Pascal Mayalla na Jacton Manyerere wakubaliana na Spika Ndugai kwa uamuzi wa kumrejesha Mwambe na wabunge 4 waliofukuzwa CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,763
Wakuu Dotto Bulendu, Pascal Mayalla na Jackton Manyerere wako mubashara Star tv wakijadili uhalali wa Spika Ndugai kumrejesha bungeni Cecil Mwambe na kuwabakiza bungeni Selasini, Silinde, Komu na Lwakatare.

Pascal anasisitiza kuwa Spika ana nguvu za " ziada" katika kufikia maamuzi fulani kama ilivyo kwa Rais na Jaji mkuu na kwa kutumia nguvu hizo maamuzi ya Spika Ndugai ni halali kabisa.

Jackton Manyerere anakubaliana na Pascal katika hili.

Pascal anasema kuna madai mitandaoni kuwa kwa sababu Spika na naibu wake ni wana CCM wamekuwa na kuwaida ya kuwapendelea wabunge wa chama chao ndio sababu Lisu na Nassari walifukuzwa lakini Muhongo na Mkono bado wanadunda japo hawapo bungeni.

Manyerere ambaye anatoka jimboni kwa Mkono amesema mbunge wake ni mgonjwa kwa takribani miaka mitano sasa na amewataka watu waache kumsema sema vibaya kwani siyo utamaduni wa kitanzania kuwateta wagonjwa.

Wanamjadala kwa pamoja wanasema ni vema sasa Tanzania ikawa na wagombea binafsi kwa sababu hii hama hama haina tija ni sawa tu na Uhujumu uchumi.

Mjadala umemalizika, nawashukuruni sana Dotto Bulendu na Pascal Mayalla kwa mjadala huu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hapo mwenye impact ni Dotto Bulendu tu hao wengine waimba mapambio
Wakuu Dotto Bulendu, Pascal Mayalla na Jackton Manyerere wako mubashara Star tv wakijadili uhalali wa Spika Ndugai kumrejesha bungeni Cecil Mwambe na kuwabakiza bungeni Selasini, Silinde, Komu na Lwakatare.

Pascal anasisitiza kuwa Spika ana nguvu za " ziada" katika kufikia maamuzi fulani kama ilivyo kwa Rais na Jaji mkuu na kwa kutumia nguvu hizo maamuzi ya Spika Ndugai ni halali kabisa.
Jackton Manyerere anakubaliana na Pascal katika hili.

Mjadala unaendelea, karibu.

Maendeleo hayana vyama!

In God we Trust
 
Back
Top Bottom