Pascal Mayalla apata ajali.....

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,942
4,413
Mdau Mpoki Bukuku wa Mwananchi na The Citizen anatujulisha kwamba Mwandishi wa siku nyingi na mtangazaji ambaye pia ni mjasiliamali ndugu yetu Pascal Mayalla amepata ajali mbaya ya pikipiki yake alipokuwa akisafiri kwenda mkoani Mkoani Dodoma.

Bw Pascal Mayalla amepata majereha sehemu mbalimbali za mwili ikiwa namkono ambao umepoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili.JF hii inapenda kumpa pole ndugu yetu paschal Mayalla,apate Nafuu ya haraka.

1.JPG

2.jpg
 
Nakumbuka haijapita wiki tangu ile thread ya Pascal kuhusu kuendesha pikipiki isiyo na namba ijadiliwe hapahapa. Na wengi tulipendekeza ile thread ifungwe kwani ilikuwa haina maslahi kwa jamii.

Ila pikipiki si usafiri wa kuamini sana kwenda umbali mrefu kama huo wa Dar -Dodoma, ni karibu KM 500.


Pole Bro Pascal, get well soon!
 
Binafsi napenda usafiri wa pikipiki,lakini ubaya wake body ni wewe mwenyewe;kuna mtu ameshangaa/ametilia mashaka kwa uwezekano wa kusafiri kwa pikipiki umbali mrefu kama huo wa Dar-Dom.

Ukweli ni kwamba inategemea na aina ya pikipiki yenyewe;kwasababu ninavyojua mimi kuna pikipiki za safari ndefu na zina kasi kuliko gari au sawa na gari.Nilikuwa Morogoro mwaka 2006 kuna jamaa wanatoka Zambia kuja Moro..kwa kutumia pikipiki.Na pikipiki hizi.

zinazotumika kwa safari ndefu huwa zinajulikana kama Cross country na nilizobahatika kuziona ni brand ya Mercedes Benz,BMW na mara nyingi utakuta hazitumii mnyororo bali zinakuwa na propeller shaft ndogo(fupi) ambayo haiwezi kulingana na ya gari.

Hivyo basi,sijui huyu ndugu yetu alikuwa na pikipiki ya vigezo vya kwenda safari ndefu au basi tu aliamua kulazimisha tu kwa utashi wake bila kuangalia vigezo vya manufacturer.

Lakini,hata hivyo na mpa pole sana na naomba mwenyezi Mungu amponye aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.
 
Huyu Pascal wamegongana uso kwa uso na mwendesha baiskeli alimwona anakatiza yeye akajua yupo mbali atamtime kabla haja pita ndio wakavaana.Hili ndilo tatizo la madereva wengi kufanya timing pasipo vipimo halisi.
 
Mimi nilikuwa addicted kwa motorbikes lakini ajali zilinilazimisha kuiacha. Hata leo kwa age yangu kubwa hivi bado naipenda lakini ajali ni ajali tu hata gari inapata ajali kwani mmeshasahau ya wiki mbili zilizopita?.
Pole Paschal Mungu atakusaidia upone.
T/C
 
pascal ni raia wa nchi yetu, hapa tunaelezwa kuwa aligongana na mwendesha baiskeli, sasa ni aje hapo? je huyu raia wa baiskeli amepona? nampa kwanza pole huyu wa baiskeli, na pili bwana pascal.

Ila nitaomba sheria ichukue mkondo wake, kwa kuwa haya mambo ya kugonga wapanda baiskeli maskini simply kwa kuwa unataka kufanya show off ya safari ndefu namna ile, labda uingie kwenye vitabu vya kumbukumbu kama ya christopher columbus pia hayaingii akilini.
 
Nakumbuka haijapita wiki tangu ile thread ya Pascal kuhusu kuendesha pikipiki isiyo na namba ijadiliwe hapahapa. Na wengi tulipendekeza ile thread ifungwe kwani ilikuwa haina maslahi kwa jamii..

Pikipiki ni usafiri mzuri tu lakini siyo safe kwa maana kwamba mwili wako hauna kingapindi ajari inapotokea. Dar na Dodoma ni karibu sana, watu wanasafiri kwa pikipiki toka California mpaka New york ( siku mbili masaa 48) iweje hapo masaa 3-5.
 
Huyu Pascal wamegongana uso kwa uso na mwendesha baiskeli alimwona anakatiza yeye akajua yupo mbali atamtime kabla haja pita ndio wakavaana.Hili ndilo tatizo la madereva wengi kufanya timing pasipo vipimo halisi.
Ukishafanya timing maana yake umeshapita pia...Mi nadhani hiyo ni ajali tu huwezi kujua huenda huyo mwenye baiskeli nae alijichanganya barabarani.

Get well soon Pascali!!!
 
Mdau Mpoki Bukuku wa Mwananchi na The Citizen anatujulisha kwamba Mwandishi wa siku nyingi na mtangazaji ambaye pia ni mjasiliamali ndugu yetu Pascal Mayalla amepata ajali mbaya ya pikipiki yake alipokuwa akisafiri kwenda mkoani Mkoani Dodoma.Bw Pascal Mayalla amepata majereha sehemu mbalimbali za mwili ikiwa namkono ambao umepoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili.JF hii inapenda kumpa pole ndugu yetu paschal Mayalla,apate Nafuu ya haraka.
View attachment 1939
View attachment 1940

Pole sana Mayala aka msimila those days Ilboru. Ulivyolala kama uko bwenini Oldonyo unasubiri kwenda kukamata chui la mzee akwii. Nitawasiliana na wasimila wote kuhusu hilo suala.

Wana JF samahani kidogo kwa lugha niliyotumia kama haieleweki kwenu. Hiyo ni lugha tuliyokuwa tunatumia pale Ilboru tukiwa na Mayala enzi zile.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom