Pascal Mayalla ataka wataalamu wa Kemia waje watueleze sintofahamu ya Fumigation na Barakoa baada ya kutafakari hotuba ya Rais Magufuli

Nasikia leo umempongeza Jiwe mpaka kinyaa. Nasikia umekubali kujifukiza, na kila kitu. We jaribu ndugu yangu unaweza kuambulia maana jamaa anataka kusifiwa/kuabudiwa na kale ka Jina ketu ka kisukuma anaweza akasikia....
Bravo!
 
Nasikia hapo Ufipa nafasi za kugombea ubunge zimejaa!
johnthebaptist mimi nakuamini kwa kiasi fulani hapo Lumumba. Mimi sina unasaba na CDM! Ila kwa ukatili wa jiwe, kuminya uhuru wa watu, kupoteza watu, kufunga watu, persecutions etc ndiyo inayonifanya niichukie CCM.
CCM ikiacha "mauji" ikawa na policy nzuri, (kitu ambacho hakiwezekani) nitabadilisha msimamo
CDM naona kama mkombozi/msemaji wa wanyonge! Lazima niwaunge mkono!
 
Huenda wanaitwa wanakataa kwa hofu kwamba kauli ishatoka ya kwamba fumigation haiui virusim. Mtaalamu atakuwa na uthubutu kusema kinyume na kauli hiyo? Ni akina Mayala tu home boys ndo wanaweza
 
Mwandishi wa habari nguli mh Pascal Mayalla amewataka wataalamu wa Kemia kuja hadharani na kutuchambulia faida na hasara za kupiga fumigation mitaani na kwenye vyombo vya usafiri kama kuna tija kwenye mapambano dhidi ya Corona.

Kadhari watuelimishe juu ya ubora wa barakoa kama zinaweza kuttumika kuihujumu nchi kwa kuletwa zikiwa na vimelea vya Corona.

Pascal na Dotto Bulendu wamesisitiza kuwa huu sio wakati wa kuwaachia waandishi wa habari waliosoma HGL na HGK pekee kuripoti habari za Corona bali wanahitajika wabobezi wa maswala ya afya katika kulihabarisha taifa.

Chanzo: Star tv
Baada ya corona kuisha mara paaaa! Inashuka sauti kutoka mbinguni ikisema ;"""haya nimeshachukua watu wangu na kuwapeleka mbinguni nyie mliobaki subirini moto wa milele""" Aloo! apo ndo utajuta kwanini ulikua unavaa barakoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo hatuheshimiani kwa taaluma, hao unaowaita wandishi wa habari wapo kwenye vyombo vya kueneza habari... lakini cha ajabu hawajisumbui kuwahoji wataalamu.

Kila saa mahojiano na wasanii, eti watu maarufu... ona hadi matangazo ya kuelimisha watu kuhusu kujihadhari na Corona wapo Snura na Sholo Mwamba sijui Gigi Money 🤷🏾‍♂️

Hao wataalamu watasikika kupitia wapi.?

Huyo Pascal Mayalla atuambie ni lini amealika na kuhoji Wakemia kwenye vipindi vyake.
Umemsahau mrisho mpoto
 
Back
Top Bottom