiongozi alisema wasibomolewe nyumba kwa wao ndo waliompigia kura. Oct 28 mkafanye kweli kwenye sanduku la kura ili kuondoa huu utawala.
Huyo naye ni victim anayejikaza kisabuni, Hana namna as long as homeboy ndiye anayemuwezesha kuprinti sinki.
 
Unataka kusema mtu anafanya biashara halali anakamatwa na kufirisiwa bila sababu? Au unatetea wahujumu uchumi waliokuwa wanatengeneza bidhaa bila kulipa kodi,wakwepa kodi wabadhirifu wa mali ya umma?

Hao walio uwawa bila kuwa na hatia kwa nini ndugu zao wasichukue hatua stahiki?
 
Ukitaka kumpiga mbwa mpe jina baya ili kuepuka kuumizwa na dhamiri itakayokusuta(wahujumu uchumi).

Hii nchi imekuwa ya ahadi, ya maziwa na asali kwa badhi na kwa wengine imekuwa kama kambi ya Sobibo.

Mkuu kama hayajakukuta mshukuru Mungu huku ukitambua maisha ni kama siku, yana saa za mwanga na saa za giza.
 
Mayala kikwetu ni njaa,
Huyu jamaa mwanzo nilikuwa naona kuwa ni mtu anayejitambua kwa kiasi fulani kumbe sikujua kuwa ni moja ya watu ambao sipaswi hata kusoma mabandiko yake maana ningeambukizwa ukatili.
Mimi huyu jamaa kumjadili naona kama ni kupoteza muda na kujaza servr za JF huyu ni wa kupuuzwa tu.
Hakuna mtu mwenye akili timamu asiyeona mateso wanayopitia wananchi wa nchi hii.
 
K

Unataka kusema mtu anafanya biashara halali anakamatwa na kufirisiwa bila sababu? Au unatetea wahujumu uchumi waliokuwa wanatengeneza bidhaa bila kulipa kodi,wakwepa kodi wabadhirifu wa mali ya umma?

Hao walio uwawa bila kuwa na hatia kwa nini ndugu zao wasichukue hatua stahiki?
Kuna watu ukisoma wanacho andika unajiuliza ni binadamu hawa? Au ni manyani? au ni wake zake shetani?
Wewe chagu wa malunde ni nani kati ya hao niliotaja?
 
Back
Top Bottom