Pascal Mayalla Mzee wa makala za "Kwa maslahi ya Taifa", mbona uko kimya bei ya sembe imefika 1,800/- kwa kilo

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,820
Pascal Mayalla nakusalimu.

Nimekuwa msomaji na mfuatiliaji mzuri sana wa makala zako ulizozibandika jina la "Kwa Maslahi ya Taifa".

Kupitia makala hizi nimekuwa nikijifunza vitu mbalimbali na bingo sana.

Kikubwa zaidi nilichojifunza, hizi makala zipo kwa ajili ya kuwaponda wapinzani na kuwasifia watawala.

Yakija mambo halisi yanayogusa maisha ya watu, msukuma wewe umekuwa ukijiweka kando.

Kupanda kwa bei ya mafuta ya kula, unga, mchele na mahitaji mbalimbali kwako inaonekana kama sio maslahi kwa taifa.

Kwako taifa ni wakubwa walioshika nafasi za uteuzi na sio hawa watu zaidi ya million 60 wanaotaabika na ugumu wa maisha, ukosefu wa ajira, maji safi na salama na huduma za kiafya.

Tunaomba uchepushe jicho lako, litoke kwenye siasa na lilenge kuripoti kero zinazoiathiri jamii.
 
Sasa hivi ana contract mbili zinazomuingizia mahela kibao,ya kwanzani ya kuwatetea wale vicheche 19, na ya pili ni kumsagia kunguni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ili afukuzwe kazi.

Hii ya kwanza analipwa na Yule Bikidude kiranja wa wale 19 na ya pili analipwa toka makao makuu ya CCM.
 
Kazi yake Pascal ni Mwandishi ,ulitegemea awe anaandika nini kwa mustakabali wa kazi Yake na familia yake ?
 
Back
Top Bottom