Pascal Mayalla: JamiiForums ndio mtandao bora kwenye utoaji elimu japokuwa wengine waliomba corona ije kupitia hukohuko

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,667
Mwandishi wa habari nguli na mwanasheria Pascal Mayalla amesema mtandao wa JamiiForums ndiyo bora katika utoaji elimu pamoja na kwamba kuna baadhi ya members waliomba Corona ije nchini.

Mayalla alikuwa anaongea katika kipindi cha Jicho Letu ndani ya habari kinachorushwa mubashara na Star TV.

Pascal amewataka wananchi wawe wanakosoa mabaya ya serikali lakini wasisahau kupongeza kwa yale mazuri kwani Biblia inatuasa tushukuru kwa kila jambo.

Source: Star TV
 
Corona inakuja kwa kuombwa?

Ukimwi uja kwa kuombwa au kufanya ngono? malaria uja kwa kuombwa au kulala bila net?

Ushindwe kubana wanaoingia nchini, kuwapima kwa umakini na kuwatenga kwa muda kabla wachanganyikana na watanzania

usingizie corona imeletwa na walio-iomba? tungekuwa na uwezo wa kuomba mambo yakatokea basi Pascal angekuwa ashapata uteuzi.
 
CORONA ISIJE [JAPO IPO KISIASA] LAKINI WAFUATAO WASIPATE.

1. MECO
2. DR CHANGAMKA ATISON
3. JUBU NDUGU-AI
4. AMFU SLOW SLOW.
5. WASIO-JULIKANA
6. Umi-Ticha

ila ikitokea wakapata cornoa, hakika serikali itakuwa serious kufunga mipaka, na pia iyakuwa serious kutoa takwimu.
MWANA FA , ISABELA wametumiwa na lumumba kuhadaa dunia kuwa wana corona na wamepona ilhali si kweli, hakuna aliyekuwa nayo ila ni mbinu chafu za MECCO, kwanza kupunguza trending stories za kina mbowe, bulaya na mdee kuhusu kupigwa na maaskari wa kiume kule segerea , lakini pia ni mbinu inayotumika kupeleka mbele uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo kabla ya mechi JIWE ameshindwa , na anajua hgivyo ndio mana alimkata Membe na wengine anao wahisi anawapa ubalozi ili wasije kabisa nchini
 
Jo ni ngumu kuwazuia watu kusema mawazo yao, kusema hisia zao.

Kwa hali tuliyo nayo watu hufurahia yatupate mabaya kuliko mema. Badala ya kuwalaumu tunatakiwa tujitafakari ni wapi tumepotoka na kukosea.

Hisia za watu ni sawa na maji, HAYAZUILIKI na ukijaribu kufanya hivyo yatatafuta yenyewe pa kutokea.

Jr
 
Jo ni ngumu kuwazuia watu kusema mawazo yao... Kusema hisia zao.. Kwa hali tuliyo nayo watu hufurahia yatupate mabaya kuliko mema.. Badala ya kuwalaumu tunatakiwa tujitafakari ni wapi tumepotoka na kukosea
Hisia za watu ni sawa na maji.. HAYAZUILIKI na ukijaribu kufanya hivyo yatatafuta yenyewe pa kutokea

Jr
Bwashee katika janga hili " mitishamba" ina msaada gani?....... Hii ni vita kamanda!
 
Kuna jamaa wa dit aliiomba corona ikaja bwashee!
Ndani ya JF kuna watu wa kila aina na kila hulka. Unaweza kukuta aliyesema Corona ije hana hata cheo cha Mwenyekiti wa tawi.

Lakini kuna Chama msemaji wake wa ngazi ya Taifa, yaani ngazi ya juu kabisa nchini kasema washindani wake ni CORONA, lakini kwa matamshi hayo sijamsikia huyu Mwandishi nguli kama mnavyopenda kumuita akikemea kitendo ambacho kinatushawishi sisi wa kima cha chini tuamini kuwa anaunga mkono kauli hiyo na ndo maana akasema CORONA itumike kama fursa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom